MSANII wa maigizo, Salma Jabu ‘Nisha,’ amedaiwa kuwatosa watoto yatima waliokuwa wakimsubiri baada ya kuweka ahadi kuwa angekwenda kuwatembelea na kuwapa msaada.
Tukio hilo lilitokea hivi karibuni ambapo Nisha aliahidi kwenda kuwapa msaada watoto yatima wa kituo cha Hisan Orphan Center kilichopo maeneo ya Mbagala Charambe, jijini Dar lakini ulipofika muda, hakutokea.
Rafiki wa karibu na staa huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake, alipoulizwa kulikoni alikiri kutotoa taarifa kwa uongozi wa kituo hicho cha watoto yatima na kudai walikuwa na dharura siku hiyo.
“Kuna tatizo lilitokea ikabidi tughairi. Tunaomba radhi kwa kuwafanya wasubiri sana ila niwaambie kuwa mpango wa Nisha kuwatembelea watoto yatima bado upo palepale,” alisema
No comments:
Post a Comment