Friday, February 22, 2013

Jisajili Hapa Kwa wanaotaka kufanya mtihani wa kidato cha Nne (CSEE) na Maarifa (QT) mwezi Novemba 2013 kama watahiniwa wa kujitegemea Kwa huraisi


T A N G A Z O   

Katibu Mtendaji Baraza la Mitihani la Tanzania anapenda kuwatangazia watu wote wanaotaka kufanya mtihani wa kidato cha Nne (CSEE) na Maarifa (QT) mwezi Novemba 2013 kama watahiniwa wa kujitegemea kwamba kipindi cha usajili kitaanza rasmi tarehe 01/01/2013 kwa ada ya shilingi 35,000/= kwa CSEE na 20,000/= kwa QT. Kipindi cha malipo bila adhabu kinaishia tarehe 28 Februari 2013.

Kuanzia tarehe 01 Machi 2013 hadi tarehe 31 Machi 2013 waombaji watajisajili kwa ada ya shilingi 50,000/= kwa CSEE na 30,000/= kwa QT (ada pamoja na faini).

Waombaji wote watajisajili kwa njia ya mtandao kupitia tovuti: www.necta.go.tz. ya Baraza la Mitihani la Tanzania. Kabla ya kujisajili kwenye mtandao, waombaji watapaswa kwenda kwenye vituo vya mitihani kuchukua namba rejea (reference number) watakazotumia kujisajili. Hakuna mtahiniwa atakayeweza kujisajili bila kupata namba rejea kutoka katika kituo anachokusudia kufanyia mtihani. Wakuu wote wa vituo nchini wamekabidhiwa namba rejea hizo tayari kwa kuzigawa kwa watahiniwa tarajali bila malipo.

Bofya Hapa Kujisajili
 
LIMETOLEWA NA:

KATIBU MTENDAJI
BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA


Bofya Hapa Kujisajili

 Hakikisha wakati wa kufungua "account" unaandika anwani ya barua pepe (email) sahihi inayotumika. Ukishindwa kutoa anwani sahihi ya barua pepe, itakua vigumu kupatiwa huduma zifuatazo:
  1. Kupata password mpya na username iwapo utazisahau!

  2. Kukutumia taarifa mbalimbali za kukusaidia unapokwama kwenye zoezi la usajili.
Tunaomba ushirikiano wako katika kutekeleza tangazo hili ili tuweze kukuhudumia ipasavyo.

 
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

No comments:

Post a Comment