Mkuu
wa wilaya ya Singida,mwalimu Queen Mlozi, akitoa taarifa yake ya
utekelezaji wa ilani cha uchaguzi ya CCM kwa mkuu wa mkoa wa Singida
(aliyeketi) Dk.Parseko Kone.Dk.Kone alifanya ziara ya kiazi katika
manispaa ya Singida.(Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu.
Jumla
ya wanafunzi 139 wa shule za msingi katika halmashauri ya manispaa ya
Singida waliacha shule mwaka jana kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo
ya utoro.
Akitoa
taarifa yake ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM kwa mkuu wa
mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone aliyefanya ziara ya kikazi ya siku
moja katika manispaa ya Singida, Mkuu wa wilaya ya Singida Queen Mlozi
amesema jumla ya wanafunzi 118 kati yao wavulana 76 na wasichana
42,waliacha shule kutokana na utoro.
Amesema
wengine 11 waliacha shule kutokana na kukosa mahitaji muhimu na wawili
walifariki dunia katika kipindi hicho cha mwaka jana.
Akifafanua
zaidi, amesema kuwa utoro wa wanafunzi katika baadhi ya shule,
umeendelea kuwa tatizo kubwa hali inasababishwa na wanafunzi kujihusisha
na biashara ndogo ndogo, kuajiriwa na pia wazazi kutowapatia mahitaji
muhimu.
Aidha,
Mlozi aitaja baadhi ya mikakati ya kudhibiti utoro wa wanafunzi kuwa ni
pamoja na kuhamasisha na kuhimiza shule na jamii kuongeza vivutio
shuleni ikiwemo kuimarisha bendi za shule, michezo, kwaya na ngoma.
Mkuu
huyo wa wilaya, ametaja mikakati mingine kuwa ni kuhamasisha jamii
kuwapa watoto chakula cha mchana wawapo shuleni na orodha za watoro
kupelekwa kwa maafisa watendaji wa kata ili sheria zichukuliwe.
Wakati
huo huo, Mlozi amesema manispaa ya Singida inakabiliwa na upungufu wa
vyumba vya madarasa 274, nyumba za walimu 793, matundu ya vyoo 870 na
maktaba 43.
No comments:
Post a Comment