Friday, February 15, 2013

REST IN PEACE GOLDIE HARVEY ANGALIA WIMBO ALIOIMBA NA AYKupitia mitandao ya Nigeria inaendelea kusikitika kufuatia taarifa za kifo cha aliyekuwa mwakilishi wa Nigeria katika shindano la Big Brother Afrika 2012,Goldie harvey, na mchumba wa rapa kutoka Kenya Prezzo.
Habari zinaendelea kupokelewa kwa hisia tofauti huku wengine wakiwa bado hawaamini kama kweli Goldie amefariki lakini ukweli ni kwamba mitandao yote ya nchini Nigeira iimedhibitisha kifo hicho.

Hii ni taarifa rasmi kutoka katika label yake Kennis Music  kuhusiana na kifo chake.
kwa niaba ya Kennis Music, nasikitika kuthibitisha rasmi kifo cha ghafla na kushtua cha pop satr wa Nigeria Goldie Harvey.

"Goldie, 31, amefariki alhamis baada ya kulalamika kupatwa na maumivu makali ya kichwa katika jumba lake lililopo park view, muda mfupi baada ya kurejea kutoka marekalani, alipoenda kushuhudia tuzo za Grammy. aliwahishwa katika hospitali anayotibiwa Reddington, Victoria Island, Lagos, ambapo madactari walisema amefariki baada tu ya kufika".

mwili wa marehem Goldie, umeshapelekwa katika mochuari  ya Lagos University Teaching Hospital iliyoko Ikeja, Lagos. Goldie aliiwakilisha Nigeria katika  Big Brother Star Game 2012.

Juhudi zake za  hivi karibuni, ni pamoja na single tatu kutoka katika album yake ya nne iliyokuwa inafata "African Invasion", "skibo", "Miliki" na "Got to have it" ambazo kwa sasa zinapata kuchezwa sana katika vituo mbali mbali vya redio na tv Africa.

Mipango ya mazishi itatangazwa na familia yake.."

Mungu ailaze roho ya marehem mahala pema peponi, Amen

Hii ni video ya ngoma aliyoshirikishwa na Ambwene Yessaya 'Skibobo'
 Goldie alikuwa amerejea Nigeria kutoka marekani ambako alihudhuria tuzo za Grammy akiwa na bosi wa record label yake Kennis music 'kenny Ogunbe'
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

No comments:

Post a Comment