Sunday, July 31, 2016

DOWNLOAD WANANDOTO KALA JEREMIAH ft MIRIAM CHIRWA (official video)




MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

Thursday, July 28, 2016

Joh Makini ft Chidinma - Perfect Combo Official Music Video




MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

Tuesday, July 26, 2016

DOWNLOAD AUDIO KALA JEREMIAH ft MIRIAM CHIRWA WANANDOTO



https://my.notjustok.com/track/117035/kala-jeremiah-ft-miriam-chirwa-wanandoto

MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

Friday, July 15, 2016

MATOKEO YA KIDATO CHA SITA(ACSEE) NA UALIMU (DSEE NA GATCE) 2016 YAMETANGAZWA


THE NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA 

BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA 

 MATOKEO YA KIDATO CHA SITA(ACSEE) NA UALIMU (DSEE NA GATCE) 2016.


MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

Thursday, July 7, 2016

JPM ateua wakurugenzi halmashauri za majiji, wilaya


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo July 07 2016 amefanya uteuzi wa wakurugenzi wa halmashauri za majiji 5, Manispaa 21, Miji 22 na Wilaya (DC) 137 za Tanzania Bara.
Uteuzi huo umetangazwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhandisi Mussa Iyombe ambapo kati ya wakurugenzi wote 185 walioteuliwa, 65 wameteuliwa kutoka orodha ya wakurugenzi wa zamani na 120 ni wakurugenzi wapya.
Orodha ya wakurugenzi walioteuliwa kulingana na mikoa yao ni kama ifuatavyo;

