Nimepata
kwa mshtuko na nikakataa kuamini kama ni kweli kuwa polisi wa Arusha
wamevamia na kuizingira nyumba ya mbunge mwenzangu wa Arusha, Lema.
Nimelazimika kumpigia simu RPC kuthibitisha na cha ajabu akaniambia ni kweli.
Nimemshauri kama kiongozi
mwenzake mwenye dhamana ya kusaidia kuilinda kweli na haki ili kuleta
Amani ya kweli kwenye mkoa wangu wa Arusha. Sidhani kama ni busara
kutaka kuvamia nyumbani kwa Raia mwema achilia mbali Kiongozi mkubwa
kama mbunge. "Kama watawala wanafanya hivi kwa mti mbichi, itakuwaje kwa
mti mkavu" itakuwaje kwa mwananchi wa kawaida anayeishi usa river au
unga ltd? Ukifuatilia na kuangalia video ya tukio la uhasibu chuoni
arusha, utagundua makosa ya mtawala mkuu wa mkoa, ambaye kimsingi ni
mkiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa kuwa sehemu ya sababu ya
uvunjifu wa amani, kutokujua hata kusoma saikolojia ya watu.
Nyumbani kwa mbunge hakai
mbunge mwenyewe. Kuna watoto akiwemo mwenye umri wa miezi mitano, mke,
ndugu etc. Utapigaje mabomu kwenye nyumba hii, bila shaka yatakuwa
mauaji. Lema si jambazi, ni kiongozi, ni role model, ni raia mwema sana
na mzalendo kwa taifa lake.
Hii wapi sababu ya kuvamia kwake usiku na kuwapa wanafamilia pychological tortue.
Kama amenielewa atasikia,
otherwise "truth will always stand" . Tuko tayari na tulishakuwa tayari,
hatujashtukizwa. Tunaendelea kuongezewa kura za madiwani arusha juni
16, 2013. Ni vyema watawala wakakumbuka habari ya Farao na Mungu juu ya
mateso ya wana wa Israel utumwani. "Mungu akaufanya moyo wa farao kuwa
mgumu, ili azidi kujidhihirisha kwa wana wa Israel"
Nassari.
No comments:
Post a Comment