Saturday, March 30, 2013

LADY JAY DEE AWATOLEA UVIVU CLOUDS FM....AWAPONDA KINOMA, SOMA MWENYEWE ALICHOANDIKA


Screenshot - 3_30_2013 , 2_49_12 AM

East African popular musician Lady Jay Dee ameamua kuwapa modongo Clouds fm kupitia Twitter leo kutokana na wimbo wake mpya uliotoka hivi karibuni Joto hasira kutopigwa katika radio hiyo. Jay dee ameandika kuwa radio ya watu isiyopiga nyimbo za wasanii wa watu ila wasanii wao tu. Angalia tweet za Queen of Bongofleva huyo.

"Radio ya watu isiopiga nyimbo za wasanii wa watu ila za wasanii wao tu, wasiopendwa na watu.
 "Anaedai kuianzisha bongoflava aliapa kuiua bongo flava. Sasa hata wasioijua Hiphop nao wana beef na Bongo flava! Damn !!"

Jay Dee pia anaonekana kujizatiti na kujiamini kuonyesha kuwa yupo kwa lolote yeye kama Komandoo Binti Machozi aliandika tena "Kill me if u can. Am on Fire, siogopi ng'oooooo Jipangeni, Ni kweli nimelamba sumu, lakini hainidhulu. Nakunywa maziwa daily, I will survive".

 "Hee! Kuna wajinga wanadhani nili tweet nikiwa nimelewa, nilimaanisha na msimamo ni huo. Sitasema oooh kuna mtu ka hack ac yangu nooo its me"

" Kuna DJ flani alikuwa akipiga nyimbo nilizoshirikishwa akifika sehemu nilioimba mimi anakata verse yangu nimtaje?? Sa hivi anakat ya Prof J"

 Hata hivyo si Jay Dee pekee kuanza kulaumu kwani wapo wanamuziki wengine wanaolaumu nyimbo zao kutokupigwa.
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

Katika hali ya kutatanisha Korea Kaskazini yatangza vita na Korea kusini.



 

Korea Kaskazini hii leo imesema inaingia katika hali ya vita na Korea Kusini, katika muendelezo wa vita vya maneno dhidi ya utawala mjini Seoul na Washington, baada ya kuwekewa vikwazo vya kimataifa kufuatia jaribio lake la silaha za nyuklia.

Shirika la habari la Korea Kaskazini KCNA, limetoa taarifa inayosema kuwa kuanzia sasa, uhusiano wa Kaskazini na Kusini utaingia katika hali ya vita, na kwamba maswala yote yanayojitokeza kati ya Kaskazini na Kusini yatashughulikiwa ipasavyo. 

Tangu mwanzoni mwa mwezi huu Korea kaskazini imekuwa ikitishia kila siku kuishambulia Korea kusini pamoja na kambi za kijeshi za Marekani, baada ya Marekani na Korea Kusini kuanzisha mazoezi ya kawaida ya kijeshi na imeyaamrisha majeshi yake kukaa kwa tahadhari.

Korea kaskazini imetoa kitisho kipya kuishambulia Marekani, baada ya ndege mbili za Marekani chapa B-2 zenye uwezo wa kubeba makombora ya nyuklia kufanya mazoezi nchini Korea ya Kusini.
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

KURASA ZA MWANZO NA ZA MWISHO ZA MAGAZETI YA LEO MAR 30 2013.


.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

.

.

MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

Friday, March 29, 2013

Rais Kikwete atembelea Jengo lililoporomoka Dar Es Salaam leo.




