Sunday, December 15, 2013

PICHA NA MATUKIO YA KUUWAWA KWA ALIYE KUWA M/KITI CCM MKOA WA MWANZA


MWILI WA ALIYEKUWA M.KITI CCM MKOA WA MWANZA. NDG. MABINA
ENEO LA TUKIO
ENEO LA TUKIO


BUGANDO AMBAKO MIILI IMEIFADHIWA
MABINA ENZI ZA UHAI WAKE.









MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

Breaking newsss!!!!!!!! ALIYEKUWA M/KITI WA CCM MKOA WA MWANZA AMEUWAWA NA WANANCHI


Breaking newsss tarifa iliyonifikia hivi punde toka magu aliyekuwa mwenyekiti wa ccm mkoa wa mwanza mwaka 2008-2012 ambaye pia ni diwani wa kata ya kisesa,na aliwahi kuwa mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya magu bwana clement mabina ameuwawa na wananchi wenye hasira Kali wananchi wa kisesa kwenye kata yake,inasemekana mabina aliwazurumu wananchi mashamba yao kwa nguvu na kuuza mashamba hayo kwa NCCF akidai mashamba hayo yakwake leo majira ya saa sita mabina alienda mashambani kwa ajiri ya kuweka mipaka kwenye hayo maeneo,baadaye wananchi wakazuia ndipo mabina akaanza kuwarushia risasi wananchi na kuua mwananchi mmoja na wengine wengi kuwajeruhi baada ya risasi kumwishia wananchi wakapiga mwano wakaanza kumfata na mapanga kupiga na kumwuua. ‘ Mungu azilaze roho zao (marehemu) mahali pema peponi’ .
KWA TAARIFA ZAIDI:
MWENYEKITI wa zamani wa chama cha mapinduzi(ccm) mkoa wa Mwanza Clement Mabina ambaye pia ni diwani wa kata ya Kisesa wilayani Magu mkoani Mwanza ameuawa na wananchi wenye hasira katika ugomvi wa mashamba.
Tukio la kuuawa kwa Mwenyekiti huyo wa Ccm Mkoa wa Mwanza ambaye alishindwa katika uchaguzi wa nafasi ya Mwenyekiti wa ccm mkoa wa Mwanza mwaka jana na Waziri wa zamani na Mbunge wa zamani wa Ilemela Dk Antony Diallo lilitokea leo asubuhi katika eneo la kijiji cha Kanyama wilayani Magu.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana na kuthibitishwa na Mkuu wa polisi wa wilaya(OCD) ya Magu ODC Mkapa pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Magu Desdery Kiswaga zimeeleza kuwa tukio limetokea majira ya saa mbili asubuhi.
ODC Mkapa alikiri kutokea kwa tukio la kupigwa na kuuawa kwa Mwenyekiti huyo wa zamani wa Ccm Mkoa na Mwenyekiti wa zamani wa Halmashauri ya wilaya ya Magu baada ya kutokea kutokuelewana baina yake na wananchi wa eneo la kijiji cha Kanyama alikokuwa na shamba lake alikokuwa amekwenda kupanda miti.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Magu Desdery Kiswaga alisema kuwa amepokea taarifa za kuuawa kwa kupigwa na wananchi wenye hasira kutokana na ugomvi wa mashamba na kuelezwa kuwa amesikitishwa sana na kuuawa kwa Mwenyekiti huyo wa zamani wa Halmashauri ya wilaya ya Magu.
Taarifa zaidi toka eneo la tukio la Kanyama kulikotokea mauaji hayo zimeeleza kuwa Mwenyekiti huyo wa zamani wa Ccm alifika katika eneo hilo majira ya asubuhi kwa ajili ya kupanda miti katika eneo la milima ya Kanyama ambalo analimiliki ambavyo hata hivyo linadaiwa kuwa na mgogoro baina yake na wananchi.
Baada ya kufika katika eneo hilo,wananchi nao walifika katika eneo hilo na kumhoji sababu za kupanda miti katika eneo hilo ambalo bado lina mgogoro wa umiliki na kutokea kutokuelewana baina yake na wananchi.
Baada ya majibishano ya muda mrefu na kuona wananchi wameanza kumzingira Mabina aliamua kufyatua risasi hewani kuwatawanya wananchi hao ambapo kwa bahati mbaya mojawapo ya risasi hizo zilimpiga mtoto aliyekuwa katika eneo hilo na kupoteza maisha.
Taarifa hizo toka katika eneo hilo la tukio zimeeleza kuwa kutokana na tukio hilo wananchi walimzingira Mabina na kuanza kumpiga kwa silaha mbalimbali za jadi kama vile mapanga, fimbo, mawe, mikuki na kusababisha kifo chake papo hapo.
Kabla ya kurejea chama cha mapinduzi(ccm) na kufanikiwa kuwa diwani wa Kata ya Kisesa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Magu, Mabina aliwahi kuwa mwanachama wa chama cha NCCR-Mageuzi na aligombea nafasi ya Ubunge katika jimbo hilo mwaka 1995 na kushindwa na aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Malaki Lupondije.


MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

Tuesday, November 26, 2013

DIAMOND ATANGAZA AJIRA KWA VIJANA.. ANGALIA AJIRA ALIZO TANGAZA HAPA!!


 
 Je unaishi Dar-es-Salaam..? Unakipaji, Uwezo na Elimu ya kupiga picha, kushoot Video na kuedit...?

NOTE:-
1)Uwe na Uwezo wa kutumia Camera zote Old na za kisasa....
2)Uwe na sample za kazi kadhaa ulizowai fanya... (kushoot na

Kuedit)
3)Quality ni kuanzia 1080 na kuendelea...
4)Age, kuanzia Miaka 20 hadi 35..
5)M'bunifu, Smart na uwe tayari kusafiri popote saa yoyote...

Kama unaamini unasifa hizo wasiliana nasi sasa kwa email hii diamondplatnumz@gmail.com ama kwa namba ya simu +255755700400
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

Watoto waeleza walivyotekwa na kulawitiwa na wazungu katika handaki Kinondoni, Dar


Zaidi ya watoto 60 wanadaiwa kutekwa na kufichwa katika handaki lililopo kwenye msitu wa Mabwepande, Wilaya ya Kinondoni , Dar es Salaam, ambalo ndani yake kuna jengo kubwa lenye vyumba.

Utekaji huo unadaiwa kufanywa na raia wa kigeni (Wazungu), wakishirikiana na Watanzania ambapo watoto hao hufungiwa katika vyumba hivyo, kuteswa, kulawitiwa na kubakwa.

Mtoto Emmanuel Robert (11) anayesoma darasa la tano Shule ya Msingi Maendeleo iliyopo Tabata, Segerea, Dar es Salaam na mdogo wake Godianus Robert (8), anayesoma darasa la tatu shuleni hapo, ndio waliofichua ukatili huo mwishoni mwa wiki.

Watoto hao walitekwa na Wazungu w awiliasubuhiyaSeptemba2mwaka huu, wak ati wakiendas huleni n akufan ikiwa
 kutoroka katikaj engohiloSeptemba 23 mwaka huu.

Wakiwa wamechoka na afya zao kuzorota katika Kituo kidogo cha Polisi, Kibaha Maili Moja, mkoani Pwani, watoto hao walisema ndani ya jengo hilo kuna watoto wengi wa kike na kiume.

Walisem a w atoto hao wanafanyishwa kazi na kuteswa kwa kutandikwa fimbo, kuchomwa moto na kupigwa shoti ya umeme hasa wanapowaulizia wazazi wao ambapo baadhi yao hubakwa na kulawitiwa.

