Jide na Mumewe wakiwasili mahakamani leo.
Msanii
wa muziki wa kizazi kipya, Judith Wambura Mbibo a.k.a Lady
Jaydee(Pichani) muda si mrefu amepokea hati yake ya mashtaka kutoka
katika mahakama ya Kinondoni ambapo ameshtakiwa na Mkurugenzi wa vipindi
wa Clouds FM baada ya kuwa na kutofautiana kwa muda.
Jaydee ambaye alikuwa Baraza la
Sanaa ambapo alikuwa akiongea katika jukwaa la wasanii, alipata ujumbe
wa kuitwa mahakamani na alipofika alikabidhiwa hati hiyo ambayo mwenyewe
alikataa kusema makosa aliyoorodheshewa, na kusema kwamba anataka
kwanza awasiliane na mwanasheria wake.
Kikubwa ambacho aliweza kusema kwa
waandishi waliokuwa wameongozana naye ni kwamba, kesi itaanza kuunguruma
tar 27 mahakamani hapo
No comments:
Post a Comment