Tuesday, October 30, 2012

SAJUKI AWASHUKURU SANA WATANZANIA KWA MICHANGO NA DUA ZAO, NA SASA AREJEA KATIKA HALI YAKE YA KAWAIDANi kitambo sasa  tangu kuwepo kwa taarifa kuwa staa wa Bongo Movie, Juma Kilowoko, 'Sajuki' ni mgonjwa , huku pia taarifa za karibuni zikidai kuwa  hali ya  nyota huyo  bado ni tete na kuzua hofu kubwa kwa mashabiki wake.
Kupitia  mtandao huu  pekee taarifa rasmi ni kuwa hali nyota huyo kwa sasa  ni njema na  yuko tayari tena  kuanza kuwatumikia  watanzania  kupitia tasnia ya  filamu.
Kwenye Exclusive interview aliyofanya na mtandao huu  mapema leo Sajuki amewashukuru watanzania  kwa kuwa pamoja nae kwenye wakati wote wa  matatizo  mpaka sasa  anajisikia yuko vizuri tofauti na ilivyokuwa awali.
Nashukuru kuwa  sasa niko poa, watanzania  waelewe hilo, kwa sasa  naweza hata kuendesha gari na karibuni nitaanza  kucheza muvi tena  alisema Sajuki.
katika kuonyesha kuwa anathamini i mchango wa Watanzania Sajuki ameachia ngoma ambayo ameamua kuipa jina la Shukurani
 
VIA:suleimanmagoma.blogspot.com
    
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

No comments:

Post a Comment