ARUSHA
⦁ Arusha Jiji – Athumani Juma Kihamia

⦁ Arusha DC – Dkt. Wilson Mahera Charles

⦁ Karatu DC – Banda Kamwande Sonoko

⦁ Longido DC – Jumaa Mohamed Mhiwapijei

⦁ Meru DC – Kazeri Christopher Japhet

⦁ Monduli DC – Stephen Anderson Ulaya

⦁ Ngorongoro DC – Raphael John Siumbu


DAR ES SALAAM
⦁ Dar es salaam Jiji – Siporah Jonathan Liana

⦁ Kinondoni Manispaa – Aron Titus Kagurumjuli

⦁ Temeke Manispaa – Nassibu Bakari Mmbaga

⦁ Ilala Manispaa – Msongela Nitu Palela

⦁ Kigamboni Manispaa – Stephen Edward Katemba

⦁ Ubungo Manispaa – Kayombo Lipesi John


DODOMA
⦁ Dodoma Manispaa – Dkt. Leonard M. Masale

⦁ Kondoa DC – Kibasa Falesy Mohamed

⦁ Kondoa Mji – Khalifa Kondo Mponda

⦁ Mpwapwa DC – Mohamed Ahamed Maje

⦁ Kongwa DC – Mhandisi Ngusa Laurent Izengo

⦁ Chemba DC – Semistatus Hussein Mashimba

⦁ Chamwino DC – Athuman Hamis Masasi

⦁ Bahi DC – Rachel Marcel Chuwa


GEITA
⦁ Bukombe DC – Dionis Maternus Nyinga

⦁ Chato DC – Mhandisi Joel Bahahari

⦁ Geita DC – Ally Abdallah Kidwaka

⦁ Geita Mji – Modest J. Apolinaly

⦁ Mbogwe DC – Mahwago Elias Kayandabila

⦁ Nyang’wale DC – Carlos K. Gwamagobe


IRINGA
⦁ Iringa Manispaa – William Donald Mafwele

⦁ Mafinga Mji – Saada S. Mwaruka

⦁ Mufindi DC – Riziki Salas Shemdoe

⦁ Iringa DC – Robert Mgendi Magunya

⦁ Kilolo DC – Aloyce Kwezi


KAGERA
⦁ Biharamulo DC – Wende Israel Ng’ahala

⦁ Bukoba DC – Abdulaaziz Jaad Hussein

⦁ Bukoba Manispaa – Makonda Kelvin Stephen

⦁ Karagwe DC – Godwin Moses Kitonka

⦁ Kyerwa DC – Shedrack M. Mhagama

⦁ Missenyi DC – Limbe Berbad Maurice

⦁ Muleba DC – Emmanuel Shelembi Luponya

⦁ Ngara DC – Aidan John Bahama


KATAVI
⦁ Mlele DC – Alex Revocatus Kagunze
⦁ Mpimbwe DC – Erasto Nehemia Kiwale

⦁ Mpanda DC – Ngalinda Hawamu Ahmada

⦁ Mpanda Manispaa – Michael Francis Nzyungu

⦁ Nsimbo DC – Joachim Jimmy Nchunda


KIGOMA
⦁ Buhigwe DC – Anosta Lazaro Nyamoga

⦁ Kakonko DC – Lusubilo Joel Mwakabibi

⦁ Kasulu DC – Godfrey Msongwe Masekenya

⦁ Kasulu Mji – Fatina Hussein Laay

⦁ Kigoma Ujiji – Manispaa – Judethadeus Joseph Mboya

⦁ Kigoma DC – Hanji Yusuf Godigodi

⦁ Kibondo DC – Shelembi Felician Manolo

⦁ Uvinza DC – Weja Lutobola Ng’olo


KILIMANJARO
⦁ Manispaa ya Moshi – Michael Nelson Mwandezi

⦁ Hai DC – Yohana Elia Sintoo

⦁ Siha DC – Valerian Mwargwe Juwal

⦁ Same DC – Shija Anaclaire

⦁ Mwanga DC – Golden A. Mgonzo

⦁ Rombo DC – Magreth Longino John

⦁ Moshi DC – Emalieza Sekwao Chilemeji


LINDI
⦁ Kilwa DC – Bugingo I. N. Zabron

⦁ Lindi DC – Samwel Warioba Gunzar

⦁ Lindi Manispaa – Jomaary Mrisho Satura

⦁ Liwale DC – Justine Joseph Monko

⦁ Nachingwea DC – Bakari Mohamed Bakari

⦁ Ruangwa DC – Andrea Godfrey Chezue


MANYARA
⦁ Babati Mji – Fortunatus Hilario Fwema

⦁ Hanang DC – Bryceson Paul Kibasa

⦁ Mbulu DC – Festi Fungameza Fwema

⦁ Mbulu Mji – Anna Philip Mbogo

⦁ Simanjiro DC – Yefred Edson Myezi

