Tuesday, October 30, 2012

13 WAFARIKI KUTOKANA NA KIMBUNGA SANDY



Mojawapo ya vimbunga vikubwa zaidi kuwahi kupiga Mashariki mwa Pwani ya Marekani kimesababisha mafuriko makubwa katika baadhi ya sehemu za mji wa New York.
Maeneo mengi mjini yamewachwa katika giza baada ya huduma za umeme kukatizwa.
Kimbunga hicho kilipiga ardhi kwenye Pwani ya New Jersey karibu na mji wa Atalanta muda mfupi jana usiku/Dhoruba kali kutoka mjini Florida hadi nchini Canada imepiga Mashariki mwa Marekani na kusababisha mawimbi makali mjini New York.
Maji yamefurika kwenye barabara na katika njia za reli pamoja, maeneo ya kuegesha magari na katika eneo la Ground Zero, eneo ambalo mashambulizi ya Septemba kumi na moja yalitokea.
Sehemu kubwa za mji wa New York ziko kwenye giza baada ya milingoti ya umeme kuharibiwa.
Wagonjwa waliondolewa kwenye hospitali moja baada ya umeme kukatika.
Zaidi ya watu milioni tano walisemekana kukosa umeme katika eneo la Pwani baada dhoruba kali huku takriban wengine milioni moja wakishauriwa kuhama nyumba zao. Athari za kimbunga hicho labda huenda zikajulikana baadaye leo.

VIA: bbc Swahili
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

SAJUKI AWASHUKURU SANA WATANZANIA KWA MICHANGO NA DUA ZAO, NA SASA AREJEA KATIKA HALI YAKE YA KAWAIDA



Ni kitambo sasa  tangu kuwepo kwa taarifa kuwa staa wa Bongo Movie, Juma Kilowoko, 'Sajuki' ni mgonjwa , huku pia taarifa za karibuni zikidai kuwa  hali ya  nyota huyo  bado ni tete na kuzua hofu kubwa kwa mashabiki wake.
Kupitia  mtandao huu  pekee taarifa rasmi ni kuwa hali nyota huyo kwa sasa  ni njema na  yuko tayari tena  kuanza kuwatumikia  watanzania  kupitia tasnia ya  filamu.
Kwenye Exclusive interview aliyofanya na mtandao huu  mapema leo Sajuki amewashukuru watanzania  kwa kuwa pamoja nae kwenye wakati wote wa  matatizo  mpaka sasa  anajisikia yuko vizuri tofauti na ilivyokuwa awali.
Nashukuru kuwa  sasa niko poa, watanzania  waelewe hilo, kwa sasa  naweza hata kuendesha gari na karibuni nitaanza  kucheza muvi tena  alisema Sajuki.
katika kuonyesha kuwa anathamini i mchango wa Watanzania Sajuki ameachia ngoma ambayo ameamua kuipa jina la Shukurani
 
VIA:suleimanmagoma.blogspot.com
    
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

Sunday, October 21, 2012

Ommy Dimpoz amkamata Lord Eyes akiiba Power windows na vifaa vingine vya gari yake.


Jioni ya leo Ommy dimpoz kupitia akaunti yake ya twitter ametweet kwamba amemkamata rapper wa Nako 2 Nako Lord eyes akiiba vifaa vya gari yake ikiwa ni pamoja na Power windows. Jionee mwenyewe picha alizoweka Ommy dimpoz pamoja na tweets zake.

Jionee picha mwenyewe.

Lord Eyes kwenye eneo la tukio






Ommy aliongeza kuwa Lord amekuwa akifanya mchezo huo kwa watu wengi akiwemo jamaa mmoja wa Clouds anaefahamika kwa jina la Kerry ambae pia amemfanyia mchezo huo siku za karibuni.


VIA: suleimanmagoma.blogspot.com
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

Friday, October 19, 2012

SALAAM ZA MAASKOFU WA KKKT KWA WATANZANIA WOTE KUHUSIANA NA MATUKIO YA KUCHOMA MOTO MAKANISA YA KIKRISTO ENEO LA MBAGALA – DSM.





SALAAM ZA MAASKOFU WA KKKT KWA WATANZANIA WOTE KUHUSIANA NA MATUKIO YA KUCHOMA MOTO MAKANISA YA KIKRISTO ENEO LA MBAGALA – DSM. 