"Jumba hili limejengwa ndani ya handaki, tulikuwa tukifanyishwa kazi ngumu na nzito, usiku tunajaza maji katika mapipa mengi na kubebeshwa ndoo kupanda na kushuka kilima.

"Tunapigwa fimbo, wasichana wanafungiwa kwenye vyumba, wanabakwa na kulawitiwa kwa zamu na Wazungu, tunachomwa moto (alionesha mguu wake uliochomwa) na kupigwa shoti ya umeme tunapowaulizia wazazi wetu," alisema Emmanuel kwa uchungu akitokwa na machozi.

Aliongeza kuwa, asubuhi ya Novemba 23 mwaka huu, katika jengo hilo kulitokea kutokuelewana kati ya Wazungu na Waswahili ambapo mswahili mmoja aliwatisha wazungu kwa kuwaambia polisi wanakuja hivyo walikimbia na kuacha mlango wazi.

"Hali hiyo iliniwezesha mimi, mdogo wangu na watoto wengine wachache waliokuwa na nguvu kufanikiwa kutoroka, nilimshika mkono mdogo wangu ambaye alionekana kuchoka nikamvuta.

"Watoto wengine wachache waliokuwa na nguvu nao wakatoka, wengi hawakuweza kutoka kutokana na kukosa nguvu, wanaumwa, wana vidonda vikubwa mwilini kutokana na kuchomwa moto na kupigwa shoti ya umeme, wasichana hawakuweza kabisa kutoka kwa kuwa wamefungiwa ndani ya vyumba," alisema Emmanuel

Aliongeza kuwa , alijikokota taratibu na mdogo wake mbali ya maumivu makali waliyonayo akatokea Mswahili mmoja ambaye alikuwa na gari lenye vioo vyeusi akawaambia wapande ili awatoroshe.

"Tulipanda gari hilo akatushusha darajani mpakani mwa Manispaa ya Kinondoni na Wilaya ya Kibaha, jirani na mzani eneo ambalo sisi hatukuwa tukilifahamu...dereva huyo alituambia gari limeishiwa mafuta hivyo alitutaka tumsubiri aende kuyanunua.

"Tulitembea kidogo tukiwa hatujui tunakokwenda... tulikaa kando ya barabara kutokana na uchovu pamoja na njaa kali kwani katika jengo hilo mbali na kazi nzito tulizokuwa tukizifanya na mateso mengi, mlo ulikuwa mmoja tu kwa siku.

"Tulikula saa 10 jioni, wali na maharage...tukiwa kando ya barabara, nilisikia sauti ya baba yangu wa kufikia, dereva wa magari makubwa yanayobeba kokoto ikiniita.

"Nilidhani naota kumbe ilikuwa kweli, alikuja akatukumbatia akalia kwa uchungu kwa namna tulivyokuwa tumechoka na afya kuzorota, akatupeleka polisi ambapo tulipatiwa maji tukaoga na kupewa chakula kizuri na kitamu, tukala na kupata nguvu za kuzungumza vizuri," alisema Emmanuel.

Akizungumza na Majira, Emmanuel alisema baada ya kutekwa yeye na mdogo wake, walifungwa na vitambaa vyeusi usoni hadi walipofikishwa ndani ya jumba hilo la mateso.

Aliiomba Serikali kufanya jitihada za hali na mali ili kuwaokoa watoto wengine waliopo katika jengo hilo.

Mama mzazi wa watoto hao, Martha Godianus (29), ambaye anafanya shughuli za mama lishe, njia panda y a Ba r a k u d a , Ta b a t a Manispaa ya Ilala, alisema amehangaika zaidi ya miezi mitatu kuwatafuta watoto hao bila mafanikio.

"Nimepoteza fedha nyingi kwa kuwatafuta na kutapeliwa mara kadhaa katika kuhangaika," alisema Godianus huku akitokwa na machozi ya furaha katika Kituo kidogo cha Polisi Maili Moja.

Alisema zaidi ya watoto saba walipotea katika mtaa wao, wawili wakapatikana baada ya wiki mbili, wengine wakiwemo wanaye wakawa hawajapatikana na kuomba Serikali ilichukulie kwa uzito suala hilo ili kubaini kundi linalowateka watoto na kuwatesa.

Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Ulrich Matei alikiri kutokea kwa tukio hilo na kuanza kulifanyia kazi kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Dar es Salaam.

Alisema makachero wa polisi wamewahoji watoto hao ili kupata maelekezo ya kufika katika andaki hilo na kuwataka watu wote wenye taarifa za eneo hilo watoe ushirikiano.

via gazeti la MAJIRA
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

Lady Jay Dee alivyoijibu kauli ya January Makamba twitter


Siku moja baada ya P Square kufanya show ya kihistoria Tanzania pale viwanja vya Leaders Club ,Mh January Makamba alivutiwa sana na walichofanya Wanageria wale na kutweet kuwa amependezwa sana na ile show lakini kwa upande wa nyumba tunatakiwa na sisi tujitahidi kuwainua wasanii wa hapa nyumbani ili siku moja wakashangiliwe kimataifa pia.
Ona Anaconda alivyojibu tweet ya Mh Makamba baada ya muda mchache baadae.




MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

Sunday, November 24, 2013

TAARIFA YA ZITTO ZUBERI KABWE (MB) KUHUSU KUVULIWA NAFASI ZA UONGOZI NDANI YA CHAMA


ZITTOKABWEf_4e9df.jpg
1. Utangulizi
Katika kikao chake cha siku mbili kilichofanyika tarehe 20 - 22 Novemba 2013, Kamati Kuu ya CHADEMA, pamoja na mambo mengine, iliazimia kunivua nafasi zangu zote za uongozi ndani ya chama. Kwa mujibu wa taarifa ya chama iliyotolewa katika mkutano na waandishi wa habari siku ya Ijumaa tarehe 22 Novemba 2013, ilielezwa kwamba sababu za kuvuliwa uongozi mimi na Dk Kitila Mkumbo ni uhaini na hujuma kwa chama kutokana na waraka unaojulikana kama mkakati wa uchaguzi 2013. Ukweli ni kwamba waraka uliotajwa si sababu ya mimi kuvuliwa nafasi zangu za uongozi kama ilivyojadiliwa katika Kikao cha Kamati Kuu.
 
Sababu za kufukuzwa kwangu kama zilizojadiliwa katika kikao cha Kamati Kuu ni tuhuma lukuki ambazo si mara yangu ya kwanza kuzisikia zikijadiliwa ndani na nje ya vikao vya chama. Hitimisho la tuhuma hizi ni kwamba mimi nimekuwa nikikisaliti chama kwa kutumika na CCM na Usalama wa Taifa. Nitazianisha tuhuma hizi na kuzijibu kama ambavyo nimekuwa nikizijibu katika vikao mbalimbali vyama.
 