⦁ Kiteto DC – Tamim Kambona

⦁ Babati DC – Hamis Iddi Malinga


MARA
⦁ Manispaa ya Musoma – Fidelica Gabriel Myovela

⦁ Bunda DC – Amos Jeremiah Kusaja

⦁ Bunda Mji – Janeth Peter Mayanja

⦁ Butiama DC – Solomon Kamlule Ngiliule

⦁ Musoma DC – Flora Rajab Yongolo

⦁ Serengeti DC – Juma Hamsini Seph

⦁ Rorya DC – Charles Kitanuru Chacha

⦁ Tarime DC – Apoo Castro Tindwa

⦁ Tarime Mji – Hidaya Adam Usanga


MBEYA
⦁ Busokelo DC – Eston Paul Ngilangwa

⦁ Chunya DC – Sofia Kumbuli

⦁ Kyela DC – Mussa Joseph Mgata

⦁ Mbarali DC – Kivuma Hamis Msangi

⦁ Mbeya DC – Ameichiory Biyengo Josephat

⦁ Mbeya Jiji – Zacharia Nachoa Ntandu

⦁ Rungwe DC – Loema Isaya Peter


SONGWE
⦁ Momba DC – Adrian Jovin Jungu

⦁ Tunduma Mji – Valery Alberth Kwemba

⦁ Mbozi DC – Edna Amulike Mwaigomole

⦁ Ileje DC – Haji Mussa Mnasi

⦁ Songwe DC – Elias Philemon Nawela


MOROGORO
⦁ Gairo DC – Agnes Martin Mkandya

⦁ Kilombero DC – Dennis Lazaro Londo

⦁ Ifakara Mji – Francis Kumba Ndulane

⦁ Kilosa DC – Kessy Juma Mkambala

⦁ Morogoro DC – Sudi Mussa Mpili

⦁ Morogoro Manispaa – John Kulwa Magalula

⦁ Mvomero DC – Florent Laurent Kyombo

⦁ Ulanga DC – Audax Christian Rukonge

⦁ Malinyi DC – Marcelin Rafael Ndimbwa


MTWARA
⦁ Mtwara DC – Omari Juma Kipanga

⦁ Mtwara Mikindani Manispaa – Beatrice Dominic Kwai

⦁ Masasi Mji – Gimbana Emmanuel Ntayo

⦁ Masasi DC – Mkwazu M. Changwa

⦁ Nanyumbu DC – Hamis Hassan Dambaya

⦁ Newala DC – Mussa Mohamed Chimae

⦁ Newala Mji – Andrew Frank Mgaya

⦁ Tandahimba DC – Said Ally Msomoka

⦁ Nanyamba Mji – Oscar Anatory Ng’itu


MWANZA
⦁ Mwanza Jiji – Kiomoni Kibamba Kiburwa

⦁ Ilemela Manispaa – John Paul Wanga

⦁ Kwimba DC – Pendo Anangisye Malabeja

⦁ Magu DC – Lutengano George Mwalwiba

⦁ Misungwi DC – Eliud Leonard Mwaiteleke

⦁ Ukerewe DC – Tumaini Sekwa Shija

⦁ Buchosa DC – Crispian Methew Luanda

⦁ Sengerema DC – Magesa M. Boniphace


NJOMBE
⦁ Njombe Mji – Iluminata Leonald Mwenda

⦁ Makambako Mji – Paul Sostenes Malala

⦁ Makete DC – Francis Emmanuel Namaumbo

⦁ Njombe DC – Monica Peter Kwiluhya

⦁ Ludewa DC – Ng’wilabuzu Ndatwa Ludigija

⦁ Wanging’ombe DC – Amina Mohamed Kiwanuka


PWANI
⦁ Bagamoyo DC – Azimina A. Mbilinyi

⦁ Chalinze DC – Edes Philip Lukoa

⦁ Kibaha DC – Tatu Seleman Kikwete

⦁ Kibaha Mji – Jenifer Christian Omolo

⦁ Kisarawe DC – Mussa L. Gama

⦁ Mafia DC – Erick Mapunda

⦁ Mkuranga DC – Mshamu Ally Munde

⦁ Kibiti DC – Alvera Kigongo Ndabagoye

⦁ Rufiji DC – Salum Rashid Salum


RUKWA
⦁ Kalambo DC – Simon Ngagani Lyamubo

⦁ Sumbawanga DC – Nyangi John Msemakweli

⦁ Sumbawanga Manispaa – Hamid Ahmed Njovu

⦁ Nkasi DC – Julius M. Kaondo


RUVUMA
⦁ Mbinga DC – Gumbo Samanditu Gumbo

⦁ Mbinga Mji – Robert Kadaso Mageni

⦁ Namtumbo DC – Christopher Michael Kilungu

⦁ Nyasa DC – Oscar Albano Mbuzi

⦁ Songea DC – Simon Michael Bulenganija

