Friday, February 21, 2014

MATOKEO KIDATO CHA NNE 2013 ANGALIA HAPA (CSEE 2013 EXAMINATION RESULTS)


MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

Tuesday, February 11, 2014

HOT NEWS: VIDEO KUTOKA ITV NEWS(UINGEREZA) ILIVYO PELELEZA BIASHARA YA PEMBE ZA NDOVU INAVYO FANYIKA TANZANIA, WACHUKUA VIDEO YA WAUZAJI BILA WAO KUJITAMBUA. TAZAMA


Timu ya kituo cha runinga cha Uingereza cha ITV News imefanya upepelezi katika soko la uuzaji wa pembe za ndovu nchini Tanzania kuonesha jinsi ilivyo rahisi kunununua bidhaa hiyo haramu.
 
Akijifanya kama mfanyabiashara kutoka China, mwandishi wa kituo hicho alizungumza na wafanyabiashara wa pembe hizo na kumhakikishia kuwa anaweza kupata oda yake pembe za ndovu sita ndani ya wiki mbili baada ya wao kuingia msituni na kwenda kuua tembo.
The team is offered more products on condition they remain “discreet”

Our team enters a market stall and asks about buying ivoryTimu ya ITV News ikiwa kwenye kibanda chenye wafanyabiashara wa pembe za ndovu ambao kwa nje wanaonekana wakifanya biashara ya vinyago na bidhaa zingine za mikono
Kamera zilizokuwa zimefichwa ziliwarekodi wauzaji hao wakiahidi kuisaidia timu hiyo kusafirisha pembe hizo kwenda nchini China.
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

HUU UNYAMA GANI HUU JAMANI MTOTO ALIYETAFUNWA USO NA BABA YAKE SASA NI MATESO.


 
Stori: Jelard Lucas na Makongoro Oging’

SUSULUKA Imani Paul, kijana mwenye umri wa miaka 18, ambaye Novemba mwaka jana alikutana na unyama wa aina yake, baada ya kutafunwa sehemu kubwa ya uso wake maeneo ya mdomoni, analia kutokana na mateso makubwa yanayotokana na maumivu ya mwili pamoja na ukosefu wa fedha za matibabu na mahitaji.

Susuluka, mkazi wa Kijiji cha Nyabibuye Kakongo, wilayani Kibondo mkoani Kigoma, alijeruhiwa vibaya kwa kutafunwa usoni na baba yake mzazi, Imani Paulo (36) kwa kung’atwa kisha kunyofolewa macho, pua na meno kubaki nje.

Inadhaniwa kuwa wakati wa tukio hilo, baba yake mzazi alikuwa hana akili za kawaida na inadaiwa kuwa hadi sasa bado anashikiliwa na polisi huku uchunguzi zaidi wa tukio hilo ukifanywa.

Kwa sasa, kijana huyo ambaye anadai kuishi katika mazingira magumu kutokana na kukosa kwake fedha za kujikimu, yupo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili akitibiwa.

“Nateseka sana, inaniuma sana, baba yangu mzazi alinitafuna uso mzima, kwa sasa sina cha kuniokoa katika maisha, fedha za kwenda India sina japo serikali imeahidi kunipeleka, lakini natakiwa kuwa na fedha za kujikimu kama shilingi milioni 1.8, hizo zitasaidia kupata vibali vya kusafiria na mahitaji binafsi, naomba Watanzania waokoe maisha yangu,” alisema Sululuka ambaye anatarajiwa kupelekwa India na serikali hivi karibuni.

Awali taarifa za kijana huyu zilieleza kuwa alikuwa ametafunwa na mwajiri wake lakini sasa ameamua kufunguka kwa madai kuwa aliogopa baba yake angekamatwa na polisi.
Kama umeguswa na kilio cha kijana huyu wa Kitanzania, mchangie ulichonacho na Mungu atakupa baraka zake na ili aweze kujikimu na hata kumsaidia kwa matibabu kwa namba zifuatazo.

Tigopesa 0653715400 na M-Pesa 0768454656.