Wapendwa Katika Bwana, Waumini wa KKKT, Wakristo Wote na Watanzania kwa Ujumla. Neema na Iwe kwenu na amani itokayo kwa Mungu Baba na Bwana wetu Yesu Kristo, Amina. 
Sisi maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), tumepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za matukio ya uchomaji wa makanisa katika eneo hili la Mbagala. Tumekuwa katika mkutano wetu wa Mwaka wa Lutheran Mission Cooperation (LMC) huko Moshi pamoja na vyama vyote vya Kimissioni vya Ulaya na Marekani. Tumelazimika kukatisha mkutano huo ili kufika hapa Mbagala. Tumekuja kwa madhumuni makubwa matatu: Tumekuja kuwapa pole na kusimama pamoja nanyi katika uchungu mkubwa mlio nao. Machozi yenu ni machozi yetu. Machozi yetu ni machozi ya Kristo mwenyewe aliye Bwana wa kanisa linaloteswa. Jipeni moyo kwa kuwa yeye aliushinda ulimwengu (Yohana 16:33). 

Tumekuja kuonyesha majonzi yetu makubwa kwa vitendo vya uvunjifu wa amani, kuporomoka kwa umoja na mshikamano wa watanzania. Huu ni msiba mkubwa, na wenye msiba ni watanzania wote, wenye dini na wasio na dini. Tumekuja kushiriki pamoja nanyi kupokea matumaini ya Tanzania mpya. 

Katika majivu haya yaliyotokana na kuchomwa kwa madhabahu ya Mbagala, Tanzania mpya itazaliwa. Majivu haya na machozi yenu ni rutuba ya Tanzania mpya itakayojali upendo, uvumilivu, ustahimilivu, umoja, mshikamano, uhuru wa kuabudu na dola isiyo na dini. Katika ujio huu wa maaskofu hapa Mbagala, hatukuja hapa kufanya haya yafuatayo:

Hatukuja kuwahukumu hata kama hatukubaliani na wanaokashifu dini za wenzao, wawe na ruhusa kutoka mamlaka zilizo juu au kama wanajituma wenyewe. Hatukuja kuwahukumu hata kama hatukubaliani na wanaodhalilisha misahafu ya dini; wawe wametumwa, kutegeshewa na mamlaka zozote au kwa misukumo ya utashi wao binafsi ili kupata kisingizo cha kugombanisha madhehebu ya dini. Hatukuja kuwahukumu hata kama hatukubaliani na wanaochoma makanisa na kuiba mali za makanisa kwa kisingizio cha kumtetea Mungu. Kisasi cha dhambi hiyo tunamwachia Mungu mwenyewe aliyedhihakiwa na walionajisi madhabahu yake. 

 Wapendwa wana KKKT na watukuka sana, wana na mabinti wa Tanzania ya Julius Kambarage Nyerere; kilichotokea Mbagala katika wiki ya kuadhimisha siku ya Baba wa Taifa, ni kebehi si kwa Baba wa Taifa bali ni kebehi kwetu sisi wenyewe tunaokalia kiti alichokalia Baba wa Taifa. Yeye amelala baada ya kazi njema. Apumzike kwa amani na tunu zake zifufuke katika majivu haya yaliyotokana na kuchomwa kwa amani na mshikamano wa Tanzania aliyoijenga. Kilichotokea Mbagala ni mateso ya kimbari, yaani mateso ya Kanisa (Persecution). Mateso haya ni matokeo ya mbegu ya magugu iliyopandwa katika bustani njema na sasa magugu hayo yanazaa matunda machungu. 

Dalili za mateso ya kimbari kama ilivyo kwa mateso ya kanisa; zilianza kitambo na hazikushughulikiwa na waliomrithi Baba wa Taifa. Dalili hizo ni kama hizi zifuatazo: Uchochezi wa wazi kuwa taifa hili linaendeshwa na unaoitwa “mfumo Kristo”, na kuwa Baba wa Taifa alaaniwe kwa yote aliyolitendea taifa hili. Ubishi usio na tija juu ya idadi ya waumini wa dini mbalimbali hapa nchini na hata kudiriki kushawishi na kugomea zoezi la sensa ya watanzania. Lengo la ubishi huu ni mbegu inayoweza kuratibisha na kurasmisha mateso ya kimbari na mateso ya kanisa. Matumizi mabaya ya baadhi vyombo vya habari, vyenye lengo la kujenga hofu ya kudumu na migawanyiko ya kidini miongoni mwa watanzania Ukimya wa vyombo vya dola juu ya vitendo vya uvunjaji wa sheria ya matumizi ya vyombo vya habari. Kwa vyovyote vile, uvumilivu wa dola hauna maslahi mapana kwa mustakabali wa taifa letu na ni mateso ya kimbari, mateso kwa kanisa, na kwa wantanzania wote; wawe wengi dhidi ya wachache au wachache dhidi ya wengi. Madai yasiyo ya kawaida na ya mara kwa mara kwa serikali inayodaiwa kutokuwa na dini. Madai hayo ni kama: Kulazimisha uvaaji wa alama za kidini katika taasisi za umma ili kurahisisha na kuratibisha tofauti za watanzania. 