⦁ Madaba DC – Shafi Kassim Mpenda

⦁ Tunduru DC – Abdallah Hussein Mussa

⦁ Songea Manispaa – Tina Emelye Sekambo


SHINYANGA
⦁ Kishapu DC – Stephen Murimi Magoiga

⦁ Msalala DC – Berege Sales Simon

⦁ Shinyanga DC – Mark Emmanuel Malembeka

⦁ Kahama Mji – Anderson David Msumba

⦁ Shinyanga Manispaa – Lewis Kweyemba Kalinjuna

⦁ Ushetu DC – Michael Augustino Matomola


SIMIYU
⦁ Bariadi DC – Abdallah Mohamed Malela

⦁ Bariadi Mji – Melkizedek Oscar Humbe

⦁ Itilima DC – Mariano Manyingu

⦁ Maswa DC – Fredrick Damas Sagamiko

⦁ Busega DC – Anderson Njiginya

⦁ Meatu DC – Said F. Manoza


SINGIDA
⦁ Ikungi DC – Rustika William Turuka

⦁ Iramba DC – Linno Pius Mwageni

⦁ Mkalama DC – Martin Msuha Mtanda

⦁ Manyoni DC – Charles Edward Fussi

⦁ Itigi DC – Luhende Pius Gerald

⦁ Singida DC – Rashid Mohamed Mandoa

⦁ Singida Manispaa – Kizito L. Brava


TABORA
⦁ Igunga DC – Revocatus Lubigili Kuuli

⦁ Kaliua DC – John Marco Pima

⦁ Nzega DC – Jacob James Mtalitinya

⦁ Nzega Mji – Phillimon Mwita Magesa

⦁ Sikonge DC – Simon Saulo Ngatunga

⦁ Tabora Manispaa – Bosco Addo Ndunguru

⦁ Urambo DC – Magreth Nakainga

⦁ Tabora -Uyui – Hadija Maulid Makuani


TANGA
⦁ Tanga Jiji – Daudi R. Mayeji

⦁ Korogwe DC – George John Nyaronga

⦁ Korogwe Mji – Jumanne Kiangoshauri

⦁ Muheza DC – Luiza Osmin Mlelwa

⦁ Handeni Mji – Keneth K. Haule

⦁ Handeni DC – William Methew Mafukwe

⦁ Pangani DC – Sabas Damian Chambasi

⦁ Mkinga DC – Mkumbo Emmanuel Barnabas

⦁ Bumbuli DC – Peter Isaiah Nyalali

⦁ Kilindi DC – Clemence Andagile Mwakasenda

⦁ Lushoto DC – Kazimbaya Makwega Adeladius


Wakurugenzi wote walioteuliwa wametakiwa kufika Ikulu Jijini Dar es salaam siku ya Jumanne July 12 2016 saa tatu asubuhi kwa ajili ya kula kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma.
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

Tuesday, July 5, 2016

Confirmed:Sikukuu ya Eid Jumatano July 06.........


Taarifa ambayo imetolewa na Mufti Mkuu wa Tanzania Zubeir Bin Ally muda mfupi uliopita ni uthibitisho wa sikukuu ya Eid ul Fitr ambapo Waislam wote walikua wakisubiri kuandama kwa mwezi, Kwenye taarifa yake Muft Zubeir amesema Mwezi huo umeonekana sehemu mbalimbali za nchi yetu ya Tanzania.



Amewaomba pia waislam kujitokeza kwenye misikiti mbalimbali kwa ajili ya ibada ya Eid ul Fitr.
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

DOWNLOAD VIDEO: HARMONIZE - MATATIZO (Official Video )


MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

Maneno Ya 20% Baada ya Kurudi Tena Ndani ya ‘Kombinenga’


Mkali wa Bongo Fleva, 20%  siku ya jana alisaini mkataba chini la Label ya Kombinenga inayomilikiwa na mtayarishaji wa muziki Man Water kutoka katika studio za Combination Sound, 20% aliweza kusaini mkataba wa miaka mitano kufanya kazi chini ya Label hiyo, ambayo itakuwa ikimsimamia katika kazi zake.