SOURCE:GBL
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

MAMA YAKE RAMBO MWENYE MIAKA 92 AFANYIWA UPASUAJI WA SURA NA KUONEKANA MREMBO WA MIAKA 25,MUONE HAPA


Mama wa star wa filamu na kipenzi cha wengi duniani muigizaji  Sylvester Stallone aka Rambo
ameonekaha hivi karibuni akiwa na muonekano tofauti na kwamba kafanya kila jambo kukimbia uzee.
Mama huyu mwenye miaka 92 amefanyiwa Upasuaji Wa Kubadili Sura sura na kuwa na muonekano wenye mvuto zaidi.
rambo 2rambo 3rambo 4rambo
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

SUGU: CHADEMA ITACHUKUA NCHI


 
 
UCHAGUZI mkuu wa Rais, wabunge na madiwani chini ya mfumo wa vyama vingi nchini, utafanyika kwa mara ya tano mwakani, huku kwa mara ya kwanza, chama tawala, CCM kikihofu kukutana na upinzani mkali, pengine kuliko wakati mwingine wowote.

Hofu hii, haitokani na kufanya kwake vibaya katika utekelezaji wa Ilani yake ya Uchaguzi iliyoipatia ushindi uchaguzi uliopita, bali kikubwa, ni kukubalika kwa vyama vya upinzani, hasa Chadema, ambacho kwa sasa ndicho kinaongoza Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni.

Kuelekea uchaguzi huo mkuu, safu hii ilifanya mahojiano na Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Simon Mbilinyi maarufu kama Sugu, ili pamoja na mambo mengine, kuelezea mtazamo wake juu ya tukio hilo kubwa kabisa kisiasa nchini.
Swali: Sisi tulio nje ya Chadema, tunafahamu kuna mgogoro mkubwa ndani ya chama chenu, wewe uko ndani, unaweza kutueleza kwa kifupi kilichopo?

Sugu: Hakuna mgogoro wowote ndani ya Chadema, kilichopo ni kwamba mwanachama mmoja na kiongozi alikiuka maadili, vikao vikamjadili na uamuzi ukachukuliwa. Chadema inajiandaa kuchukua nchi, lazima tuonyeshe kwa vitendo kwamba tukiwa pale, maadili ni kitu muhimu kabisa, lazima tutoe kibanzi ili kuwa tayari kuiona boriti.

Sisi siyo kama CCM, wanaogopana, hawawezi kuchukua hatua. Tumefika hadi vijijini ambako wanasema hatufiki, umati wa watu wanaokuja kutusikiliza unaonyesha wazi hakuna mgogoro, ni uamuzi tu ambao hata hivyo mjadala wake ulishafungwa.

Swali: Unamzungumziaje Zitto Kabwe, nadhani alikuwa mmoja wa vijana walioku-impress kuingia katika siasa.

Sugu: No, Zitto siyo, mimi nilikuwa impressed zaidi na Mnyika (John).

Swali: Jeuri ya Chadema kuamini kwamba itachukua nchi mwakani inatokana na nini?
Sugu: Siyo jeuri, bali ni hali halisi. Kwanza CCM imeishiwa mbinu na taifa liko tayari kwa mabadiliko.

Kinana (Abdulrahman, Katibu Mkuu, CCM) na Nape (Nnauye, Katibu wa Itikadi, CCM) wanaenda kwa wananchi wanawasaidia kupalilia mazao yao (kicheko), hii ni dhahiri kwamba hawajui mahitaji yao, wakulima hawahitaji kusaidiwa kupalilia, wao walitakiwa kuwaeleza CCM ina mpango gani kuhakikisha mbolea inawafikia kwa wakati na bei muafaka, wasichokijua ni kwamba wanapokwenda kwa staili ile wanawaongezea hasira.

Jambo jingine ni kuwa taifa lipo tayari kwa mabadiliko. Kote tunakopita, wananchi wanaonekana kabisa kuhitaji mabadiliko, tunafika hadi katika maeneo ambayo hata gari halijawahi kufika, wanapotuona sisi tumekwenda na helikopta, wanasema kama nyinyi mmeweza kuleta ndege, basi hata uwanja wake tutapata.
Nchi imeiva mzee, ni muda tu, ukichanganya na haya mambo ya CCM kuogopana kuchukuliana hatua, ukichukulia na muda uliobaki, njia ni nyeupe kwa Chadema kuichukua nchi.

