Msanii mkongwe na maarufu nchini, Juma Kassin Kiroboto, aka Nature,
ameonyesha kukerwa na kile kilichoendelea jana usiku katika kipindi cha
burudani cha televishen inayotizamwa africa ya mashariki alipokuwa
akifanya nao interview. Nature alionekana akiwa amevaa kawosh na ndala
na mara baada ya mahojiano mafupi ya mwanzo ambapo mtangazaji alisema
watarejea baada ya mapumziko mafupi Nature hakuonekana tena.
Kilichotokea kwa mujibu wa Nature mwenyewe, ni wakati wa mapumziko
hayo, mtangazaji wa kipindi hicho alimfata na kumuambia kuwa hataendelea
na interview tena kwasababu ya mavazi aliyokuwa kavaa ambayo ni ndala
na kawosh. kuonyesha kukerwa kwake na ishu hiyo Nature aliamua kuandika
kupitia ukurasa wake wa facebook....
hivi kwa mfano angekuwepo mzungu pale na kavaa ndala wangesitisha
mahojiano na kuvaa kaoshi ni tatizo,kunywa nimekunywa bt kuna baya
nimeliongea na hivi kama kweri we nimuandishi wa habari unaruhusiwa
kuvaa vile kisheria kama yule mtangazaji nimeboreka kinoma na
ikiwezekana nasitisha kuanzia ssa kupeleka ngoma zangu pale siitaji
interview
No comments:
Post a Comment