Saturday, September 6, 2014

MAALIM SEIF APATA AJALI MBAYA MKOANI MWANZA: ALIKUWA ANAELEKEA KWENYE AJALI ILIYOTOKEA MARA JANA


Gari aliyokuwa amepanda MAALIM SEIF ikiwa imeharibika vibaya Na Karoli Vinsent
Habari zilizotufikia mda huu Zinasema MSAFARA wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na Katibu Mkuu Taifa wa Chama cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad umepata Ajali mbaya  Mkoani Mwanza na kupelekea Viongozi mbalimbali wa Chama hicho kuwa na hali mbaya.       
Vilevile Mkurugenzi huyo wa Habari wa Chama hicho alisema kwa sasa Majeruhi hawo wamekimbizwa kwenye Hospitali ya Bugando kupatiwa matibabu na hali yao inaendelea vizuri isipokuwa Katibu chama cha Cuf kutoka Wilaya ya Nyamagana Rehema Mwenda hali yake sio Nzuri kutokana na kupoteza Fahamu,
Mkurugenzi wa habari wilaya'na MH SHIDO Ambae ni mwenyekiti wa serikal ya mtaa uliyopo kata ya miringo,wameumia vibaya wamelazwa hospitali ya BUGANDO
    Akithitisha kutokea kwa Ajali hiyo wakati anaongea na Mwandishi wa Mtandao huu, mda huu kwa njia ya simu kutoka Mkoani Mwanza kwenye Ajali hiyo, Naibu Mkurugenzi wa Habari kutoka Chama cha Wananchi CUF bwana Kambaya alithibitisha kutokea kwa Ajali hiyo na kusema Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Maalim na Katibu Mkuu Taifa wa Chama cha Wananchi (CUF) Seif Sharif Hamad  ajadhurika na yuko salama bali waliodhurika na Ajali hiyo ni viongozi wa chama hicho,
Rehema Mwendaalikuwa kwenye msafara huo aiugulia maumivu
“Ni kweli Msafara wa Makamu wa rais na Katibu mkuu Taifa umepata ajali ila yeye yuko salama,lakini viongozi wetu wa chama akiwemo katibu wa Chama cha Wananchi CUF  Wilaya ya Nyamagana Be Rehema Mwenda Pamoja na Mkuu wa Kitengo cha cha Habari wa chama Chetu wilaya ya nyamagana Hassan Shido  ndio wamepata majeraha kutokana na Ajali hiyo,”alisema Kambaya.

Kambaya alizidi kusema Ajali imetokana na Dereva wa Gari aina Scania kwenda kuligonga  Gari lilokuwa limewabeka viongozi hao,ambapo gari hilo  lilikuwa la nne kutoka gari  lililombeba Maalim Seif  kwenye msafara huo,
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

Tazama Picha za Ajali Mbaya Ambayo Haijawai Kutokea Musoma,Na Kusababisha Fiesta Kuahirishwa Mkoani Hapa







Ni ajali mbaya kuwahi kutokea katika mkoa wa Mara...Ni ajali iliyotokea leo asubui mida ya saa nne asubuhi ambapo basi la J4 lilokuwa likitoka Mwanza kwenda tarime limegongana uso kwa uso na basi la Mwanza Coach ambalo lilikuwa likitoka Musoma likienda Mwanza.

Chanzo cha ajali hiyo ni gari ndogo aina ya Land Cruiser ambayo ilikuwa ikiovatek bas la J4 ndipo baada ya kupoteza uelekeo kwenye kona ilioko maeneo ya sabasaba %ziro ziro% na kuacha mwanya wa basi hizo mbili kupoteza uelekeo na kugongana uso kwa uso.

Mpaka kufikia sasa watu waliofariki katika ajali hiyo ni 70 ambapo bas la J4 limeuwa abiria wote na majeruhi wa mwanza coach ni wengi pia.

Mungu zilaze mahali pema roho hizo
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.