Ninatambua kwamba chama changu kinapita katika wakati mgumu sana sasa hivi. Nataka nitamke mapema sana kwamba mimi Zitto Zuberi Kabwe sitokuwa chanzo cha CHADEMA kuvunjika. Hiki ndicho chama kilichonilea na kunifikisha hivi nilivyo. Ningependa chama hiki mtoto wangu atakapokuwa mtu mzima na atakapoamua kujiunga na siasa aingie CHADEMA. Bado nina imani kubwa na chama changu na ninaamini ndicho kinachostahili kuendesha nchi jana, leo na kesho.(P.T)
 
2. Kuhusu tuhuma mbalimbali zinazo elekezwa kwangu
Zipo tuhuma nyingi ambazo zimekuwa zikirudiwarudiwa katika vikao vya chama na nje ya vikao na baadhi ya viongozi wenzangu. Tuhuma hizi zinalenga kuonyesha kwamba mimi ni mbinafsi na kwamba ninapokea rushwa ili kukihujumu chama changu. Nitazianisha tuhuma kwa kifupi na kuzijibu kama ambavyo nimekuwa nikizijibu katika vikao mbalimbali vya chama.
 
i) Tuhuma kwamba sikushiriki kumpigia kampeni mgombea wetu wa urais katika uchaguzi wa mwaka 2010. Ningependa kueleza yafuatayo kuhusu jambo hili:
 
Mimi nilikuwa mgombea wa ubunge katika Jimbo la Kaskazini huko Kigoma.Pamoja na kuwa mgombea wa ubunge, nilifanya kampeni katika majimbo mengine 16 katika mikoa mbalimbali, ikiwemo Dar es Salaam, Mtwara, Pwani, Shinyanga, Mara na Rukwa. Hakuna kiongozi yeyote wa juu aliyefanya kampeni katika majimbo mengi kama mimi, ukiacha mgombea urais.Kote nilipopita nilimpigia kampeni wagombea wetu wa udiwani, ubunge na Rais.Katika Mkoa wa Kigoma nilizunguka na mgombea urais katika kata zote za Kigoma Kaskazini na majimbo yote manane ya Mkoa wa Kigoma.
 
ii) Tuhuma kwamba katika Mkoa wa Kigoma nilishindwa kuwapigia kampeni wagombea wetu kiasi kwamba peke yangu ndiye niliyeshinda katika uchaguzi huo. Ukweli ni kwamba niliwapigia sana kampeni wagombea wetu, na hivyo ndivyo wapiga kura wa Kigoma walivyoamua.
iii) Tuhuma kwamba nilishiriki kuwashawishi wagombea wetu katika baadhi ya majimbo kujitoa katika uchaguzi wa mwaka 2010 ili kuwapisha wagombea wa CCM wapite bila kupingwa kwa njia ya rushwa. Majimbo yanayotajwa ni pamoja na Sumbawanga, Musoma Vijijini na Singida Mjini. Kama nilivyokwisha kueleza katika vikao mbalimbali vya chama jambo hili si la kweli na hakuna popote ambapo watoa tuhuma hizi wamewahi kutoa ushahidi kwamba nilifanya jambo hili. Nipo tayari kwa uchunguzi ndani ya chama na watoa tuhuma waje na ushahidi bayana wa jambo hili. Si afya kwa chama kuendelea kurudiarudia tuhuma hizi kila mara tangu mwaka 2010 bila uchunguzi wowote kufanyika na jambo hili lifikie mwisho.
iv) Tuhuma kwamba nimekuwa sishiriki katika operesheni mbalimbali za chama: Ukweli ni kwamba nimeshiriki sana katika operesheni mbalimbali za chama ndani na nje ya nchi. Kwa mfano, mwaka 2011 tulikuwa na operesheni kubwa katika mikoa ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini na nilikwenda katika mikoa yote tuliyotembelea. Mwaka 2012 baada ya hoja ya mkonge bungeni nilifanya ziara Mkoa wa Tanga. Mwaka 2012 kulikuwa na operesheni kubwa moja katika mikoa ya kusini ya Mtwara na Lindi. Operesheni hii sikushiriki kwa sababu nilikuwa nchini Marekani kufungua matawi kwa mwaliko wa Watanzania wanaoishi huko.
v) Tuhuma kwamba nimekidhalilisha chama kwa tamko la PAC kwamba Hesabu za Vyama hazijakaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG): Katika jambo hili ninatuhumiwa kwamba mimi kama Naibu Katibu nilipaswa kuwasiliana kwanza na viongozi wa chama 'kuwatonya' ili wajiandae. Kwamba kutokuwatonya kumekidhalilisha chama na kukiweka kundi moja na CCM na nastahili kuadhibiwa vikali kwa kuwa katika taarifa yangu nilikuwa na nia mbaya na chama chetu. Maelezo yangu niliyoyatoa na ambayo ningependa kuyakariri hapa kuhusu jambo hili ni kama ifuatavyo:
Utawala bora hautaki mimi kutumia nafasi yangu ya uenyekiti wa PAC kulinda chama changu na kuonea vyama vingine. Kufanya hivyo ni kuendeleza tabia zile zile ambazo tunazipinga na ambazo tunapigania kuzibadilishaNapenda kusisitiza kwamba hakuna chama ambacho kimewahi kukaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG). Natambua kwamba mahesabu ya chama changu yamekuwa yakikaguliwa na wakaguzi wa nje kwa utaratibu tuliojiwekea. Lakini matakwa ya kisheria ni kwamba mahesabu ya vyama vya siasa hayajakaguliwa na CAG, na hili ni kosa la kisheria, bila kujali kosa hili ni la nani.
vi) Tuhuma kwamba mimi ni mnafiki katika kukataa kwangu kuchukua Posho za Vikao
Mtakumbuka kwamba mimi nilikataa kuchukua posho tangu mwaka 2011 kama ishara ya kuonyesha kwa vitendo msimamo wa chama chetu wa kupinga posho za kukaa na matumizi mengine yasiyofaa katika fedha za umma kama ilivyoanishwa kwenye Ilani yetu ya mwaka 2010-2015. Mtakumbuka kwamba hivi karibuni Mheshimiwa Lema amenishutumu kwamba kukataa kwangu kuchukua posho ni unafiki kwa sababu ninapokea posho kubwa zaidi katika mashirika ya umma ambapo mimi ni mwenyekiti wa kamati husika. Ninapenda kueleza yafuatayo kuhusu jambo hili:
Sipokei posho yeyote ya vikao (sitting allowance) ndani na nje ya Bunge tangu mwaka 2011. Hii ni pamoja na vikao vyote katika Kamati za Bunge ninavyohudhuria. Mtu yeyote mwenye ushahidi vinginevyo auweke hadharani.Swala la kukataa posho (sitting allowance) ni swala la kiilani katika chama chetu, na kwangu ni swala la kimisingi zaidi. Katika Wilaya yangu vifo vya kina mama wajawazito ni 1900 kati ya wanawake 100,000 wenye ujauzito. Vifo hivi vinatokana na ukosefu wa huduma kwa sababu ya bajeti finyu. Ndiyo maana nilifurahi sana kwa chama chetu kuliweka swala la kupunguza matumizi ya Serikali katika Ilani, na kuondoa posho za wabunge, ambao tayari wanapokea mishahara mikubwa, kungesaidia sana kupatikana fedha ambazo zingeokoa vifo vingi vya kina mama.Jambo hili si suala la ugomvi baina yangu na Mheshimiwa Lema. Ni suala la msingi katika chama chetu.
 
