Tuesday, February 11, 2014

HUU UNYAMA GANI HUU JAMANI MTOTO ALIYETAFUNWA USO NA BABA YAKE SASA NI MATESO.


 
Stori: Jelard Lucas na Makongoro Oging’

SUSULUKA Imani Paul, kijana mwenye umri wa miaka 18, ambaye Novemba mwaka jana alikutana na unyama wa aina yake, baada ya kutafunwa sehemu kubwa ya uso wake maeneo ya mdomoni, analia kutokana na mateso makubwa yanayotokana na maumivu ya mwili pamoja na ukosefu wa fedha za matibabu na mahitaji.

Susuluka, mkazi wa Kijiji cha Nyabibuye Kakongo, wilayani Kibondo mkoani Kigoma, alijeruhiwa vibaya kwa kutafunwa usoni na baba yake mzazi, Imani Paulo (36) kwa kung’atwa kisha kunyofolewa macho, pua na meno kubaki nje.

Inadhaniwa kuwa wakati wa tukio hilo, baba yake mzazi alikuwa hana akili za kawaida na inadaiwa kuwa hadi sasa bado anashikiliwa na polisi huku uchunguzi zaidi wa tukio hilo ukifanywa.

Kwa sasa, kijana huyo ambaye anadai kuishi katika mazingira magumu kutokana na kukosa kwake fedha za kujikimu, yupo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili akitibiwa.

“Nateseka sana, inaniuma sana, baba yangu mzazi alinitafuna uso mzima, kwa sasa sina cha kuniokoa katika maisha, fedha za kwenda India sina japo serikali imeahidi kunipeleka, lakini natakiwa kuwa na fedha za kujikimu kama shilingi milioni 1.8, hizo zitasaidia kupata vibali vya kusafiria na mahitaji binafsi, naomba Watanzania waokoe maisha yangu,” alisema Sululuka ambaye anatarajiwa kupelekwa India na serikali hivi karibuni.

Awali taarifa za kijana huyu zilieleza kuwa alikuwa ametafunwa na mwajiri wake lakini sasa ameamua kufunguka kwa madai kuwa aliogopa baba yake angekamatwa na polisi.
Kama umeguswa na kilio cha kijana huyu wa Kitanzania, mchangie ulichonacho na Mungu atakupa baraka zake na ili aweze kujikimu na hata kumsaidia kwa matibabu kwa namba zifuatazo.

Tigopesa 0653715400 na M-Pesa 0768454656.

SOURCE:GBL
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

No comments:

Post a Comment