 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es salaam leo akiwa ameongozana na mkewe Mama Salma Kikwete kujionea mwenyewe jengo lililoporomoka asubuhi saa mbili na nusu leo Machi 29, 2013 ambapo hadi Rais anafika mahali hapo saa saba kamili watu wawili wamethibitishwa kuwa wamekufa na wengine 19 kujeruhiwa, wawili wakiwa mahututi. Juhudi zinaendelea kuokoa watu wanaosadikiwa kunaswa kwenye kifusi cha jengo hilo lililokuwa limefikia ghorofa ya 15, likijengwa ubavuni mwa Msikiti wa Shia Ithnaasheri.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa  mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es salaam leo akiwa ameongozana na mkewe Mama Salma Kikwete kujionea mwenyewe jengo lililoporomoka asubuhi saa mbili na nusu leo Machi 29, 2013 ambapo hadi Rais anafika mahali hapo saa saba kamili watu wawili wamethibitishwa kuwa wamekufa na wengine 19 kujeruhiwa, wawili wakiwa mahututi. Juhudi zinaendelea kuokoa watu wanaosadikiwa kunaswa kwenye kifusi cha jengo hilo lililokuwa limefikia ghorofa ya 15, likijengwa ubavuni mwa Msikiti wa Shia Ithnaasheri.
 
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo toka kwa Mkuu wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Bw. Suleiman Kova na Mkuu wa Mkoa huo Mhe saidi Meck Sadiki katika eneo la  jengo lililoporomoka mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es salaam  asubuhi saa mbili na nusu leo Machi 29, 2013 ambapo hadi Rais anafika mahali hapo saa saba kamili watu wawili wamethibitishwa kuwa wamekufa na wengine 19 kujeruhiwa, wawili wakiwa mahututi. Juhudi zinaendelea kuokoa watu wanaosadikiwa kunaswa kwenye kifusi cha jengo hilo lililokuwa limefikia ghorofa ya 15, likijengwa ubavuni mwa Msikiti wa Shia Ithnaasheri.
 
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakisindikiwa na  Mkuu wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Bw. Suleiman Kova baada ya kutembelea eneo la  jengo lililoporomoka mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es salaam  asubuhi saa mbili na nusu leo Machi 29, 2013 ambapo hadi Rais anafika mahali hapo saa saba kamili watu wawili wamethibitishwa kuwa wamekufa na wengine 19 kujeruhiwa, wawili wakiwa mahututi. Juhudi zinaendelea kuokoa watu wanaosadikiwa kunaswa kwenye kifusi cha jengo hilo lililokuwa limefikia ghorofa ya 15, likijengwa ubavuni mwa Msikiti wa Shia Ithnaasheri.(PICHA NA IKULU).
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

NAFASI ZA KAZI 1,134 KUTOKA SERIKALINI....BOFYA HAPA




Serikali kupitia Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inawatangazia Watanzania wenye sifa na uwezo kujaza nafasi wazi za kazi kama zilivyo katika Tangazo la Lugha ya Kiingereza na Kiswahili.

Kwa mujibu wa Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Xavier Daudi nafasi hizo za kazi ambazo zinapatikana katika tovuti ya Sekretarieti ya Ajira ambayo ni www.ajira.go.tz ni kwa ajili ya Waajiri mbalimbali wa ofisi za umma.


Daudi alifafanua kuwa Waajiri hao ni pamoja na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Katibu Mkuu wizaraya Mambo ya Nje ya Nchi na Ushirikiano wa Kimataifa, Afisa Mtendaji Mkuu Wakala wa Vipimo, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo Jinsia na Watoto, Katibu Mkuu Wizara ya Kazi na Ajira, Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika, Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara. Katibu Mkuu Wizara ya Sayansi na Teknolojia, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Makazi, Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Katibu Ofisi ya Rais Maadili,

Wengine ni Katibu Tawala wa Mkoa Kagera, Iringa, Ruvuma, Mbeya, Mwanza, Shinyanga, Manyara, Dar es Salaam, Morogoro, Geita, Pwani, Mara, Kilimanjaro, Lindi, Singida, Tabora, Tanga, Katavi na Arusha, Mkurugenzi Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Mkurugenzi Halmashauri Manispaa Iringa, Songea, Shinyanga,
Morogoro, Singida, Kigoma/Ujiji na Temeke.