3. Usambazaji wa Ripoti ya Siri kuhusu Zitto Kabwe
Hivi karibuni kulisambazwa waraka unaoitwa ripoti ya siri kuhusu mimi ukibeba lundo la tuhuma kwamba nimehongwa fedha nyingi ili kukihujumu chama changu. Waraka huu ulidaiwa kuwa umechomolewa kutoka makao makuu ya CHADEMA. Jambo hili pia lilijadiliwa katika kikao cha juzi kwa kifupi, na majibu ya viongozi wa chama ilikuwa ni kwamba waraka huu haukuandaliwa wala kusambazwa na makao makuu. Katika mchango wangu nililalamikia mambo matatu yafuatayo:
 
Kwamba baadhi ya waliokuwa wanasambaza waraka ule walikuwa ni viongozi wa chama chetu. Bahati mbaya hadi leo hakuna hata mmoja ambaye amekwishachukuliwa hatua za kinidhamu. Ninaamini kwamba kuna siku watu hao watachukuliwa hatua kwa mujibu wa taratibu za chama chetu.Kwa kuwa chama kimekana rasmi kuhusika na waraka huu, nitaendelea na taratibu za kisheria ili kuhakikisha kwamba wote waliohusika kutengeneza hekaya ile wanachukuliwa hatua stahiki za kisheria.
 
4. Hitimisho
Ninatambua kwamba kuna watu walitegemea leo ningejibu mapigo na ningewazodoa watu kwa majina kama ilivyo kawaida katika siasa za Tanzania. Natambua pia kwamba, kama ilivyo kawaida wakati wa migogoro katika vyama vya siasa hapa Tanzania, kuna watu walitegemea leo ningetangaza 'maamuzi magumu'. Natambua kwamba wapo ambao wangependa kupata nafasi ya kuendelea kutumia suala hili katika harakati zao za kudhoofisha mapambano ya demokrasia na uthabiti wa siasa za ushindani nchini mwetu. Napenda wanachama wa CHADEMA na wapenda demokrasia na siasa safi wote nchini watambue kwamba mimi bado ni mwanachama mwaminifu wa chama hiki na nitakuwa wa mwisho kutoka kwenye chama hiki kwa hiari yangu. Nitafuata taratibu zote ndani ya chama katika kuhitimisha jambo hili.
 
Naomba wanachama waelewe kwamba mimi kama binadamu ninaumia ninapopigwa. Tuhuma ninazorushiwa ni kubwa na zinanikwaza. Tuache siasa za uzushi ili tujenge chama chetu na nchi yetu, ili hatimaye tuwakomboe Watanzania wenye matarajio na imani kubwa kwa chama chetu.
 
Kama mwanasiasa kijana niliyekaa katika siasa kwa muda sasa yapo mengi mazuri nimeyafanya. Lakini kuna maeneo nilipojikwaa na yapo makosa niliyofanya kisiasa katika maisha yangu ya siasa.
 
Kinachoendelea ndani ya chama chetu ni mapambano ya kukuza demokrasia. Ni mapambano baina ya wapenda demokrasia dhidi ya wahafidhina, waumini wa uwajibikaji dhidi ya wabadhirifu na wapenda siasa safi dhidi ya watukuzao siasa majitaka. Hii ni changamoto kubwa ndani ya chama chetu inayohitaji uongozi shupavu kuikabili.  Nitasimama daima upande wa demokrasia. Kama alivyopata kunena mmoja ya wanasiasa maarufu, 'kiwango cha juu kabisa cha uzalendo katika nchi ni kukubali kutofautiana kimawazo', na ninatamani huu ndio uwe utamaduni wa chama chetu.
 
Kabwe Zuberi Zitto, Mb
Dar es Salaam.
24 Novemba, 2013
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

Binti auawa Kimara, Dar kwa mpenzi wake akisubiri matokeo ya kidato cha nne


Mwanafunzi aliyehitimu kidato cha nne mwaka huu, Sharifa Abdallah (18) ameuawa kwa kuchomwa kisu shingoni na mbavuni chumbani kwa mvulana aliyedai  kuwa mpenzi wake maeneo ya Kimara Golani, Dar es Salaam.

Tukio hilo lilitokea juzi saa 8:30 mchana na baadaye mvulana huyo aliyetambuliwa na Polisi kwa jina la Abdul Alpha (22) kujisalimisha katika kituo cha Polisi cha Stendi Kuu ya Mabasi yaendayo mikoani cha Ubungo, akidai alikuwa akitaka kutoroka lakini aliona amefanya dhambi kubwa.
Akizungumza na mwandishi jana, mama mkubwa wa marehemu, Mwajuma Khamis alisema Sharifa alimaliza kidato cha nne katika sekondari ya Luguruni na alikuwa akisubiri matokeo.
Alisema juzi waliporejea kutoka kazini hawakumkuta nyumbani, waliulizia kwa ndugu kutokana na kwamba hakuwa na tabia ya kutoka nyumbani, lakini hawakufanikiwa kumpata hadi jioni ndipo polisi walipowataarifu kupatikana kwa mwili wake.
Alisema mwili wa marehemu ulikutwa chumbani kwa kijana huyo karibu na nyumbani kwao ukiwa na majeraha mwilini, lakini hawakujua kama mtoto wao ana mwanaume, wanatarajia kumzika kesho saa saba mchana.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura alisema polisi walipata taarifa za tukio hilo katika kituo cha Ubungo na kwenda katika chumba cha kijana huyo kilichokuwa kimefungwa kwa ndani na kukuta mwili wa msichana huyo ukiwa umejeruhiwa.
Alisema baada ya kumhoji mtuhumiwa, alisema alifanya hivyo kutokana na wivu wa kimapenzi, kwani alikuwa na uhusiano na msichana huyo lakini wazazi wa msichana hawakutaka amwoe, hivyo kumtaarifu kuwa amepata mchumba mwingine.
Alipoulizwa kwa nini hakutoa taarifa katika kituo cha Polisi Kimara alikofanyia mauaji, alisema aliogopa watu wa maeneo yale wangempiga na kumwua, kwa kitendo hicho.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Tumbi, Kibaha, huku kijana huyo akishikiliwa na Polisi.
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

