Mkali huyo wa ngoma ya Kesho alifunguka hayo kupitia
website yake alipokuwa akizinadi shoo hizo atakazofanya kwenye majiji ya London na Reading, Uingereza ambapo aliwataka warembo hasa Wabongo waishio humo kupendeza ili achague mmoja atakayekuwa mchumba wake.
Bila kujali mjadala utakaoibuka kwa kuwa tayari ana mchumba ambaye ni Penniel Mungilwa ‘Penny’, Diamond alifunguka: “Mashabiki wangu wa London na Reading kijana wenu nakuja kuweka historia kwa mara nyingine. Warembo mpendeze nakuja kuchagua mchumba mmoja wa kuja kumtambulisha kwa mama Diamond.”
MPEKUZI
No comments:
Post a Comment