“Kwa upande wake 20% alisema kuwa sasa amerudi rasmi kuja kuwachinja tena na kusema amerudisha sauti ya gharama kwa jamii na mashabiki wake, sauti yenye kuburudisha, sauti yenye kufunza na kutoa burudani kwa watu wake” alisema 20%
Kwa upande wake Man Water amedai kuwa sasa 20% amerudi rasmi mwaka 2016 chini ya Kombinenga na kuwataka mashabiki wake mkao wa kula kupokea kazi nzuri zenye ujumbe mzito na wakusisimua kutoka kwa msani huyo

“Twenty Percent is back. …2016

Kaa mkao wakula ngoma zenye jumbe nzito na za kusisimua…kila kitu kiko sawa sasa…new page” aliandika Man Water.

MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

Mtoto wa Idi Amin akosoa sherehe za Entebbe


 
Bw Netanyahu amehimiza kuimarishwa kwa uhusiano baina ya Afrika na Isra


Mwanawe aliyekuwa kiongozi wa Uganda Idi Amin Dada amepinga sherehe za maadhimisho ya miaka 40 tangu kutekelezwa kwa operesheni ya makomando wa Israel uwanja wa ndege wa Entebbe.

Makomando hao walifika kuwaokoa mateka Wayahudi waliokuwa wanazuiliwa na wanamgambo wa Palestina waliokuwa wameteka ndege ya shirika la Air France.

Bw Hussein Lumumba Amin amesema ni makosa kwa serikali ya Uganda na nchi jirani za Afrika kushiriki sherehe hizo pamoja na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.

Kwenye taarifa yake kwa vyombo vya habari, Bw Amin, anasema baada ya kutekelezwa kwa shambulio hilo 1976, Umoja wa Afrika ulilaani kitendo hicho.

Aidha, amesema si haki kwa babake, Idi Amin, kuoneshwa kama mhusika katika utekaji nyara wa ndege hiyo.

Anasema babake alikuwa anatekeleza wajibu wa mpatanishi na kwamba hata aliwafaa mateka waliokuwa wanazuiliwa.

Aidha, alikuwa anatetea haki za Wapalestina.
 
Mnara wa walinzi na waelekezi wa ndege uwanja wa Entebbe
“Kama Amin angekuwa anapendelea upande mmoja wakati huo, mateka hao huenda labda wangezuiliwa gereza kuu la Luzira au afisi iliyoogopwa sana ya makachero wa serikali ambapo hawangeweza kutoroka,” Bw Lumumba anasema.

Anasema Bw Amin aliwaokoa mateka hao kwa kuhakikisha ndege hiyo, baada ya kutekwa, iliweza kutua Libya na kuongezwa mafuta kabla ya kuendelea na safari hadi Uganda.
  • Netanyahu: Israeli inataka uhusiano na Afrika
Kabla ya hapo, anasema ndege hiyo ilikuwa inazunguka angani bahari ya Mediterranean na haikuwa na mafuta ya kutosha kufika Uganda.

Kiongozi huyo wa zamani, alimsihi kiongozi wa Libya wakati huo, Kanali Muamar Gaddafi, aruhusu ndege hiyo kuongezwa mafuta.

Wakati huo, Bw Lumumba anasema kwenye taarifa yake, serikali za nchi za Kiarabu zilikuwa zimekataa ndege hiyo itue nchi zao.

“Kuingilia kati kwake huenda kuliokoa mateka wote na wahudumu wa ndege kutoka kwa mkasa wa kuanguka baharini,” anasema Bw Lumumba.

Anaeleza kuwa uwanja wa ndege, Idi Amin, angewazuru mateka na alihakikisha walipewa chakula na malazi mema.
Mateka takriban 100 waliokolewa

“Habari zinazoenezwa kuhusu kisa hicho cha Entebbe zinafanya ionekane kana kwamba Amin mwenyewe alikuwa mtekaji nyara. Makusudi, wamekaa kimya kuhusu usaidizi wowote ambao huenda (Amin) alitoa kwa mateka hao wa Israeli wakati huo,” anasema Lumumba.