‘Nilikuwa naomba Mungu kila siku ili afukuzwe Chadema’ - Mama Zitto




Baada ya Kamati Kuu ya Chadema kumvua uongozi aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Taifa Zitto Kabwe, mama yake mzazi Shida Salum (pichani) aibuka kueleza jinsi zahama hiyo ilivyokuwa ‘ushindi’ kwa mwanae. PICHA | MAKTABA 
Dar es Salaam. Siku moja baada ya Kamati Kuu ya Chadema kumvua uongozi aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Taifa wa chama hicho, Zitto Kabwe, mama yake mzazi, Shida Salum ametoa ya moyoni akieleza kuwa kilichomkuta mwanaye kimefunika mabaya mengi yaliyopangwa afanyiwe.
“Kwa upande wangu naona kama ni ushindi kwa Zitto kutokana na jinsi ninavyojua hali ilivyo, mambo yalikuwa ni mengi mno na nikwambie tu, Zitto kuvuliwa uongozi kumefunika hayo yaliyokuwa yamekusudiwa kufanywa dhidi yake. Nilikuwa naomba Mungu  kila siku ili afukuzwe Chadema,” alisema mama huyo wakati akizungumza na gazeti hili nyumbani kwake Tabata, Dar es Salaam.
Shida Salum alisema kuwa Mungu amemnusuru mwanaye na kusisitiza, “Watu walikaa na kutengeneza ripoti ya siri kuhusu Zitto na kuiweka kwenye mtandao kisha kuituma kwa wanachama wa Chadema wanaowafahamu. Mpaka wanafikia hatua hiyo maana yake ni kwamba wamejaribu njia zote za kummaliza, lakini wameshindwa.”
Alisema kutokana na hali ilivyo hivi sasa amemnyang’anya mwanaye kwa muda simu zake zote za mkononi, kompyuta mpakato (Laptop) pamoja na iPad ili asiwasiliane na watu, kwa maelezo kuwa wapo wenye nia mbaya wanaomsaka kumpa pole za kinafiki. “Kwa sasa nataka mwanangu atulize akili.”
Shida Salum, mbali na kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, pia ni  mwasisi wa  Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu (Shivyawata) na Mwenyekiti wa Chama cha Watu Wenye Ulemavu wa Viungo (Chawata).
Zitto pamoja na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Dk Kitila Mkumbo juzi walivuliwa uongozi kutokana na uamuzi wa kikao cha Kamati Kuu kilichokutana kwa siku mbili, kuanzia Novemba 20 mwaka huu katika Ukumbi wa Blue Pearl jijini Dar es Salaam, wakituhumiwa  kukisaliti chama.
Mbali ya kuwavua uongozi Zitto, Dk Mkumbo pamoja na  aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho mkoani Arusha, Samson Mwigamba, pia Kamati Kuu imewapa siku 14 wajieleze kwa nini wasifukuzwe uanachama.
Kwa uamuzi huo Zitto amebaki na wadhifa wa ubunge wake wa Jimbo la Kigoma Kaskazini na Uenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC).
Katika ufafanuzi wake wa jana, Shida aliwataka wanachama wa Chadema kuwa watulivu kwa maelezo kuwa Zitto hajafukuzwa uanachama, “Siku nyingi walikuwa wanamwinda na hata hilo jambo ambalo Chadema wanasema amefanya, hawana uhakika nalo.”
Juzi wakati akisoma uamuzi wa Kamati Kuu,  mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu alisema wamebaini kuwapo kwa mkakati mkubwa wa watu hao kutimiza malengo hayo ambao umeandikwa katika waraka unaoitwa ‘Mkakati wa Mabadiliko 2013’, ambao umeandaliwa na kikundi kinachojiita ‘Mtandao wa Ushindi’.
Alisema kikundi hicho vinara wake wapo wanne,  Zitto anajulikana kama Mhusika Mkuu (MM), Mkumbo (M1), Mwigamba (M3) na mtu mwingine wa nne ambaye alieleza kuwa hajatambulika na anatumia jina la M2.
Atoa ya moyoni
Mama Zitto ambaye wakati akizungumza na gazeti hili alikuwa amelala kutokana na kusumbuliwa na maradhi alisema, “Kutolewa katika uongozi ni jambo la kawaida.  Zitto hajafukuzwa chama ila anaweza akafukuzwa maana kapewa siku 14 tu za kujieleza.”
Alisema kauli iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibroad Slaa, kwamba chama hicho walimwondoa Aman Kabourou (aliwahi kuwa Mbunge wa Kigoma Mjini-Chadema)  itakuwa Zitto, inaonyesha jinsi watu walivyo na chuki na mwanaye.
“Hayo ni maneno ya chuki, maana hata Zitto naye ana watu wake ambao wanaweza kutengeneza aina fulani ya chuki kwa viongozi wa chama na wanaweza kupata wakati mgumu kufanya safari au mikutano yao mikoani,” alisema.
Alisema tangu siku nyingi ndani ya Chadema kulikuwa na mpango wa kumng’oa Zitto, akifafanua kuwa hata katika kikao cha Kamati Kuu iliibuliwa hoja ya ruzuku za vyama, huku wajumbe wakimshutumu Zitto kwamba kwa nafasi yake na Naibu Katibu Mkuu alitakiwa kuitetea Chadema kuhusu ruzuku.
Katika vikao vya Kamati ya PAC, Zitto aliingia katika malumbano na chama chake baada ya kutuhumu vyama vya siasa kuwa hesabu zake hazikaguliwi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), huku akitaka ruzuku kwenye vyama hivyo isimamishwe.
“Zitto alipoingia katika kikao cha Kamati Kuu alishikilia msimamo wake kwamba kama Chadema inachukia ufisadi, nacho lazima kihakikishe kinakaguliwa,” alisema na kuongeza;
“Wao wanaona ili waweze kusalimika katika suala hili la ruzuku ni lazima wamfukuze Zitto. Chadema hawako sawa, hesabu zao haziko sawa.”
Alisema kuwa tatizo lililopo ni kuwapo kwa mkakati wa watu fulani kuiyumbisha Chadema , hivyo kila juhudi zinafanywa ili kukitingisha chama hicho kipoteze mwelekeo.
“Siwezi kusema wamemwonea au hawajamwonea, wao wametumia waraka wa Mwigamba ambao Zitto amekiri katika Kamati Kuu kwamba hajawahi kuusikia wala kuuona, tofauti na Dk Kitila ambaye amesema amewahi kuuona,” alisema na kuongeza;
“Zitto anahusishwa na kitu ambacho Chadema hawana uhakika nacho, ukiusoma ule waraka katika aya ya mwisho umeandikwa hivi, ‘Huyu mtu tunayefikiria awe mwenyekiti hajaoa,
tumshauri aoe akikataa tutafute mtu mwingine’, maana yake ni kwamba waraka huo ulikuwa haujamfikia Zitto, kama ungekuwa umemfikia Zitto watu hao wasingemwomba Zitto agombee uenyekiti.” Alipoulizwa nafasi yake ndani ya Chadema kutokana na yaliyomkuta mwanaye alisema, “Mimi hawawezi kunitengenezea jambo. Hivi Zitto anaweza kuwa mbaya mimi nikawa mzuri.”
Mama huyo alieleza kuwa tangu alipovamiwa na majambazi nyumbani kwake, Aprili 19 mwaka huu hajawahi kuhudhuria kikao chochote cha Chadema. “Wale wanaodhani Zitto kaonewa wanatakiwa kuwa wavumilivu na wapole, wasubiri kwani kila kitu kinawezekana.”
Ushauri kwa mwanaye
Alisema kuwa mwanaye ana uamuzi wake na kwamba hata kama Chadema itamfukuza uanachama, haitaweza kumnyang’anya vyeti vyake vya elimu aliyoipata.
“Zitto anaweza kufanya kazi mahali popote duniani, lakini pia ni mwalimu anaweza kuamua kufundisha. Ubunge ni mgawanyo wa madaraka. Watu wote hatuwezi kuwa wabunge,” alisisitiza.
Alisema wakati Kikao cha Kamati Kuu kikifanyika Zitto alikuwa nje ya nchi na kwamba yeye alimshauri kuhakikisha kuwa anahudhuria kikao hicho.
“Alipotua tu na ndege aliniambia kuwa kuna foleni na alitaka kukodi pikipiki ili awahi kikao, aliniambia lazima aende ili kujua hatima yake.
Aliacha gari lake na kwenda na hata mimi nilimsisitizia kwamba ni lazima aende katika kikao,” alisema. Alisema kuwa Zitto alipofika katika kikao hicho aliweza kuzima hoja zote zilizomhusu ikiwamo ya ruzuku za vyama, kwamba baadhi ya wajumbe walipoona amebadili mwelekeo wa kikao, mjumbe mmoja (akamtaja kwa jina) aliibua waraka uliomng’oa Zitto katika wadhifa wake.
“Unajua Kamati Kuu ilijadili zaidi kuhusu ruzuku. Hata ule waraka uliongezwa maneno baada ya baadhi ya wanachama kumpora Mwigamba laptop yake alipokuwa mkoani Arusha katika kikao cha Chadema,” alisema.
Huku akiwataja wanachama wa Chadema walioongeza maneno katika waraka huo (wakiwamo wabunge wawili) na viongozi wa ngazi za juu wa Chadema, mama Zitto alisema kilichomkuta mwanaye ni ushindi mkubwa, kwamba alipangiwa kufanyiwa makubwa zaidi ya yaliyomkuta.
“Hakuna amani maana ukisikia kengele inagongwa hapa nyumbani unasema hao ndiyo wamekuja kumuua Zitto nini, hivi sasa mpaka walinzi wanaolinda hapa wakisikia unakuja nyumbani kwa Zitto lazima wakuandike jina na kukufuatilia,” alisema mama huyo.
Dk Kitila alonga
Akizungumza na gazeti hili jana, Dk Mkumbo alisema kutokana na ushauri wa watu mbalimbali, yeye na Zitto  wamepanga kukutana na waandishi wa habari na kutoa tamko.
“Tumepanga mimi na Zitto tutatoa ufafanuzi kuhusu jambo hili, nadhani ni kesho (leo), tutawajulisha lakini,” alisema.
 Baada ya chama hicho kutangaza kuwaengua katika uongozi Zitto na Dk Kitila, saa mbili baadaye  Makamu Mwenyekiti Taifa wa Chadema, Said Arfi aliandika barua  ya kujiuzulu.
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

