Saturday, March 30, 2013

Katika hali ya kutatanisha Korea Kaskazini yatangza vita na Korea kusini.



 

Korea Kaskazini hii leo imesema inaingia katika hali ya vita na Korea Kusini, katika muendelezo wa vita vya maneno dhidi ya utawala mjini Seoul na Washington, baada ya kuwekewa vikwazo vya kimataifa kufuatia jaribio lake la silaha za nyuklia.

Shirika la habari la Korea Kaskazini KCNA, limetoa taarifa inayosema kuwa kuanzia sasa, uhusiano wa Kaskazini na Kusini utaingia katika hali ya vita, na kwamba maswala yote yanayojitokeza kati ya Kaskazini na Kusini yatashughulikiwa ipasavyo. 

Tangu mwanzoni mwa mwezi huu Korea kaskazini imekuwa ikitishia kila siku kuishambulia Korea kusini pamoja na kambi za kijeshi za Marekani, baada ya Marekani na Korea Kusini kuanzisha mazoezi ya kawaida ya kijeshi na imeyaamrisha majeshi yake kukaa kwa tahadhari.

Korea kaskazini imetoa kitisho kipya kuishambulia Marekani, baada ya ndege mbili za Marekani chapa B-2 zenye uwezo wa kubeba makombora ya nyuklia kufanya mazoezi nchini Korea ya Kusini.
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

No comments:

Post a Comment