Wednesday, March 6, 2013

Siri yavunjika kwa Kuvunjika kwa Ndoa ya Monalisa wa Siri ya Mtungi


SIRI ya kuvunjika kwa ndoa ya staa wa filamu Bongo, Yvonny Cherry ‘Monalisa’ imevuja ambapo imeelezwa kuwa tattoo aliyokuwa ameichora mkononi mwake yenye alama ya kopa na mshale ndiyo chanzo.
Akizungumza na Tollywood Newz jijini Dar es Salaam, Monalisa alisema: “Sikuwahi kuwaza hili hata mara moja. Siku moja Kanisani, Mchungaji aliniambia kwamba tattoo yangu ndiyo chanzo cha kunivurugia uhusiano wangu.

“Aliniambia kwamba, alama ya kopa ambayo humaanisha moyo – upendo, halafu mshale kupita katikati yake, humaanisha maumivu na kuteswa katika uhusiano. Lilikuwa jambo jipya kwangu lakini niliamua kufuta haraka sana na sasa nimeweka nyingine ya ua rose.” Source:Globalpublishers
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

No comments:

Post a Comment