MTIKISIKO CHADEMA:BAADA YA ZITTO KUWEKWA BENCHI, ARFI ANG'ATUKA.


ChademaMotoClip 9245c
Mgogoro ndani ya Chadema umezidi kupamba moto baada ya Kamati Kuu kuwavua uongozi Zitto Kabwe na Dk Kitila Mkumbo, huku Makamu Mwenyekiti Taifa, Said Arfi akiandika barua ya kujiuzulu.
Zitto alivuliwa uongozi wa Naibu Katibu Mkuu Taifa na Naibu Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, wakati Dk Mkumbo amevuliwa ujumbe wa Kamati Kuu. Wawili hao wanatuhumiwa kukisaliti chama.(HD)
Taarifa zilisema hoja ya kukisaliti chama pia ilimkumba Arfi akidaiwa kumwezesha Waziri Mkuu Mizengo Pinda kupita ubunge bila kupingwa, katika uchaguzi mkuu uliopita na ndiyo sababu ya kuamua kuachia ngazi nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Taifa.
Mbali ya kuwavua uongozi Zitto na Dk Mkumbo, pia Kamati Kuu imewapa siku 14 wajieleze kwa nini wasifukuzwe uanachama. Kwa uamuzi huo Zitto amebaki na wadhifa wa ubunge wake wa Kigoma Kaskazini na wadhifa mwingine kwenye Kamati ya Bunge.
Zitto azungumza
Mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho, Zitto aliliambia gazeti hili, "Sina cha kueleza, kikao kilikwenda vizuri na taarifa rasmi ya chama kuhusu uamuzi wa kikao itatolewa baadaye mchana (jana saa nane mchana), tusubiri Kamanda."
Arfi ajiuzulu
Makamu Mwenyekiti wa Taifa, Said Arfi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini, jana aliwasilisha barua ya kujiuzulu nafasi ya uongozi wa chama, akisema; "...kuchoshwa na unafiki unaoendelea ndani ya chama. Napenda ifahamike pia kwangu masilahi ya wapigakura, wakazi na wananchi wa Mpanda Mjini na Wilaya ya Mpanda ni muhimu katika kuwatumikia, hivyo basi sipo tayari kuchaguliwa marafiki.
Katika barua hiyo anasema amechochwa na tuhuma ambazo zimekuwa zikielekezwa kwake kuwa alimsadia Waziri Mkuu Mizengo Pinda kupita bila ya kupingwa katika uchaguzi wa ubunge katika uchaguzi mkuu uliopita.
"Kwa kipindi kirefu zimekuwepo shutuma dhidi yangu na kutiliwa shaka uhusiano wangu na Mhe Pinda Waziri Mkuu. Pamoja na kulijadili katika vikao kadhaa Mpanda na Dar es Salaam bado yapo mashaka kwa nini alipita bila kupingwa. Huo ulikuwa uamuzi wa Wanampanda kwenu imekuwa ni tatizo, lakini hamsemi kwa nini. Majimbo mengine 16 nchini yalipita bila kupingwa mlikuwa wapi na nani alaumiwe? Huu ni unafiki wa kupindukia.
Vilevile, katika barua hiyo, Arfi anasema amechukizwa na kauli ya mwasisi wa chama hicho, aliyemtaja kwa jina moja la Mtei kuwachagulia marafiki.
"Aidha mmechukizwa sana kwa nini nilihoji kauli ya Mwasisi wa chama, Mhe Mtei kutuchagulia viongozi. Naomba ifahamike wazi kwamba huu ni mtazamo wangu na utabakia hivyo siku zote kwa chama cha demokrasia kutoruhusu uongozi wa kiimla kwa kukidhi matakwa ya waasisi ambao huvigeuza vyama kuwa mali binafsi.Kwa kusema ukweli na kusimamia ukweli daima itabakia kuwa lengo langu katika maisha yangu siku zote hata kama itanigharimu maisha yangu."
Hata hivyo, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbroad Slaa alipoulizwa kwa njia ya simu kuhusu barua ya Arfi ya kujiuzulu uongozi, alisema; "Mimi nimekwishaondoka ofisini."
Taarifa ya chama
Akitangaza uamuzi wa Kamati Kuu jana Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu alisema, Zitto, Dk Mkumbo na Mwenyekiti wa Chadema mkoani Arusha, Samson Mwigamba walikuwa na mtandao wa kukiua chama hicho, huku wakitengeneza tuhuma za kuwachafua Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe na Katibu wake, Dk Willbroad Slaa.
Alisema kuwa kamati kuu ilibaini kuwapo kwa mkakati mkubwa wa watu hao kutimiza malengo hayo ambao umeandikwa katika waraka unaoitwa 'Mkakati wa Mabadiliko 2013', ambao umeandaliwa na kikundi kinachojiita 'Mtandao wa Ushindi'.
"Kikundi hicho vinara wake wapo wanne, Zitto anajulikana kama Mhusika Mkuu (MM), Mkumbo (M1), Mwigamba (M3) na mtu mwingine wa nne hatujamtambua kwa sasa yeye anatumia jina la M2" alisema Lissu.
Alisema wakati wa kuhojiwa na Kamati Kuu Dk Mkumbo alikiri kuwa mhusika mkuu wa mtandao huo ni Zitto, lakini Zitto alikana kuutambua waraka huo licha ya kueleza unamhusu kwa kuwa umetaja jina lake, kauli ambayo alidai Kamati Kuu haikutaka kuiamini.
Huku akieleza jinsi watu hao walivyokuwa wakiwasiliana na kupanga mikakati ya kuimaliza Chadema kwa siri chini ya ufadhili wa fedha kutoka kwa Zitto, Lissu alisema Naibu Katibu Mkuu huyo wa zamani alikuwa akitumiwa na Chama Tawala (CCM) kuimaliza Chadema.
"Mkakati wa Mabadiliko 2013 ni mpango haramu na ambao unaichanachana katiba ya chama chetu. Ni mkakati wa vita dhidi ya chama chetu na utaratibu wetu wa kikatiba. Hatuwezi kunyamazia mkakati huu wa kutumaliza, uvumilivu umefika kikomo," alisema.
Uamuzi
Alisema kutokana na hali hiyo kamati kuu iliamuru wahusika wote wavuliwe nyadhifa zao zote za uongozi wa chama, kukubaliana kuunda timu ndogo ya pamoja ya watendaji wa sekretarieti ya makao makuu ya chama hicho ili kumtambua mtu wa nne (M2).
"Kamati ya Bunge imetakiwa kuchukua hatua za haraka kuhakikisha Zitto anavuliwa nafasi zote za Naibu Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, pia wote wanatakiwa kujieleza ndani ya siku 14 kwa nini wasivuliwe uanachama na watapewa fursa ya kujitetea," alisema.Alisema Kamati Kuu itakutana kwa dharura kwa ajili ya kufanya uamuzi juu ya hatima ya watuhumiwa hao.
Kauli ya Mbowe
Awali Mbowe alipinga madai kuwa Zitto ameondolewa kwa kuwa alikuwa akitaka kugombea nafasi ya uenyekiti wa chama hicho, akasisitiza kuwa uamuzi huo umefanyika kwa kuwa Chadema ni chama cha watu, siyo mali ya mtu binafsi.
Mvutano Zitto, Lema
Kwa zaidi ya wiki mbili Zitto amekuwa akilumbana na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kuhusiana na masuala ya posho.
