Thursday, March 14, 2013

PAPA MPYA APATIKANA JANA USIKU!Moshi mweupe ulifuka katika mnarawa paa ya kanisa dogo la Sistina Vatican mjini Rome kuashiria papa mpya ameshapatikana.Hii ilikuwa jana usiku.
Maelfu ya watu walishangilia baada ya kupata ishara hiyo kuwa papa mpya ameshapatikana.Huku kengele za kanisa kuu la mtakatifu Petro na makanisa mengine huko Rome zilisikika.
Baada ya saa moja kupita ndio ikafahamika mrithi wa Papa Benedict wa xvi ni Askofu mkuu wa Buenos Aires nchini Argentina, Jorge Mario Bergoglio.
Papa huyu mpya amechagua jina la Papa Francis 1
Baadae alijitokeza kibarazani juu kuusalimia umati mkubwa wa watu.Papa mpya aliuomba umati huo kukaa kimyaa kwa muda kumuombea.''Naomba mniombee kwa Mungu ili anibariki''
Papa Francis amekuwa papa wa 266 mwenye miaka 76 papa wa kwanza asiyetoka barani Ulaya na watatu asiye muitaliano.
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

No comments:

Post a Comment