KWA mujibu wa taarifa iliyotolewa na
baba yake mdogo kupitia East Africa Radio leo asubuhi, mazishi ya rapper Albert
Mangwea aliyefariki jana katika hospitali ya St. Helen jijini Johannes
burg,
Afrika Kusini yanaweza kufanyika mjini Morogoro.
“Tumekubaliana kwamba tumelazimika
kuzika Morogoro kwasababu huyu kaka yetu ambaye ni baba wa marehemu tumemzika
pale Morogoro na familia yote ya marehemu ipo pale Morogoro.
Lakini hapa Dar es
Salaam tutafanya mapokezi na msiba utakuwa hapo kwa kaka yangu ni sehemu za
Mbezi hapo, kwahiyo tutakuwa kwa kaka yangu anaitwa David Mangwea,” amesema.
Ameongeza kuwa taarifa hizo za msiba nao
walizipata jana jioni lakini bado hawajawa na uhakika ni vipi mwili wa marehemu
utaletwa nchini kutokea Afrika Kusini.
“Kitu tunachokifanya na tumewaagiza tu
hao vijana wetu waliopo hapo Dar es Salaam wajaribu kuwasiliana na ubalozi wa
Afrika Kusini kuona namna gani ambavyo tunaweza kupata more information na
kiasi kwamba tukaweza kujua namna gani msiba utakuja hapa.”
Mpaka sasa bado haijajulikana mwili wa
marehemu Mangwea utakuja lini nchini.
CHANZO JUMA MTANDA BLOG
CHANZO JUMA MTANDA BLOG
No comments:
Post a Comment