Tunajiuliza: Likitokea la Mbagala katika mashule yetu na vyuo vya umma, watachomwa wangapi na kuuawa wangapi? Madai yanayojirudiarudia kutaka balozi za nchi fulani kufungwa hapa nchini. Madai haya yanaashiria kutaka balozi za nchi fulani tu ndiyo ziwe hapa nchini. Madai na mashinikizo ya Uanzishwaji wa mahakama za kidini hapa nchini Mashinikizo ya kidini yanayoingilia mifumo ya kitaaluma na kisheria. Mashinikizo ya kidini juu ya mfumo wa uteuzi wa watendaji wa serikali na katika ofisi za umma, Kuhoji na kupotosha juu ya ushirikiano wa serikali na mashirika ya dini katika utoaji wa huduma za kijamii hususan afya na elimu hapa nchini Wapendwa wana KKKT na Wapendwa watanzania wote. Hata kama wanaofanya mambo haya ya kusikitisha wametunukiwa hadhi ya kuitwa kuwa ni “wana harakati”, tofauti na wanaharakati wanaotambuliwa na watanzania walio wengi, tunawiwa kuonya kwa uvumilivu wote kuwa uana harakati wao usitumike kuvunja nchi na sheria za nchi.

 Tanzania yenye amani na mshikamano ni tunda la dini zote, makabila yote, itikadi zote za vyama, rangi zote na hali zote za kiuchumi. Hata wasio na dini wanachangia amani ya nchi hii. Kwa macho na masikio yetu, tumeendelea kushuhudia vitendo vya uchomaji makanisa huko Zanzibar, Mwanza, Mdaula, Mto wa Mbu, Tunduru, Rufiji, Kigoma na sasa Mbagala. Wakati wote uvumilivu wa wakristo huenda umetafsiriwa kuwa ni unyonge na woga. Ikumbukwe kuwa hata wanyonge na waoga, hufika wakati wakasema “sasa basi” pale wanapodhalilishwa kupita kiasi. Hatuombei wakristo wafikishwe hapo. 

Tumeshuhudia wizara zetu zikivamiwa mchana kweupe na kushinikiza kuachiwa kwa watuhumiwa wa uhalifu; tumeshuhudia vituo vya polisi vikichomwa moto; mahakama zikilazimishwa kufunga shughuli zake, misikiti ikitekwa, uhai wa viongozi wa dini ukitishiwa hadharani na viongozi wastaafu wakizabwa vibao hadharani kwa sababu ya zinazoitwa harakati za kidini.

 Tumefikia kuhoji, watu hawa wavamie nini ndipo hatua zichukuliwe? Wachome nini ndipo viongozi wenye dhamana ya kulinda mali na uhai washtuke? Wamwue nani ndipo iaminike kuwa watu hawa ni tishio kwa usalama wa taifa letu? Sisi tulioitwa kwa njia ya nadhiri na viapo vitakatifu, tunawasihi sana waumini wa dini zetu na watanzania kwa ujumla, wenye wajibu wa kututii na wasiolazimika kututii, kuzingatia kuwa Mwenyezi Mungu analipenda taifa hili na watu wake. Kamwe hawezi kuliacha liangamie.

 Kwa Wakristo wote, huu ni wakati wa kuendelea kufunga na kuomba kwa ajili ya amani ya taifa hili. Mkristo wa kweli ni yule aliye tayari kuteswa kwa ajili ya Kristo na kanisa. Wakristo hatuko tayari kuua, kutesa, kulipiza kisasi ili kumtetea Kristo. 

Mungu wetu hatetewi kwa kuua wengine na kuchoma madhabahu ya dini nyingine. Katika mateso haya, kanisa litaimarika zaidi; na katika majivu haya ya Mbagala, Tanzania mpya itazaliwa na ukombozi wa kweli utapatikana. 

Tunawataka wakiristo wote kusamehe na kuendelea kuwa raia wema. Kushiriki kikamilifu katika kuleta mabadiliko ya kweli kwa kupitia njia sahihi zilizowekwa. Wakati wengine wanaweka mikakati ya kuchoma madhabahu, wakiristo tuweke mikakati ya kuomba na kushiriki vema katika haki zetu za uraia. Pamoja na kuwa wapole kama njiwa, imetupasa pia kuwa na busara kama nyoka (Mathayo 10:16).
 Daima tukumbuke kuwa,


 “KUSHINDANA KWETU SISI SI JUU YA DAMU NA NYAMA BALI NI JUU YA FALME NA MAMLAKA, JUU YA WAKUU WA GIZA HILI, JUU YA MAJESHI YA PEPO WABAYA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO” (Waefeso 6: 12). 
               Ni sisi Maaskofu wenu kwa Neema ya Mungu
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

Thursday, October 18, 2012

JENIIFER KYAKA (ODAMA) KUSHUKA BONGO NA VIFAA VYA MOVIE


Kampuni ya J-Film 4 Life inapenda kuwajulisha kuwa sasa imeongeza vifaa vipya vya movie vyenye viwango vya kimataifa. Tegemeeni kupata movie katika quality ya hali ya juu sana kutoka J-Film 4 Life iliyoko Kinondoni Biafra Tanzania.

Kama wewe ni msanii wa Bongo Movie unakaribishwa katika kampuni yake ya kisasa.



Mkurugenzi wa J-Film 4 Life akichagua camera kali na za kisasa.

 Mmeona mambo haya!!!
 Kazi imepamba moto katika kuchagua stand maridadi kwaajili ya camera
 Duh hii kiboko!!!
 Mama yangu kazi imeanza..ni balaaaa!!!!
Unaionaje hii??

 Mhh!!

ANGALIA PICHA ZINGINE "Read More" HAPO CHINI
 Baada ya kuchagua saaaaana , nikaamua kupumzisha akili kwanza...!!!
 Duh hizi silaha au stand????
 Kazi imeanza sasa kutafuta Boom Mic ya ukweli, si unajua mambo ya sauti kwenye movieeeeee!!!
 Nikikagua Stick ya Boom
 Mhh!! Kazi ipo!!!
 Bei gani kwani??
 Iko poa!!!
 What?

SIKU YA PILI KAZI ILIENDELEA YA KUTAFUTA VIFAA  VINGINE BORA VYA MOVIE.
 Leo kazi ipo!!!
Baada ya zoezi zima kumalizika ukafika wakati wa kupata snaps za kumbukumbu

MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

Monday, October 15, 2012

MTAHINIWA KIDATO CHA NNE AFARIKI DUNIA


MTAHINIWA KIDATO CHA NNE AFARIKI DUNIA ROBERT SHAFT ALIKUWA MWANAFUNZI KIDATO CHA NNE MWAKA 2012 ALIKUWA BADO ANAFANYA MTHIANI WA KUHITIMU KIDATO CHA NNE MWAKA 2012 AMEFARIKI TAREHE 09/10/2012 SIKU YA JUMANNE MWENYEZI MUNGU AILAZE ROHO YA ROBERT MAARA PEMA PEPONI "AMEN"
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

Wednesday, October 10, 2012

MKURUGENZI MKUU WA MSD ASIMAMISHWA KAZI.


 
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi akitoa ufafanuzi  kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu hatua zilizochukuliwa na Serikali kufuatia kubainika kwa matumizi ya dawa bandia za kupunguza makali ya Ukimwi zenye jina la Biashara TT –VIR 30.
Mmoja wa maafisa kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa Nchini (TFDA) ambaye hakutaka jina lake liandikwe kwenye vyombo vya habari akiwaonyesha waandishi wa habari Dawa badia za kupunguza makali ya Ukimwi (ARVS) zilizoondolewa katika vituo vya kutolea huduma mara baada ya kugundulika.
Makopo ya dawa za kupunguza makali ya Ukimwi yakitofautiana vifungashio. Kopo la kwanza kushoto linaonyesha dawa halisi  ya kupunguza makali ya Ukimwi iliyokidhi viwango ikifuatiwa na makopo 3 yenye dawa bandia ya kupunguza makali ya Ukimwi yenye jina la biashara TT –VR 30 toleo namba 0c.01.85  yaliyotengenezwa na kiwanda cha Tanzania Pharmaceutical Industries Ltd.(Picha na Aron Msigwa – MAELEZO).

Na. Aron Msigwa –MAELEZO.

Serikali imewasimamisha kazi mkurugenzi mkuu wa Bohari ya Dawa nchini (MSD) ,Mkuu wa kitengo cha Udhibiti na Ubora na Afisa Udhibiti Ubora wa ohari hiyo ili kupisha uchunguzi dhidi yao kufuatia kuruhusu kusambazwa kwa dawa bandia za kupunguza makali ya UKIMWI aina ya TT –VIR 30 katika vituo  mbalimbali vya kutolea huduma  za afya nchini.

Aidha imepiga marufuku usambazaji na matumizi ya dawa aina ya TT –VIR 30 toleo na 0C .01.85 inayotengenezwa na kiwanda cha Tanzania Pharmaceutical Industries Ltd (TPI) kufuatia dawa hiyo kutengenezwa chini ya kiwango na kutofaa kwa matumizi ya binadamu.

Akizungumza leo jijini Dar es salaam Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi amesema kuwa hatua hiyo imechukuliwa mara baada ya kubaini kuwepo kwa dawa bandia ya kupunguza makali ya Ukimwi katika hospitali ya wilaya ya Tarime kufuatia ukaguzi uliofanywa na Wizara ya Afya kupitia Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA).

Amesema kuwa ukaguzi na uchunguzi wa kimaabara dhidi ya dawa hiyo isiyokidhi viwango ulibainia kuwa nyaraka zilizopo kuhusiana na dawa hizo unaonyesha kuwa Kiwanda cha Tanzania Pharmaceutical Industries Ltd (TPI) waliiuzia Bohari ya Dawa (MSD) dawa hiyo bandia toleo namba 0C. 01. 85  iliyotengenezwa nchini mwezi Machi 2011 na kuonyesha mwisho wa matumizi yake mwezi Februari 2013.

Amefafanua  kuwa dawa hiyo bandia ilikua na dawa zenye rangi mbili tofauti njano na nyeupe na kuwa na viambata tofauti vilivyopaswa kuwepo aina ya Efaverenz badala ya Niverapine, Lamivudine na Stavudine na kuongeza kuwa vidonge vilivyokutwa kwenye vifungashio vya dawa husika vilikua tofauti na vifungashio vilivyosajiliwa na TFDA.

Dkt. Mwinyi amesema kuwa serikali inahakikisha kuwa dawa zenye ubora unaotakiwa za kupunguza makali ya UKIMWI zinaendelea kupatikana katika vituo vya kutolea huduma kote nchini na kuwaagiza waganga wakuu wa mikoa, wilaya  na kamati za dawa na Tiba katika vituo vya huduma za afya kuhakikisha kuwa zinapokea, kuhakiki na kusimamia kikamilifu ubora na matumizi sahihi ya dawa na vifaa tiba nchini.

Kuhusu upatikanaji wa dawa hizo amewatoa hofu wananchi  na kuwahakikishia  kuwa dawa za kutosha zenye viwango stahili zitaendelea kupatikana  katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini na kuwataka wananchi kutoa kushirikiana na mamlaka husika kwa kutoa taarifa pale wanapobaini kuwepo kwa dawa zenye ubora wenye mashaka au uvunjifu wa sheria inayosimamia ubora na usalama wa dawa.

VIA: MO BLOG
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

UCHAGUZI UVCCM ARUSHA VURUGU TUPU CHATANDA ANUSURIKA KICHAPO.


Picha Juu na Chini ni Baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa Uvccm mkoani Arusha kutoka wilayani Monduli wakiingia kwa mara ya pili  kupiga kura za kumchagua mwenyekiti wa umoja huo baada ya zoezi la awali kuvurugika katika ukumbi wa CCM mkoa.(picha na Mahmoud Ahmad-Arusha).
Mahmoud Ahmad Arusha
Hali ya tafrani imeibuka katika uchaguzi wa jumuiya ya umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi(Uvccm) mkoa wa Arusha baada ya katibu wa CCM mkoani hapa,Mary Chatanda kunusurika kipigo baada ya kutuhumiwa kuvuruga uchaguzi huo kwa lengo la kumpitisha chaguo lake ambaye alitajwa kuwa ni  ,Dk Harold Adamson.

Katika vurugu hizo  Chatanda alinusurika kipigo kutoka kwa wajumbe waliotoka wilayani ya Monduli baada ya kuamuru zoezi la uchaguzi huo lilirudiwe kwa madai kwamba wajumbe hao pamoja na wale wanaotoka wilayani Meru  idadi yao ilikuwa na kasoro.

