Kwa mujibu wa chanzo makini, tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo dada huyo alikodi Bajaj hiyo toka nyumbani kwake, Kinondoni-Shamba jijini Dar kwenda kujirusha katika klabu moja ya usiku iliyopo Mwananyamala ndipo alipolizwa pochi hiyo iliyokuwa na fedha (zaidi ya elfu hamsini) pamoja na vitambulisho.
Chanzo hicho kilizidi kueleza kuwa, kabla hajafika klabu, dada huyo aliamua kumpitia shosti yake aliyekuwa katika Baa ya Uhuru Peak, Mwananyamala ili wakajirushe pamoja ndipo dereva huyo alipomfanyizia.
“Alipofika hapa Uhuru Peak akaacha pochi yake ndani ya Bajaj ili amshtue fasta rafiki yake ndipo dereva alipotumia mwanya huo kutokomea kusikojulikana,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya dakika kadhaa, dada huyo alitoka nje na kuanza kuangaza huku na huko ghafla akapata msala mwingine wa kutiwa mbaroni na Jeshi la Polisi lililokuwa katika msako wa kuwakamata machangudoa.
No comments:
Post a Comment