Mwanasiasa Nicolas Maduro ameapishwa rasmi kuwa rais wa Venezuela na kuchukua nafasi ya Hugo Chavez.
Akizungumza baada ya kuapishwa Maduro ametoa wito wa kufanyika mazungumzo na upinzani ili kuijenga nchi yao iwe bora zaidi.
Maduro
mwenye umri wa miaka 50 amesema anataka kuanza kipindi chake cha urais
kwa kuwataka watu wa Venezuela kuijenga nchi hiyo iwe ya amani.
Hata
hivyo, wakati akihutubia mbele ya marais, mawaziri wakuu na viongozi
wengine, hotuba hiyo ilivurugwa baada ya mtu mmoja kuvamia jukwaa na
kumpokonya kipaza sauti.
Akizungumza
baada ya tukio hilo lililoleta mkanganyiko, Maduro ameisema vikosi vya
usalama vimeshindwa kazi, kwani angeweza kuuawa.
Maduro
ameapishwa saa chache baada ya tume ya uchaguzi ya Venezuela kusema
itahesabu tena kura zilizosalia za uchaguzi wa Jumapili iliyopita
kufuatia mpinzani wake Henrique Capriles, kudai kura zihesabiwe upya.
No comments:
Post a Comment