Wema ambaye ni Miss Tanzania mwaka 2006, huku akifurukuta kwenye tasnia
ya filamu za Kibongo, ametokelezea na mwanaume huyo aliyetajwa kwa jina
moja la Raheem katika mitandao mbalimbali ya kijamii.
GUMZO MITANDAONI
Picha hiyo ambayo pozi lake ni ‘very romantic’ imezua gumzo katika
mitandao mbalimbali ilipotundikwa na wadau wengi walionekana kuamini
kuwa Wema alikuwa akimnadi mpenzi wake mpya.
Mtoa maoni mmoja aliandika: “Naona Wema ameamua kutuonesha shem wetu mpya, sasa hapo kazi kwa wenye vijicho.”
Mwingine aliandika: “Mmh! Mbona (Raheem) haonekani uso? Kama lengo lake
lilikuwa kumwanika angemuacha tu aonekane ila dah! Ana kifua kizuri
sana. Huyu jamaa anaonekana anafanya sana mazoezi.”
DIAMOND ATAJWA
Katika gumzo hilo, wengine walikwenda mbali zaidi, wakisema kwamba
inawezekana Wema alikuwa na Raheem kwa siri muda mrefu lakini sasa
ameamua kuvunja ukimya ili kumringishia x – boyfriend wake, Nasibu Abdul
‘Diamond’.
“Siku zote alikuwa wapi? Atakuwa anamwoneshea Diamond tu huyu,” mtoa maoni mwingine aliandika.
INTERVIEW NA RAHEEM
Ni jadi ya magazeti ya Global Publishers likiwemo hili la Risasi
Mchanganyiko kutafuta mzani wa habari kabla ya kwenda hewani hivyo
lilimtafuta Raheem ambaye alitoa ushirikiano wa kutosha.
Raheem alikiri kuitambua picha yake na Wema lakini alisema imemshtua na
kumcha-nganya maana hakutegemea kama ingefika mitandaoni na hatimaye
kwenye vyombo vya habari.
Alisema: “Ni kweli nilipiga hiyo picha na Wema lakini ni ya kawaida tu,
haina maana nyingine tofauti. Wema ni rafiki yangu na dada yangu.
Tunaheshimiana, hakuna cha zaidi.
“Wema ni maarufu na watu wanaweza kujaji wanavyotaka, hilo
litanisababishia matatizo kwa sababu mimi nina mpenzi wangu na Wema si
mtu wangu kabisa…she is just my sister (ni dada yangu tu).”
Risasi: Hiyo picha mlipiga lini, wapi na kwa matumizi gani?
Raheem: Ilikuwa kwenye function (tukio) fulani ambayo siwezi
kuizungumzia. Kama wiki sita au miezi miwili hivi iliyopita na tulipiga
kama marafiki tu, hakuna cha zaidi.
Risasi: Kwa hiyo Wema akithibitisha wewe ni mpenzi wake itakuwaje?
Raheem: Nitamshangaa sana! Wema ni dada yangu tu.
Risasi: Inasemekana Wema ameamua kuianika hiyo picha kwa lengo la kumrusha roho Diamond, unasemaje hapo?
Raheem: Sijui na kwa kweli siwezi kuzungumzia mambo ya mtu binafsi. Sijui chochote.
Wema alipatikana na kusomewa mashitaka yake ambapo alikiri kupiga picha
na Raheem, akafafanua kuwa aliipiga muda mfupi baada ya kutoka kufanya
interview na kituo kimoja cha redio (jina kapuni) lakini akasema haina
uhusiano wowote na suala la mapenzi.
“Ni kweli nilipiga hiyo picha, yeye aliniomba tu kama fan (shabiki)
wangu, akataka ku-show love (kuonesha upendo), sikuona sababu ya
kumkatalia. Nakumbuka siku hiyo nilikuwa na Martin (Kadinda – meneja
wake) na baada ya siku hiyo sijawahi kuonana naye tena mahali
popote…sioni tatizo kabisa, ni kawaida kwa sisi mastaa,” alisema Wema.
Risasi: Lakini Wema wadau wanasema eti ni mpenzi wako na umefanya hivyo kwa lengo la kumrusha roho Diamond.
Wema: Umeshasema wadau, waache na mambo yao lakini maelezo yangu ni hayo na naamini yamejitosheleza.
Risasi: Kuna kitu nahitaji ufafanue zaidi…lile pozi lipo romantic sana,
hufikiri kuwa inaweza kuwa sababu ya watu kuwa na hisia kwamba ni mpenzi
wako?
Wema: Ni kweli picha ni romantic lakini yule kijana (Raheem) si mpenzi wangu. Naomba nieleweke hivyo. Ahsante
No comments:
Post a Comment