Nafasi nyingine ni kwa ajili ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya Mufindi, Kyela, Rungwe, Mbeya, Chunya, Biharamulo, Bukoba, Muleba, Namtumbo, Songea, Morogoro, Makete, Mkuranga, Mbinga, Tunduru, Ukerewe, Sengerema, Ilemela, Busega, Maswa, Meatu, Shinyanga, Kishapu, Kilosa, Msalala, Rufiji, Rorya, Ruangwa, Lushoto, Mkinga, Mpanda, Monduli, Ngorongoro,Kigoma, Nachingwea, Rombo, Same, Singida, Urambo, Tabora, Babati, Mbulu, Simanjiro, Kiteto, Handeni, Pangani, Kibondo, Chamwino, Mtwara, Nanyumbu, Mpwapwa, Kongwa naTandahimba. Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Njombe, Kibaha, Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) na TEMESA.

Katibu huyo amesema kuwa nafasi hizo zilizotangazwa zimegawanyika katika kada zifuatazo; Mchambuzi Mifumo ya Kompyuta daraja la II – (Nafasi 10), Afisa Vipimo II – Nafasi 6, Mpima Ardhi daraja la II (Nafasi 26), Mhandisi daraja la II – Ufundi Umeme – Nafasi 9,  Afisa Mipango Miji daraja la II– Nafasi 13, Mhandisi daraja la II - Ujenzi (Nafasi 16), Mhandisi daraja la  II - Maji (Nafasi 13), Afisa Misitu daraja la II (Nafasi 7), Afisa wa Sheria daraja la II – nafasi 3, Mtakwimu Daraja la II – nafasi 8, Mthamini daraja la II – Nafasi 7,  Mkadiriaji Ujenzi daraja la II  – nafasi 4, Afisa Ufugaji Nyuki Daraja la II – nafasi 1, Mhandisi Daraja la II – Nishati (Nafasi 3), Msanifu Majengo Daraja la II– (nafasi 3) na Mjiolojia Daraja la II – Nafasi 7, Fundi Sanifu daraja la II (Ujenzi) -Nafasi
26, Mvuvi Msaidizi Daraja la II – nafasi 8 na Fundi Sanifu Msaidizi (Maji) -nafasi 19.

Nafasi nyingine zilitotangazwa na Serikali ni Nahodha Daraja la II – Nafasi 6, Fundi Sanifu daraja la II - Haidrolojia -Nafasi 6 ,Fundi Sanifu Daraja la II -Nafasi 6, Msaidizi Misitu Daraja la II – nafasi 7, Fundi Sanifu Daraja II – Ramani – Nafasi 6, Fundi Sanifu Daraja la II –Maendeleo ya Jamii– Nafasi 3, Dereva Mitambo Daraja la II– nafasi 1,  Mpiga chapa msaidizi- Nafasi 5, Operata wa kompyuta msaidizi - nafasi 3, Fundi Sanifu Daraja la II - Migodi – nafasi 9, Polisi Msaidizi– Nafasi 5, Mpokezi–Nafasi 1, Katibu Mahsusi daraja la III-nafasi 10, Mlinzi –Nafasi 100, Dereva Daraja la II – nafasi 178,   Msaidizi wa Ofisi– Nafasi 30, Afisa Kumbukumbu daraja la II– nafasi 1,  Mwenyekiti wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya – nafasi 5, Afisa Mtendaji wa Kata Daraja la III– nafasi 10, Afisa Mtendaji wa Kijiji Daraja la II– nafasi 6.