Nduguye Bw Netanyahu, Luteni Kanali Yonatan "Yoni" Netanyahu aliyeongoza makomando 29 wa Israeli ndiye pekee kutoka Israel aliyeuawa wakati wa operesheni hiyo.

Wanajeshi 20 wa Uganda waliuawa.
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

Uganda na Tanzania wajadili bomba la mafuta




 

Baada ya tangazo la marais wa Uganda na Tanzania sasa maafisa wameanza vikao vya utekelezaji mradi wa bomba la mafuta
Uganda na Tanzania zimeanza upya mazungumzo utekelezaji wa makubaliano baina ya viongozi wa mataifa hayo mawili kupitisha mradi wa bomba la mafuta kupitia Hoima Tanga badala ya Hoima - Lamu Kenya.
Ujumbe wa Uganda unaongozwa na waziri wa kawi Irene Muloni huku Tanzania wakiongozwa na Prof Sospeter Muhongo.


Wengine wanaohudhuria mazungumzo hayo huko Hoima ni wawakilishi wa kampuni ya kuchimba mafuta yenye asili yake nchini Uingereza Tullow, mjumbe wa kampuni ya kuuza mafuta ya Total yenye asili yake nchini Ufaransa na kisha
kampuni ya kichina ya CNOOC inayotekeleza mradi wenyewe wa kuchimba na kuweka bomba la mafuta Kuanzia Hoima hadi bandari ya Tanga.

 
Bomba hilo la mafuta litakwenda kilomita 1,400km kuanzia Hoima, hadi kwenye bandari ya Tanga.
Mada kuu ya mazungumzo hayo huko Hoima ni utekelezaji wa miradi kwa kuzungumzia hali halisia.
Kwa mfano maswala ya ardhi itakayotumika kwa mradi huo itamilikiwa na nani na itatwaliwa vipi kutoka kwa uma, pia kuna swala la ukubwa wa ardhi yenyewe, wanadani wanasema kuwa mradi huo ulikuwa umependekezwa utekelezwe kwenye ardhi ya takriban mita 20 ,sasa hilo linaonekana kupata upinzani na hivyo kunahoja mbadala ukubwa huo upunguzwe katika mradi huo utakaotekelezwa kwa umbali wa kilomita 1403
Uganda yavunja mkataba na kampuni ya Urusi
Uganda kupitishia mafuta yake Tanzania

Kenya iliamua kujenga bomba la mafuta kutoka Turkana hadi Lamu

Aidha swala la ujenzi wa mtambo wa kusafishia mafuta wenye thamani ya dola bilioni 2.5 uliopata pigo baada ya Serikali ya Uganda kukatiza mazungumzo na kampuni moja ya Urusi pia utajadiliwa.
Uganda imeanza mazungumzo mbadala na kampuni moja ya ujenzi kutoka Korea Kusini.
Uganda ilikuwa imependekeza kujenga bomba la mafuta safi mkabala na bomba la mafuta la Hoima -Tanga.
Mkurugenzi wa usafirishaji wa mafuta nchini Uganda Robert Kasande akizungumza na wanahabari alisema kuwa tayari wajumbe wamekubaliana mambo mengi kati ya maswala makuu yaliyohitaji kujadiliwa.
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

Rais Magufuli atengua na kufanya uteuzi mwingine leo July 05 2016





Taarifa niliyoipokea kutokea ikulu inasema kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa kifungu cha 48 cha sheria ya tafsiri za sheria (Interpretation of Laws Act) Sura 1, leo tarehe 5 Julai, 2016 ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Maendeleo ya TIB Prof. William Lyakurwa.

Kufuatia hatua hiyo, kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo chini ya kifungu cha 9 (2) cha ya Sheria ya mashirika ya umma (Public Corporations Act) Sura 257, Rais Magufuli amemteua Prof. Palamagamba J. A. M. Kabudi kushika nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Maendeleo ya TIB kwa kipindi cha miaka mitatu.

