Staa
anayefanya poa katika sinema za Kibongo, Rose Donatus Ndauka amenaswa
akiwa kimahaba akifanya mambo ya chumbani hadharani na mchumba’ke,
Malick Bandawe, Ijumaa Wikienda limewapiga chabo.Tukio
hilo lililoshuhudiwa na mwanahabari wetu, lilijiri wikiendi katika
Ukumbi wa Hazina Lounge uliopo Coco Beach, Dar ambapo kulikuwa na
sherehe ya ‘bethidei’ ya mdogo wake Rose, Recho Ndauka.Baada ya kukolea
kwa ‘maji’, Rose na mwandani wake walianza kugandana kama ruba huku
wakifanyiana vitendo vya kimalavidavi.Wakati burudani zikiendelea
ukumbini hapo, wawili hao walijitenga pembeni na kuanza kumwagiana
mabusu mfululizo huku kila mmoja akijitahidi kuzionesha hisia za upendo
alizonazo kwa mwenzake, jambo lililowashangaza baadhi ya wageni
waalikwa.
“Makubwa
haya! Sijawahi kumuona Rose akiwa kimalovee hivi yaani leo ndiyo mara
ya kwanza ila kwa upande mwingine wanaendana na wanapendeza sema tu
hawataki kufunga hiyo ndoa jamani tuione,” alisikika dada mmoja
akijadili na mwenzake. Pamoja
na hayo, sherehe hiyo ya mdogo wake ilitawaliwa na vituko kibao baada
ya wageni waalikwa kukolea ‘maji’ kwani kulikuwa na pombe kali tu huku
wasichana wakiwa wamevalia vimini vilivyoacha wazi sehemu kubwa za
maungo nyeti hasa wakati wakiserebuka hivyo kuwatoa udenda wanaume
wakware.
Kwa hisani ya GLP
No comments:
Post a Comment