Vita hiyo ilianzishwa na Lema katika kikao cha wabunge wiki iliyopita aliposema kuwa Zitto anafanya unafiki kukataa posho.
Alimtuhumu mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini kwamba anakataa posho za vikao bungeni, lakini anapokea posho nyingi kutoka mashirika mbalimbali ya kijamii nchini.
Lema aliweka tuhuma hizo kwenye Mtandao wa Jamii Forum huku akisema suala hilo halihitaji vikao vya chama kulijadili isipokuwa vyombo vya habari na hususan, mitandao ya kijamii kwani hata Zitto hutumia mitandao hiyo.
Zitto alijibu kuwa tangu siku nyingi alikwishapiga marufuku kwenye Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kupokea posho kutoka taasisi au mashirika yanayosimamiwa na kamati hiyo.
Alisema tangu alipokuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), alipiga marufuku posho na pia aliwahi kuwashtaki kwa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) wabunge wanaochukua posho kutoka taasisi za Serikali.
Zitto pia alipata msukosuko mwingine baada ya kusambazwa ripoti inayoitwa 'Taarifa ya Siri ya Chadema' iliyomtuhumu kuwa alikuwa anashirikiana na CCM na viongozi wa Idara ya Usalama wa Taifa kuihujumu Chadema.
Pia, Zitto aliingia katika malumbano na chama chake baada ya kutuhumu vyama vya siasa kuwa hesabu zake hazikaguliwi na Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG), huku akitaka ruzuku kwenye vyama hivyo isimamishwe.Chadema ilipinga vikali madai hayo na kueleza kuwa imekuwa inatumia taasisi binafsi kufanya kazi hiyo. Vyama vinavyopata ruzuku ya Serikali ni vile vyenye wabunge Chadema, CCM, UDP, TLP, CUF na NCCR-Mageuzi.
Mvutano kikaoni
Wakati wajumbe wa kikao hicho wakivutana, Zitto alikuwa njiani akirejea kutoka Sudan Kusini, ambapo alienda na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC).
Taarifa kutoka ndani ya kikao hicho zinaeleza kuwa, baada ya kuibuka sintofahamu hiyo, Mbowe aliwapoza wajumbe wa kikao hicho, akiwaeleza kuwa haitakuwa busara kumjadili mtu ambaye hayupo.
"Mbowe alipendekeza kuwa ajenda hiyo iwekwe kando na itajadiliwa baadaye kutokana na Zitto kutokuwepo katika kikao hicho," zilieleza habari hizo.
Baadaye Zitto alituma ujumbe ambao ulitangazwa kwa wajumbe wote, kwamba alikuwa njiani kurejea Tanzania, kwamba akifika moja kwa moja atakwenda katika kikao hicho.
Zitto awasili, mzozo waibuka
Kama vile alikuwa akisubiriwa yeye, mara baada ya kufika katika ukumbi huo saa 2:23 usiku huku akisindikizwa na walinzi wanne, mvutano mkali uliibuka katika ukumbi huo na mara kadhaa walinzi wa chama hicho, Red Brigade walionekana kukaa tayari mlangoni kuzuia vurugu kama ingetokea.
Gazeti hili lilikuwa nje ya ukumbi huo na mara kadhaa lilisikia sauti za malumbano za baadhi ya viongozi wa chama hicho, akiwamo Zitto, Mbowe na Lema.
Wakati wakitoa maelezo kwa nyakati tofauti Lema na Zitto walishutumiana huku kila mmoja akimtaja mwenzake kuwa anatumia vibaya nafasi yake na mitandao ya kijamii.
"Tatizo lake ni kutumia mitandao ya kijamii kueleza mambo ya chama wakati akijua siyo utaratibu, ugomvi wangu naye kwa kiasi kikubwa uko hapo," alisikika akisema Lema.
Kuna wakati yaliibuka malumbano makali huku sauti za juu zikisikika kutoka ndani ya ukumbi huo, kati ya Zitto, Lema na Mbowe.Taarifa kutoka ndani ya kikao hicho zinaeleza kuwa Dk Mkumbo alikumbwa na rungu hilo baada ya kubainika kuwa alikuwa ameanda taarifa za siri ambazo zilikutwa katika kompyuta mpakato (laptop) ya Mwigamba ambayo alinyang'anywa baada ya kudaiwa alikuwa anasambaza taarifa za kuhujumu chama hicho.
Kikao hicho kilimalizika saa 10:00 alfajiri huku maamuzi hayo yakifanywa siri na Mbowe alipoulizwa kuhusu kuwepo kwa taarifa za Zitto na Dk Mkumbo kuvuliwa uongozi," alisema , "Taarifa zitatolewa baadaye mchana."
Wasomi wazungumza
Akizungumza na gazeti hili jana, Profesa Gaudence Mpangala alisema Chadema ni chama kikubwa kinachoweza kushinda uchaguzi mkuu ujao hivyo kinapaswa kuwa na viongozi walioshikamana na kuwa na nia moja.
Aliongeza kuwa endapo wapo viongozi wanaoonekana kwenda kinyume na viongozi wenzao na kwenda kinyume na misimamo ya Chama, kinayo haki ya kufanya maamuzi ya namna yoyote yenye lengo la kukinusuru.
"Chadema ni chama kikubwa kinachoweza kushika dola...kinahitaji mshikamano mkubwa kwa viongozi wake na kuhakikisha hawatokei wasaliti....kama ni kweli waliosimamishwa ni wasaliti ni halali kabisa" anasema Profesa Mpangala.
Naye aliyekuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha SAUT, Dk Charles Kitima alisema wakati umefika kwa vyama vya siasa kutambua kuwa uwepo wa demokrasia ndani ya vyama vingi vya siasa nchini ni kusahihishana na kujisahihisha.
Dk Kitima alisema kuwa na mitazamo tofauti siyo usaliti ni demokrasia na kusema endapo mtu au kiongozi anafanya kitendo cha kuvunja katiba ya nchi huyo moja kwa moja anakuwa mkosaji.
Mbunge wa Jimbo la Wawi (CUF), Hamad Rashid anasema matukio ya kufukuzana na kutuhumiana baina ya viongozi yanayofanywa na watendaji mkuu wa vyama vya upinzani yatasababisha upinzani uzidi kudidimia na kudumaa.
Alisema vyama vya siasa vimekuwa na usultani wa kuonekana kuwa vinapaswa kuongozwa na baadhi ya watu, na wengine wenye uwezo na mawazo mapya na yasiyopendwa na wakubwa anatafutiwa mbinu ya kuondoka.
Rashid alisema hali hiyo inasababishwa na kukosekana kwa mfumo mzuri wa uongozi ndani ya vyama vya siasa, ambapo anasema vyama haviongozwi kama taasisi na badala yake vinaongozwa kama mali za watu.
"Hili linalotokea Chadema sasa ni matokeo ya mfumo mbovu wa uongozi ndani ya vyama vya siasa nchini....vingi haviongozwi kama taasisi." alisema.
CHANZO MWANANCHI
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