Kufuatia mabadiliko hayo, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango kwa mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa kifungu cha 48 cha sheria ya sheria ya tafsiri za sheria (Interpretation of Laws Act) Sura 1, ametengua uteuzi wa Wajumbe Bodi ya Benki ya Maendeleo ya TIB. 

Aidha, kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo chini ya kifungu cha 9 (1) cha ya Sheria ya mashirika ya umma (Public Corporations Act, Sura 257) Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango ameteua wajumbe wapya wa Bodi wafuatao kwa kipindi cha miaka mitatu

⦁ Brig. Gen (Rtd) Mabula Mashauri
⦁ Dkt. Razack B. Lokina

⦁ Bi. Rose Aiko

⦁ Prof. Joseph Bwechweshaija

⦁ Bw. Said Seif Mzee

⦁ Dkt. Arnold M. Kihaule

⦁ Bw. Maduka Paul Kessy

⦁ Bw. Charles Singili

Uteuzi wa Mwenyekiti na Wajumbe wapya wa Bodi unaanza tarehe leo July 5 2016.
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

Sababu za Diamond kuhusu picha ya Alikiba kwenye ofisi za WCB….





Perfect Crispin ni mtangazaji wa Clouds FM ambaye hapa anatusogezea stori zilizochukua headlines kutoka kwenye tasnia ya Bongo Fleva, ambapo leo July 5,2016 ametusogezea hizi stori tatu ikiwemo ya Diamond Platnumz kuzungumzia picha ya Alikiba iliyowekwa katika ofisi za WCB.

‘Unajua ofisi ya WCB sio ya Diamond Platnumz sio ya Harmonize sio ofisi ya wakina Tale ni ofisi ya Muziki wa Bongo Fleva ambayo imekuwepo kuleta maendeleo kwenye muziki wetu, kwahiyo nimeamua kuweka zile  picha za mastaa ikiwemo ya Alikiba  kwamba ndio wasanii wenye mchango kwenye muziki wetu’-Diamond Platnumz
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

Baada ya ajali mfululizo zilizohusisha mabasi, polisi wamekuja na hii taarifa



Ni takribani wiki moja yametokea matukio makubwa matatu ya ajali za barabarani mfululizo ambayo yamehusisha mabasi yanayofanya safari zake mikoani, taarifa ya polisi imesema ajali hizo zimesababisha jumla ya vifo vya watu 46 na majeruhi 73.

Matukio hayo yanahusisha ajali iliyotokea June 28 2016 Misungwi Mwanza  ambapo basi la kampuni ya Super Samy likitokea Shinyanga kwenda Mwanza lilipata ajali kwa kuacha njia na kupinduka hivyo kusababisha vifo wa watu 5 na majeruhi 13.

Tukio lingine ni mnamo July 01 2016  VETA Dakawa katika barabara ya Morogoro/Dodoma malori mawili yaligongana na kuwaka moto na kusababisha vifo vya watu 5 na  na baadae katika eneo hilohilo siku July 02 2016 usiku gari la kampuni ya OTA lilipata ajali kwa kuyagonga mabaki ya malori yaliyopata ajali na kubaki eneo la tukio na kusababisha vifo  vya watu 6 na majeruhi 6

Halikadhalika mnamo July 04 2016 maeneo ya Maweni-Kintiku Singida mabasi mawili ya kampuni ya City Boys yaligongana na kusababisha vifo wa 30 na majeruhi 54 ambapo hadi leo wamebaki majeruhi 33 wakiendelea na matibabu. Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa polisi, kikosi cha usalama barabarani, Mohamed Mpinga amesema
>>>’kwa ajali iliyotokea Maweni Singida siyo ajali ya kawaida bali ni tukio la kufanya mauaji bila kukusudia, hivyo polisi imedhamiria kuwafikisha mahakamani madereva waliohusika na ajali hiyo kwa mashtaka ya mauaji bila kukusudia kutokana na taarifa za awali za chanzo cha kutokea kwa ajali hiyo kwamba madereva wa mabasi hayo walikuwa wakifanya mzaha wakati wa kupishana.

