Hatimaye
jeshi la Polisi linamshikilia mwanaume anayetuhumiwa kumnajisi, kumbaka
na kumlazimisha kula mbegu zake za kiume binti yake wa kambo.
Mwanaume
huyo, Adam Tuliani, maarufu kwa jina la Kiredio (37) mkazi wa kijiji
cha Mwandege, Wilaya ya Mkuranga, anadaiwa kumfanyia unyama huo mtoto
wake wa kambo mwenye umri wa miaka tisa .
Akitoa
taarifa hiyo, Kaimu Mkuu wa Kituo cha Polisi Vikindu, Inspekta wa
Polisi Bahati Ponela alisema kupatikana kwa mtuhumiwa huyo kunatokana na
juhudi zilizofanywa na Mkuu wa kituo hicho, Inspekta Joseph Ndifwa na
wananchi wa eneo hilo.
"Polisi
imemkamata mtuhumiwa leo (jana) baada ya juhudi kubwa ya kumsaka
iliyoongozwa na Mkuu wa kituo baada ya kuwa mafichoni kwa wiki moja,"
alisema inspekta Bahati.
Hata
hivyo, Inspekta bahati alisema tukio la mtoto huyo kufanyiwa ukatili
huo kwa miaka miwili mfululizo, halikuwahi kuripotiwa kwenye kituo na
kusababisha mtuhumiwa kutokamatwa haraka.
"Hakuna
mtu aliyekuja hapa kuripoti katika kipindi chote hicho kama
ilivyoelezwa, jambo hili baya na mkuu wangu asingesita kuchukua hatua za
haraka za kumkamata mtuhumiwa kama ilivyofanyika sasa," alisema
Inspekta bahati.
Awali ilibainika mtoto huyo alifanyiwa vitendo hivyo kwa miaka miwili mfululizo kuanzia mwaka 2011 hadi mwanzoni mwa mwaka huu.
Wakati
mtuhumiwa huyo akishikiliwa na polisi, imethibitika mtoto aliyefanyiwa
unyama huo ameambukizwa virusi vya Ukimwi na ana matatizo ya kutokwa na
haja sehemu zote za siri bila mwenyewe kujitambua.
Akizungumza
na NIPASHE Jumapili, mama mdogo wa mtoto huyo, Chiku Selemani, alisema
kwenye vipimo alivyofanyiwa katika Hospitali ya Mkuranga imeonyesha
mtoto huyo ameambukizwa virusi vya Ukimwi na sehemu zake za siri
zimeharibiwa kiasi cha kusababisha haja kutoka bila kujitambua.
Awali,
mtoto huyo alieleza jinsi alivyokuwa akilazimishwa kula mbegu hizo kila
siku wakati baba yake huyo alipomaliza kufanya mapenzi na mama yake
mzazi na baada ya kumuingilia yeye.
Alisema
wakati anafanyiwa vitendo hivyo, mama yake alikuwa akishuhudia na
wakati mwingine alimsihi asikatae kwa sababu watakosa chakula.
KITONGOJI CHAPIGWA BUTWAA
Mwenyekiti
wa kitongoji cha Mwandege, Abdallah Ngumbule alisema walikuwa
hawatambui kama mtoto huyo aliyeonekana kurandaranda mitaani alikuwa
akifanyiwa vitendo hivyo vya kikatili.
Ngumbule
alisema ofisi yake ilitambua kuwapo kwa hali hiyo kupitia vyombo vya
habari, na haraka walianza kushirikiana na polisi kumtafuta mtuhumiwa na
mke wake ambao wote walikuwa wametoroka.
"Huyu
mtoto tulikuwa tunamuona akizurura mitaani, lakini hatukujua kama
anakimbia mambo machafu ya baba yake. Tulipobaini jambo hili tuliungana
na polisi kuwatafuta mtuhumiwa ili akamatwe," alisema.
MAMA AOMBA MSAADA
Hata hivyo, Chiku ambaye ni mama mdogo wa binti huyo ameomba kusaidiwa katika kumtunza baada ya hali yake kuwa mbaya kiuchumi.
Alisema
madaktari wamemtaka kumpeleka mtoto huyo kwa ajili ya kupatiwa matibabu
kila mara, kitu ambacho alisema hataweza kwa kukosa pesa za nauli.
"Maisha
yangu magumu, sina kitu chochote cha kuniingizia kipato, naomba
Watanzania wenzangu wanisaidie katika jambo hili," alisema Chiku.
Kwa
mtu atakayeguswa na tukio hili na kutaka kutoa msaada wake, awasiliane
kwa kutumia namba za simu 0717336368, 0767377080 au 0683336368 au afike
ofisi za The Guardian.
Chanzo: Jestina George blog
No comments:
Post a Comment