Swahiliworldplanet kama kawaida yake ilimtafuta Batuli na kumueleza kila kitu ukiwemo ujumbe wa mashabiki wake na muigizaji huyo kusema kuwa ni kweli mwanae amefanana sana na Ray na suala hilo pia linaleta mvutano hata kwa wasanii wenzake lakini amesema kuwa hayuko tayari kuliweka wazi suala hilo kwa sasa ila atalizungumzia kwa kina siku zijazo ili watu na mashabiki wake waelewe kila kitu. "Ni kweli mwanangu amefanana sana na Ray hili linaleta mvutano hata kwa wasanii wenzangu. Ipo siku nitalijibu swali hili kwa ufasaha zaidi ila kwa sasa sipo tayari kuongea chochote" alisema muigizaji huyo aliyejaaliwa mvuto wa aina yake. Mtoto huyo pia anadaiwa kuwa na kipaji cha uigizaji na anatarajiwa kuonekana kwa mara ya kwanza hivi karibuni katika filamu inayoandaliwa na Batuli mwenyewe. Angalia picha ya Batuli na mtoto wake hapo chini......................
Batuli katika pozi
No comments:
Post a Comment