Filamu
inayoitwa “Without Daddy” ambayo imekua ikipikwa kwa muda mrefu sasa,
inatoka leo. Filamu hiyo ina upekee fulani sababu itakua ni filamu ya
kwanza ambayo Mama yake marehemu Steven kanumba ameigiza.
Watu wengi wana hamu kuangalia movie hii kwa sababu mbalimbali.
Wengine wanataka wapime kipaji chake, wengine ku-show support kwa mama
wa msanii kipenzi chao wanayem-miss… Steven Kanumba.
Utabiri wangu ni kwamba mama atakuwa mkali kwenye kuigiza. Sababu?
Kwanza yuko comfortable mbele ya kamera kwa interview mbalimbali
nilizomuona. Pili asilimia kubwa ya kina mama wana uwezo wa kuigiza
sababu sehemu kubwa ya maisha yao ni kuigiza mbele ya watoto, kama vile
wanapotumia ucheshi kuficha ugumu au ukubwa wa tatizo ili watoto
wasi-panic. Tatu yeye ndiye aliyezaa kipaji, Steven Kanumba, hivyo kuna
uwezekano mkubwa personality na ucheshi aliokua nao hayati Kanumba kwa
kiasi fulani aliridhi kutoka kwa mama yake
No comments:
Post a Comment