MTAYARISHAJI nguli wa
muziki wa kizazi kipya nchini, Joachim Kimario 'Master Jay' amesema amekosa
imani na Tuzo za Kilimanjaro Music, kwa kuwa zinalengo la kuwadhalilisha baadhi
ya wasanii.
Master jay amekosa
imani kumetokana na Kamati ya Kilimanjaro Academia ambayo imepewajukumu la
kuchagua wasanii kuingia kwenye kinyang'anyiro hicho kukosa sifa.
Akizungumza Dar es
Salaam juzi, Master Jay alisema tatizo linaanzia kwenye kamati hiyo kuchagua
wasanii waliokosa sifa na vigezo, huku ikiwa haiko wazi kwa wadau pamoja na
wasanii ambao ni washiriki wa tuzo hizo.
Alisema watu
waliochaguliwa kwenye kamati hiyo, wamekosa uelewa wa muziki na ndiyo maana
wanachagua baadhi ya wasanii waliokosa ubora na kusababisha kupoteza imani ya
tuzo hizo kwa jamii nzima.
Mtayarishaji huyo
alisema ndiyo maana baadhi ya wasanii wanajitoa kwenye kinyang'anyiro hicho kwa
kuogopa kujidhalilika.
"Sijui ni akina
nani wanaounda kamati hiyo kwani imepoteza sifa na ndipo tatizo linapoanzia
hapo kila mwaka, kukosa uelewa kwenye kamati hiyo na kutokuwa na uwazi
kunachangia malalamiko ya kila siku kwa baadhi ya wadau wa muziki.
"Baadhi ya
wasanii wanalalamika sana kuhusu tuzo hizi na ndiyo maana wengi wanajitoa, si
kwamba wanajitoa kwa kuogopa kushindana hapana bali kudhailika kwani hizi tuzo
sasa zinadhalilisha baadhi ya wasanii," alisema Master Jay
Hata hivyo
aliwapongeza kwa kuongeza vipengele vingine kwenye tuzo hizo, ambapo mwaka jana
kulikuwa na vipengere 29 na sasa vimeongezwa na kuwa 32.
"Kila mwaka
wanapiga hatua 10 mbele na kurudi hatua 30 nyuma, hali ambayo inaonesha hakuna
maendeleo yoyote kwenye upande wa tuzo hizo, hivyo wanahitaji marekebisho ili
kuwe na usawa na kurudisha imani ya tuzo hizo kwa wasanii," alisema Master
Jay.
Kwa upande wake
Mratibu wa tuzo hizo kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Angelo Luhala
alisema tatizo lipo kwa waandaaji ambao ni Kampuni Bia Tanzania (TBL) kushindwa
kutoa elimu ya kutosha kwa wadau wote wa muziki nchini.
Alisema TBL inatakiwa
kuelimisha umma kujua kazi ya Kilimanjaro Academia, inavyofanya kazi pamoja na
mchakato mzima wa tuzo hizo zinavyokwenda, ili kuepuka ulalamikaji unaojitokeza
kwa baadhi ya wadau wa muziki.
"Elimu ikitolewa
kwa washiriki pamoja na wadau wa muziki, imani itarudi kwenye tuzo hizo na
watajua mchakato mzima unavyofanyika hivyo uwazi wa jambo hilii ndiyo
utapunguza malalamiko katika tuzo hizo," alisma Luhala.
No comments:
Post a Comment