Aidha, kada nyingine ni Afisa Mtendaji wa Kijiji daraja la III) – nafasi 232, Afisa Mtendaji Mtaa daraja la III– nafasi 3, Afisa Lishe daraja la II– nafasi 4, Fundi Sanifu Daraja la II - Ufundi na Umeme, Afisa Biashara msaidizi– Nafasi 1, Mchapa Hati daraja la II – Nafasi 1,  Mhandisi Daraja la II –Baharini-(nafasi 1), Dereva Mitambo Daraja la II – (nafasi 1), Dereva wa Vivuko daraja la II – Nafasi 3, Mkufunzi Mwandamizi Daraja II - Nafasi 1, Mkufunzi Daraja ii - Nafasi 2, Fundi Sanifu Msaidizi (bomba)–nafasi 3, Fundi Sanifu Msaidizi (Umeme) –Nafasi 4, Mkufunzi Daraja II– nafasi 3, Mkufunzi daraja la II -Jiolojia – nafasi 1, Mkufunzi Msaidizi– Jiolojia – nafasi 1, Fundi Sanifu daraja II -Ubunifu Mipango Miji – nafasi 1, Fundi Sanifu daraja II- Urasimu Ramani – Nafasi 5, Fundi Sanifu daraja II- Uchapaji Ramani –Nafasi 4, Fundi Sanifu Daraja la II -Maabara– nafasi 13, Fundi Sanifu Msaidizi (Ujenzi– nafasi 1), Fundi Sanifu daraja la II -Nafasi 4, Wakufunzi wasaidizi – nafasi 54 na Mhasibu Mkuu daraja II.

Katibu alifafanua kuwa nafasi 949 zilizoko katika tangazo la Kiswahili ni kwa ajili ya Waajiri walioainishwa hapo juu na kwa Tangazo la nafasi wazi 185 zilizoko katika tangazo la lugha ya Kiingereza ni kwa ajili ya Taasisi na Wakala mbalimbali za Serikali.

Daudi amesema mwisho wa kupokea barua za maombi ya kazi ni tarehe 9 Aprili, 2013.


Aidha, amewataka waombaji wote wa fursa za ajira kufungua matangazo yote mawili ya kazi na kuzingatia masharti ya Matangazo yote kama yalivyo katika lugha ya Kiingereza na Kiswahili kabla ya kutuma maombi yao.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
Ofisi ya Rais-Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.  27 Machi, 2013

Kwa maelezo zaidi; wasiliana na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
kwa Barua pepe; gcu@ajira.go.tz  au Simu; 255-687624975
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

BREAKING: IDADI YA MIILI ILIYOPATIKANA NA MAJERUHI MPAKA SASA BAADA YA GOROFA KUPOROMOKA LEO DAR


Hiyo taarifa hapo chini ni ya Meya wa Ilala
Hiyo taarifa hapo chini ni ya Meya wa Ilala Jerry Silaa.
Jengo lililoanguka Dsm ijumaa ya pasaka march 29 2013 Meya on idadi ya maiti
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

PICHA 6 ZA JENGO LA GOROFA LILILOANGUKA LEO DAR ES SALAAM


.
.
.
.
.
.
.
Picha zimepigwa na Ramadhani.
Kwa maelezo ya shuhuda, inasemekana limeanguka saa moja asubuhi ambapo kwa muda huo kulikua na watoto wa kihindi wanacheza mpira, kulikua na vibarua ambao wanataka kumwaga zege kuendelea na ujenzi na ndio walikua wanabadilisha nguo kuanza kazi.
Ni posta mtaa wa Indira Gandhi pembeni ya msikiti mkubwa wa Itnasheri, lilikua ni gorofa la floor 12 ambapo mpaka sasa hakuna hesabu kamili ya vifo lakini shuhuda anasema kwa muda mfupi baada ya kuanguka alishuhusia maiti nne.

Sehemu ya chini zinaonekana bado nzima hazijadondoka ila kifusi cha kutoka juu ndio kimefunika lakini kuna watu ndani yake wako hai na inaripotiwa wanapata hewa vizuri na wamekua wakiwapigia ndugu zao na kuwaita waje kwenye eneo la tukio.
Endelea kuwa karibu na millardayo.com taarifa zaidi zinazidi kufatiliwa.
.
.
hii picha imepigwa na Salma Msangi wa Channel ten ambae unaweza kutazama kazi zake pia kupitia salmamsangi.com
hii picha imepigwa na Salma Msangi wa Channel ten ambae unaweza kutazama kazi zake pia kupitia salmamsangi.com
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

HII NDIO RIPOTI YA MAKONGO HIGH SCHOOL KUHUSU KUFELI KWA DOGO JANJA NA UTORO ULIOKITHIRI



Baada ya taarifa kuenea kuhusu uwepo wa msanii Dogo Janja nchini Afrika Kusini kwa show alizopata zilizofanyika ndani ya wiki tatu, Uongozi wa shule anayosoma ya Makongo Sekondari, umetoa taarifa kuhusu mwenendo wake pamoja na matokeo aliyopata ya kidato cha pili.
 
