Monday, March 4, 2013

HAYA NDIO MANENO MAFUPI YA DIAMOND KUHUSU KUNUNUA GARI JINGINE NA GHARAMA YA NYUMBA ALIYOMJENGEA MAMA


.
Diamond akiwa mbele ya Prado yake siku alipoamua kuitangaza kwenye media june 2012.

Kupitia post hii millardayo.com inakujulisha kwamba mwimbaji staa ambae ndio mwimbaji Mtanzania alieongoza kwa kuandikwa sana kwenye internet mwaka 2012, Diamond Platnums ametangaza mpango wa kununua gari jingine.
Tofauti na Prado aliyoinunua june 2012, Diamond hajataka kutaja ni aina gani ya gari aliloliagiza sasa hivi lakini kakubali kwamba kaliagiza Japan na litakua la gharama ya juu kuliko Prado.
Ukiachia mbali hilo gari analoliagiza, Diamond amekiri pia kwamba amemaliza kuijenga nyumba yenye gharama ya milioni mia mbili sitini ambayo ameijenga maalum kwa ajili ya mama yake mzazi.
Diamond ambae amekua akiandamwa na maneno maneno ambayo anaamini wanaoyasambaza ni wasiompenda amesema “mimi nikimtanguliza Mwenyenzi Mungu mbele ata mtu atake kunifanya kitu gani haweziii mpaka aandike Mwenyenzi Mungu mwenyewe, ndio maana wao kila wakipiga vita… mimi nazidi kuwa maarufu, nazidi kuwa na hela… sasa hivi nabadilisha Prado nanunua gari jingine….. jamani mtaiona”

VIA:millardayo.com
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

No comments:

Post a Comment