PICHA:P SQUARE WALIPOISHIKA DAR PALE LEADERS CLUB


Takriban saa 2 None Stop....P Square kwa stage
Anaconda Jide akiwa na P- Square
Team Anaconda ikiwajibika Kwa Stage
Team Anaconda...Ni Balaa...
Anaconda Jide...Kwa stage
Ben Pol- Kwa stage
Back Stage-Gadner Habash na Weusi
Mc wa Shughuli Dullah
Nyomi lilivyofunga..leaders

Picha kwa msaada Alvin Collection
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

Dk Kitila: Nilishiriki kuandaa, kuhariri waraka



“Nitafuata taratibu zote za chama kama zilivyoelezwa katika Kamati Kuu, nitashiriki kikamilifu katika kutuliza hali ya kisiasa ndani ya chama ili Chadema kibaki imara na kiendelee kuwa tumaini la Watanzania” Prime Dk Kitila. 
Dar es Salaam. Aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Dk Kitila Mkumbo amezungumzia mambo sita yaliyojitokeza baina yake na wajumbe wenzake kabla ya kutimuliwa katika wadhifa huo.
Aidha, alisema alishiriki kuuandaa na kuuhariri ‘Waraka wa Mkakati wa Mabadiliko 2013’ uliokuwa mahususi kumwandaa aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe kuwa mwenyekiti.
Dk Mkumbo alivuliwa wadhifa huo akituhumiwa kufanya vitendo kinyume cha katiba na taratibu za chama hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mhadhiri huyo wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alisema: “Waraka ulilenga kujenga hoja ya kufanya mabadiliko ya uongozi na kuainisha mikakati ya ushindi kwa mgombea mlengwa katika Uchaguzi Mkuu wa Chadema ambao kwa ratiba ya awali ulikuwa ufanyike Desemba mwaka huu.”
Alisema katika kikao cha Kamati Kuu kilichowavua wadhifa huo, wajumbe walisema waraka huo ulikuwa na upungufu na ulikiuka misingi na kanuni zilizoainishwa katika Katiba ya Chadema.
“Kwa kuwa dhamira yangu imekuwa ni kusukuma mabadiliko ambayo Watanzania wanayatizama nje ya mfumo wa sasa wa utawala, nilikiri makosa na niliomba msamaha na kuomba kujiuzulu nafasi zote za uongozi ombi ambalo lilipingwa na wajumbe. Mwanasheria wetu akawashauri kuwa tukijiuzulu tutaondoka na heshima zetu, akataka tufukuzwe ili tuondoke na aibu,” alisema Dk Mkumbo. Alisema kunapokuwa na uchaguzi ndani au nje ya chama, watu lazima wafanye mikakati akisema hata leo Chadema kunafanyika mikakati ya kuiondoa CCM madarakani mwaka 2015 na kwamba kitendo hicho siyo dhambi.
Alisema katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa ndani wa Chadema, kuna haki ya kujiandaa… “Sisi tunaamini mabadiliko, mimi na Mwigamba tulianza kutengeneza mkakati, kwanza tuainishe sababu za kutaka mabadiliko, pili tutafute nani anayefaa kuwa mgombea wetu.”
“Tuliazimia kwamba tukimpata tuchambue nguvu na udhaifu wake na pia kuchambua udhaifu wa mgombea tunayedhani atatoka upande wa pili. Tulifanya hivyo kwa siri na ilikuwa siri kati yangu mimi na Mwigamba kwa sababu mikakati ya uchaguzi ni siri.”
Alisema kuwa baada ya kukamilisha mchakato huo wangemfuata Zitto na kumwomba kuwa mgombea: “Ndiyo maana tulieleza katika waraka kwamba hatuna uhakika kama Zitto atakubali kugombea, tulitaka kufanya haraka kukutana naye, ila uchaguzi ulipohairishwa nasi tukatulia.”
Alisema kikao cha Kamati Kuu kilipokutana Zitto alikuwa hajui lolote kuhusu waraka huo, pia yeye (Dk Kitila), alikuwa hajui kama waraka huo ulikuwa umevuja kwa wanachama wa Chadema, wakiwamo wajumbe wa Kamati Kuu.
“Siamini kama kugombea nafasi yoyote ndani ya chama ni uhaini. Msingi namba moja wa Chadema ni demokrasia ambayo inatakiwa kuruhusu ushindani katika nafasi za uongozi na hasa wa juu. Wanasema uhaini kwa sababu ya wasiwasi wa siasa za ushindani katika chama chetu, hakuna uhaini wala hujuma,” alisema.
Alisema siasa za ushindani nchini hazijaanza leo na kutolea mfano jinsi uchaguzi wa Chama cha Tanu alivyokuwa na ushindani kati ya Mwalimu Julius Nyerere na Ally Sykes.
“Rais Barack Obama wa Marekani alianza mikakati mapema, waliomfikisha pale alipo ni watu wanne waliotengeneza mkakati wa kupata mgombea na kufanya ashinde bila Obama kujua,” alisema.
Alisema yeye na Mwigamba walitumia njia hiyo na kwamba baadaye wangemfuata Zitto, wangembembeleza na wanaamini kuwa angekubali, “Siasa za ushindani ndani ya vyama ndiyo huzaa ushindani wa kweli katika jamii na kujenga demokrasia ya kweli katika jamii.”
Alisema waraka huo ulioandaliwa na watu wawili unaoeleza udhaifu na nguvu ya Chadema ulikuwa siri,  lakini anashangazwa kuona viongozi wa chama hicho kuusambaza, huku akiwataka wanachama wa Chadema kuusoma waraka huo na kueleza uhaini wao ni nini.
Alisema waraka huo haukulenga kukibomoa Chadema, bali kujenga taasisi na kufafanua kuwa aliomba kujiuzulu nafasi yake si kwa sababu ya kuogopa aibu ya kufukuzwa isipokuwa kutambua jinsi wenzake walivyokosa imani naye.
Aliwataka wanachama wa Chadema kupigania kwa dhati misingi mama ya chama ikiwamo demokrasia ya ndani.
“Tutawashawishi Watanzania kwamba chama hiki ni cha demokrasia kwa sisi wenyewe kuonyesha ushindani ndani ya chama. Hakuna namna ya kuweza kudhihirisha hilo zaidi ya kuruhusu uchaguzi huru na watu washindane kwa hoja,” alisema Dk Kitila.
Alisema wanachama wa Chadema wanatakiwa kulaani tabia iliyoibuka ndani ya chama hicho kuwaita watu wenye mtazamo tofauti na viongozi kuwa ni wasaliti. “Kukataa siasa za ushindani ndani ya chama ni kuhujumu demokrasia na ndiyo usaliti, kukataa demokrasia na kukosolewa huo ndiyo usaliti wenyewe.”

Alisema lugha za kuitana wasaliti au wahaini zilitumika katika mataifa ya kikomunisti kunyamazisha upinzani na kuzaa udikteta kwenye mataifa hayo, kwamba utamaduni huo ukilelewa Chadema utajenga udikteta.
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.