Michael Alfred Mbaula ambae ni Afisa taaluma amesema “mahudhurio ya Dogo Janja darasani yalikua mazuri na alikua anashirikiana vizuri na wenzake kipindi kilichopita ila mara yake ya mwisho kuingia darasani ni novemba 2012, na kwa sasa atalazimika kurudia kidato cha pili kwa sababu amefeli kwa wastani mdogo ambao usingemruhusu kuendelea na kidato cha tatu”
 
Kuhusu kauli ya Dogo Janja kwamba juzi alipokwenda Afrika Kusini alikua ameomba ruhusa ya wiki mbili shuleni, Mbaula amesema “sio kweli kwamba aliomba ruhusa na wala ofisi haina taarifa japo shule haina tatizo akitoa taarifa hata katikati ya masomo iwapo anatakiwa kufanya shughuli za mziki kwa sababu Makongo ni shule ya vipaji, kuomba ruhusa ya wiki moja au mbili ambazo alikua akiziomba mwaka uliopita ndani ya mwezi mmoja ni sahihi ila kukaa miezi mitatu bila kuja shule ndio tatizo”
 
Mbaula amesema “Dogo Janja amefeli kidato cha pili kwa kupata wastani wa 27 ambapo alifanya vibaya sana kwenye hesabu kwa kupata sifuri, Civics alipata 27, historia 33, Jiografia 22, Kiswahili 46, Kiiingereza 42, Phisics 20, Chemistry 30, Biology 27, Commerce 8, Bookkeeping 11 hivyo ni lazima arudie darasa kitu ambacho anaweza kukifanya hapahapa Makongo”
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

PICHA 5 ZA MAREHEM STIVEN KANUMBA AKIWA KATIKA SCENE ZA MOVIE YAKE YA MWISHO.


Ni siku chache zimebaki kufika April,7 siku ya kukumbuka kifo cha Marehem Stiven Kanumba,ambapo atakua akitimiza mwaka mmoja tangu atutoke Dunian.

Katika kumuenzi Marehem litafanyika tamasha kubwa na la bure kabisa pale Leaders Club, Watu kutoka sehem mbali mbali za tanzania watakutana pale kwa lengo la kumuenzi na kuangalia yale aliyofanya enzi za uhai wake na kuzindua Filamu yake ya mwisho itwayo "LOVE AND POWER"  


Angalia picha 5 za marehemu kanumba akiwa katika scenes za movie hiyo.





MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

Thursday, March 28, 2013

Mahakama nchini Marekani yawatilia ngumu wanandoa wa jinsia moja kupata marupurupu ya serikali.


Mahakama ya juu nchini Marekani imesikiliza hoja dhidi ya sheria inayowanyima marupurupu ya serikali watu wa jinsia moja waliooana kisheria.
Majaji wanaosikiliza kesi hiyo walifuatilia kwa makini hoja kuhusu sheria ya kulinda ndoa inayojulikana kama DOMA.
Sheria hiyo inaeleza maana ya ndoa kuwa kati ya mwanamume na mwanamke, kwa maana kwamba wanandoa wanaume hawawezi kuomba wapewe baadhi ya malipo kutoka kwa serikali.
Jumanne wiki hii mahakama hiyo pia ilisikiliza hoja kama sheria inayopiga marufuku ndoa kati ya wanaume katika jimbo la California, ni kinyume na katiba.
Majimbo tisa ya Marekani yanatambua ndoa kati ya watu wa jinsia moja, huku 30 yakiwa yameipiga marufuku.
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.