>>>Aidha tumewasiliana na wenzetu wa SUMATRA, kampuni ya mabasi ya City Boys na makampuni mengine yaliyohusika katika ajali yafungiwe kutoa huduma za usafirishaji katika njia zote hapa nchini
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

Zamaradi kuhusu mahojiano na mwanaume anayejihusisha mapenzi ya jinsia moja


Kama utakuwa unakumbuka hivi karibuni mtangazaji wa Clouds TV, Zamaradi aliingia kwenye headlines za kufanya mahojiano na mwanaume anayejihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Sasa leo July 5, 2016 amezungumza na Ayo TV kueleza kile ambacho alikuwa akitarajia baada ya kurusha mahojiano hayo na kusema….‘Nilitarajia kwamba kuna watu watakuwa hawanielewi kwa kile nilichokuwa nakifanya na yule mtu, kwahiyo nilijua kwamba kuna aina ya watu ambao ni vigumu sana na kama utakuwa unakumbuka kabla ya kuanza kipindi nilisema najua kuna watu watanikosoa kwa kile ninachokirusha kwahiyo impact imekuwa kubwa’- Zamaradi

MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

PICHA 15: DC Gondwe rasmi ofisini kwake Handeni Tanga!


Mtangazaji mkongwe Godwin Gondwe ni miongoni mwa wakuu wa Wilaya wapya walioteuliwa na Rais Magufuli ambaye mwishoni mwa wiki alikuwa ni miongoni mwa wakuu wa wilaya wapya nane wa wilaya za mkoa wa Tanga walioapishwa na mkuu wa mkoa huo, Martin Shigela, kushika wadhifa huo.
Gondwe ameteuliwa kuwa mkuu wa Wilaya ya Handeni na hapa rasmi ameanza kutekeleza majukumu yake
13495301_1026842670733760_2749475014848608034_n
.
13516149_1026842207400473_6121894779098771318_n
.
13435456_1026841477400546_1374006405219847851_n
13528754_1026843010733726_2728326069503132052_n
13557670_1026841917400502_1946866140714881756_n
.
13557676_1026841860733841_3504302852576707063_n
13567067_1026842744067086_7480311689404712173_n
.
13567480_1026843117400382_5163859454991466912_n
.
13567293_1026843074067053_2688152585902801072_n
.
13590228_1026842850733742_2155676313116316571_n
.

13590398_1026842484067112_1792617471443967264_n
.
13590504_1026842294067131_3447681663306351623_n
.
13599852_1026841610733866_1859383303269268075_n
.
13620253_1026841664067194_2102052997560850740_n
DC Gondwe akipokea mchango wa madawati kutoka kwa mwakilishi wa A to Z Company .







13620932_1026841570733870_5882275500979903394_n
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

Picha zaidi Ajali ya basi kampuni ya 'City Boy' iliyotokea jana singida


Kamanda wa polisi mkoa singida Thobias Sedoyoka amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kwamba ajali hiyo inahusisha basi lenye usajili wa no T 531 BCE likitokea dar kwenda kahama na basi T 247 linalotoka kahama kwenda Dar yote ya kampuni moja CITY BOYS, yamegongana uso kwa uso na kuuwa abiria 24 papo hapo na kujeruhi wengine Kabla ya kuua watu, lilikamatwa na tochi likiwa na spidi 122km/hr. Kwa taarifa zaidi kuhusu ajali hiyo
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

Friday, July 1, 2016

Jeff Untouchable Feat Sifa Digitali-Embe Dodo Mp3 Download


DOWNLOAD HAPA CHINI
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.