Katika vurugu hizo makundi ya baadhi ya vigogo wa CCM hapa nchini yanyohusihswa na waziri mkuu mstaafu aliyejiuzulu,Edward Lowasa pamoja na Bernad Membe yalijidhihirisha waziwazi ambapo yalikuwa yakitambiana nje ya ukumbi wa mkutano.

Hatahivyo,katika hali isiyo ya kawaida polisi pamoja na maofisa wa usalama wa taifa waliwatimua waandishi wa habari waliokuwa nje ya ukumbi wa mkutano katika jengo la CCM mkoani hapa kwa amri ya katibu wa CCM wilaya kwa madai kwamba hawana mashati yenmye rangi ya kijani.
Zoezi la kupiga kura za uchaguzi wa nafasi ya mwenyekiti wa Uvccm mkoa lilianza majira ya saa 6;00 mchana ambapo upepo wa awali katika uchaguzi huo ulionyesha kwenda kwa mgombea,Robinson Meitenyiku anayetokea wilayani Arusha.

Vurugu hizo zilianza majira ya saa 9;00 mchana ambapo Chatanda alipoamuru wajumbe wa mkutano huo watoke nje ya ukumbi kwa madai kwamba kuna baadhi yao kutoka wilaya za Meru na Monduli walizidi.

Akitangaza uamuzi huo katibu huyo alisema kwamba wajumbe kutoka wilayani Monduli idadi yao haikuwa halali pamoja na ile ya wilayani Meru kwamba wajumbe watano walizidi kitendo kilichopingwa vikali.

Hatahivyo,mara baada ya wajumbe hao kutoka nje ya ukumbi wa uchaguzi walianza kupaza sauti kwamba katibu huyo analengo la kuvuruga uchaguzi huo kwa kuwa anataka kumpitisha mgombea wa nafasi hiyo,Dk Adamson.

Wakati vurugu hizo zikiendelea ndipo baadhi ya wajumbe kutoka wilayani Monduli walitishia kumchapa ndani ya ukumbi huo lakini juhudi zao zilizimwa na baadhi ya walinzi wakiwemo askari wa jeshi la polisi mkoani Arusha.

Mmoja wa wajumbe hao kutoka wilayani Monduli,Isaac Kadogoo alimwakia vikali Chatanda ndani ya ukumbi huo na kumtuhumu kwamba kitendo chake cha kukaa karibu na sanduku la kura kilikuwa na lengo la kutaka kuchakachua kura hizo.

“Mheshimiwa katibu rudi ukae meza kuu hata kama wewe ni msimamizi wa uchaguzi huu ondoka hapo kwenye sanduku la kura tuna wasiwasi na wewe”alisikika Kadogoo
Wakati hayo yakijiri nje ya ukumbi wa mkutano huo baadhi ya wajumbe walipinga kitendo cha Chatanda kuwatoa nje na kusema kwamba ana lengo la kuuvuruga uchaguzi huo ili chaguo lake lipite.

Hatahivyo,ilipotimu majira ya saa 9;15 mchana ndipo wajumbe hao walitangaziwa kurudi ndani ya ukumbi huo kwa lengo la kurudia zoezi la kupiga kura na ndipo walipojipanga kwa mistari na kuelekea katika ukumbi wa uchaguzi kupiga kura kwa mara nyingine.
Maofisa wa usalama wa taifa sanjari na askari wa jeshi la polisi mkoani Arusha walikuwa wakiranda randa nje na ndani ya  ukumbi wa mkutano kuimarisha ulinzi wakiwemo na baadhi ya maofisa wa Takukuru mkoani Arusha.

VIA: MO BLOG
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

TAREHE 10 MWEZI 10 NDO SIKU NILIYO ZALIWA NINA FURAHA KUISHEREKEA SIKU HII TENA


KWANZA NATOA SHUKRANI KWA MWENYEZI MUNGU KUNIFANYA NIMEIONA TENA SIKU YANGU NILIYO ZALIWA

NINAFURAHI NIKIANGALIA PICHA HII

INANIKUMBUSHA MBALI SANA KUMBE NDO NILIKUWA HIVI!!!!
SHUKURANI KWA MAMA YANGU MZAZI KWA KUNIPENDA KIPINDI CHOTE NILICHO KUWA  NAYE BI, MKUBWA

LKN MPAKA SASA MIAKA MINGI  ILIYO PITA:



THE KING
(MWARICK JUNIOR)

MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.