Mwanamitindo wa kimataifa wa Tanzania, Flaviana Matata.
Na Mwandishi Wetu
Mwanamitindo
wa kimataifa wa Tanzania, Flaviana Matata kesho atashiriki katika misa
maalum ya kuwakumbuka watanzania waliopoteza maisha katika ajali ya MV
Bukoba mwaka 1996.
Misa
hiyo itafanyika kwenye eneo la makaburi ya kumbukumbu ya MV Bukoba
ambapo Flaviana alipoteza mama yake mzazi na kaka yake katika ajali
hiyo.
Mwaka
jana, mwanamitindo huyu kupitia shirika lake la Flaviana Matata
Foundation alitoa msaada wa maboya yaani vyombo vya kuokoa maisha majini
(life vests) 500 kwa mawakala wa meli ya serikali yaani Marine Services
Ltd ikiwa ni nja moja ya kujaribu kusaidia usalama majini.
Mkurugenzi
wa kampuni ya Compass Communications, Maria Sarungi alisema kuwa mbali
ya kushiriki katika misa hiyo, pia mwana mitindo huyo atafanya
mazungumzo na wadau mbali mbali jinsi ya kuendeleza juhudi za kuimarisha
usalama majini.
Flaviana
amesema kuwa juhudi zake kubwa kwa hivi sasa ni kuhakikisha kuwa ajali
za vyombo vya kwenye maji zinaepukika na ndiyo maana anapigana huku na
kule katika sakata hilo.
Amesema
kuwa lengo lake kubwa ni kuona vyombo vya kuokolea katika kila meli
vinapatikana na hasa kwa kutafuta misaada kwa wadau mbali mbali.
“Suala
la usalama majini bado haujatiliwa mkazo vya kutosha na jamii pamoja na
serikali” alieleza mwanamitindo huyu. “Muda umefika kwa wahusika wote
kushirikiana kwa pamoja kuzungumzia na kukabiliana na changamoto hii”
amesema Matata.
No comments:
Post a Comment