HATIMAYE nguli wa sanaa za maigizo Bongo, Jacob Stephen Mbura ‘JB’ amelianika jimbo atakalogombea ubunge mwaka 2015.
JB
aliyaongea hayo mwanzoni mwa wiki hii, jijini Dar es Salaam ambapo
alisema macho yake yote yapo
Mkoa wa Dar es Salaam ambao una majimbo
nane.
JB:
Niliposema natangaza kugombea ubunge mwaka 2015 wengi waliamini ni
maneno tu, lakini nia yangu ni sahihi. Nitagombea na leo nasema jimbo
langu lipo Mkoa wa Dar es Salaam.
Aliongeza kuwa, jimbo atakalogombea
litaendelea kubaki kuwa siri ya moyo wake na meneja wake wa kampeni
ambaye hakupenda kumtaja jina.
Majimbo yanaounda mkoa wa Dar es
Salaam katika uwakilishi bungeni ni Ukonga, Ilala, Kinondoni, Segerea,
Kawe, Kigamboni, Ubungo na Temeke.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment