Thursday, March 28, 2013

Mahakama nchini Marekani yawatilia ngumu wanandoa wa jinsia moja kupata marupurupu ya serikali.


Mahakama ya juu nchini Marekani imesikiliza hoja dhidi ya sheria inayowanyima marupurupu ya serikali watu wa jinsia moja waliooana kisheria.
Majaji wanaosikiliza kesi hiyo walifuatilia kwa makini hoja kuhusu sheria ya kulinda ndoa inayojulikana kama DOMA.
Sheria hiyo inaeleza maana ya ndoa kuwa kati ya mwanamume na mwanamke, kwa maana kwamba wanandoa wanaume hawawezi kuomba wapewe baadhi ya malipo kutoka kwa serikali.
Jumanne wiki hii mahakama hiyo pia ilisikiliza hoja kama sheria inayopiga marufuku ndoa kati ya wanaume katika jimbo la California, ni kinyume na katiba.
Majimbo tisa ya Marekani yanatambua ndoa kati ya watu wa jinsia moja, huku 30 yakiwa yameipiga marufuku.
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

No comments:

Post a Comment