Friday, February 22, 2013

Upinzani nchini Djibout kushiriki uchaguzi wa bunge leo baada ya kususia kwa miaka 10.Uchaguzi wa bunge nchini Djibout unafanyika leo ambapo kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 10 upinzani unashiriki.

Uchaguzi huu unafanyika miaka miwili baada ya rais Ismail Omar Guelleh kuchaguliwa kuongoza nchi hiyo kwa mhula wa tatu.

Chama chake cha PRP kimekuwa kikishinda uchaguzi tangu nchi hiyo ilipopata uhuru mnamo mwaka 1977 kutoka mikononi mwa Ufaransa.

Upinzani umekuwa ukisusia uchaguzi kwa madai kuwa hakuna uwezekano wa kushinda katika mfumo wa vyama vya wafuasi wa mirengo tofauti serikalini chini ya rais Guelleh.

MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

No comments:

Post a Comment