Angalia, sisi tupo 49 tu bungeni, lakini tunatoa hoja ambazo zinakubalika na kufanyiwa kazi, zile zinazokataliwa, tunawapelekea wananchi na wao wanatuelewa, ndiyo maana mara nyingi tumetoka bungeni na kuwafuata wananchi kuwaeleza ndipo serikali inakubali. Wewe mwenyewe ni shuhuda wa jinsi serikali ilivyobadili mambo mengi baada ya sisi kutoka bungeni na kuwashtakia kwa wananchi.
Swali: Ni ugumu gani unafikiri utawakabili mkijiandaa kuichukua nchi?
Sugu:  Hakuna ugumu, CCM imekwisha, ukiangalia mpasuko wao na muda uliobaki, hakuna ugumu kabisa. Kitu cha msingi ni uboreshwaji tu wa daftari la wapiga kura, vijana wajiandikishe kwa wingi, ingawa siwadharau pia akina mama kwa sababu pale Mbeya ni mtaji wangu mkubwa sana.
Swali: Ukiwa Mbunge, unadhani malengo yako yametimia kwa asilimia ngapi?
Sugu: Ni zaidi ya asilimia 90 na mengine yamezidi 100. Nilichoahidi kukifanya mimi kama mimi nimefanikiwa kwa asilimia 90, mengine niliahidi kusimamia na kufuatilia, haya yamezidi sana. Nape alikuja Mbeya anawaambia watu kuwa eti lile jimbo ni la CCM, na mimi ni mpangaji tu.

Nataka nimwambie kuwa mimi ni kama Mpemba au Mkinga, nimekuja Kariakoo nikakuta jengo chakavu, nikalipiga chini (kubomoa) na kujenga ghorofa, ninao uwezo wa kuwapangisha niliowakuta na ndicho kilichopo Mbeya.

Swali: Utagombea tena Ubunge mwakani?
Sugu: Yaaa, nitagombea, lakini sisi hatuzungumzii sana ubunge, tunazungumzia Halmashauri, tunataka kuchukua halmashauri, pale ndiyo kila kitu.
Swali: Unauzungumziaje msimamo wa Chadema wa serikali tatu katika Katiba mpya tunayoelekea kuipata?
Sugu: Tunataka watu waelewe kuwa Chadema haina msimamo katika hili, sisi tunafuata matakwa ya wananchi, wananchi wametaka serikali tatu na Warioba (Joseph, Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba) ambaye ni CCM, aliwasilisha maoni ya wananchi, alisema asilimia 61 wametaka serikali tatu, sasa kwa nini useme msimamo wa Chadema, tunataka matakwa ya wananchi yazingatiwe kwa sababu hiyo ni katiba yao
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

Sunday, February 2, 2014

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI FEBRUARY 02, 2014






.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

Namna Jokate alivyom-surprise Wema On Stage Arusha.


IMG-20140202-WA0012
Unaweza kujikuta ukishindwa kuielewa hii hali lakini inabidi ukubaliane na ukweli halisi wa hiki kilichotokea,Jokate na Wema historia yao ilianzia kwenye shindano la kumtafuta Miss Tanzania 2006 ambapo Mshindi alikua ni Wema Sepetu akifatiwa na Jokate kisha mshindi wa tatu akiwa Lissa Jensen.
2006
Headline zilikuja kutengenezwa tena zikiwahusisha warembo hawa kuonekana wako na mtu mmoja ambapo magazeti mengi yaliandika mahusiano haya  yaliyokua yakimhusu Diamond Platnumz kutoka na warembo hawa.
IMG-20140202-WA0009
Kimepita kimya kirefu sana juu ya hawa watu wawili hadi usiku wa February 01 huko Arusha kwenye Tamasha la Divaz Night Endless Fame ambalo ndani yake kulikua na mastar kadhaa akiwemo Wema Sepetu,Aunt Ezekiel,Martin Kadinda,Kajala,Zamaradi Mketema,Chid Benzi,Mirror,Jordan na wengine kibao.
IMG-20140202-WA0011
Wakati Madam Wema Sepetu akimwaga mauno kwenye jukwaa bila kutegemewa na mtu yoyote Jokate alipanda Jukwaani na kuanza kumtunza Wema pesa na wakati huo Wema alikua akicheza Wimbo wa Diamond My Number One ‘Ngololo’ ambapo Jokate aliungana na Wema kuucheza Wimbo huo.
IMG-20140202-WA0008


MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

Saturday, February 1, 2014

HABARI PICHA: MAJANGA OMMY DIMPO ACHEZEA WASICHAN JUKWAANI KWA STAILI ZA XXX...




MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

BAADA YA KUWA MCHUNGAJI, MASANJA KANUNUA GARI KALI NA KWA SASA ANATEMBEA NA BOARDGURDS WAWILI



PICHA YA JUU AKIWA KWENYE GARI LAKE
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.