Meli ikiwa inazama na ikiwa imezungukwa na mitumbwi pamoja na boti ambazo zilisaidia kwenye uhokoaji
MV Bukoba ikiwa inazama ilikuwa ni tarehe 21 mei 1996
Makaburi ya Igoma ambako ndugu zetu waliokuwa wakisafiri kwa meli ya MV Bukoba walizikwa.
RIPOTI
ya Tume ya Jaji Robert Kisanga, iliyochunguza chanzo cha ajali ya mv
Bukoba, inasema usiku wa kuamkia siku ya ajali, meli hiyo ilipakia
abiria kati ya 750 na 800 pamoja na wafanyakazi 37.
Kati ya hao, 114 waliokolewa wakiwa hai; wakati 391 waliopolewa
wakiwa wamefariki na kuzikwa katika makaburi ya Igoma, nje kidogo ya
Jiji la Mwanza. Miili mingine ilichukuliwa na jamaa kuzikwa kwao. Jumla
ya miili 332 haikupatikana.
Kila mwaka, ifikapo Mei 21, serikali inayosema haina dini, huongozana
na viongozi wa madhehebu ya dini na waganga, kwenda eneo la ajali
kufanya kumbukumbu.
Serikali ilishitaki aliyekuwa nahodha wa mv Bukoba, Jumanne
Rume-Mwiru, (sasa marehemu), Mkaguzi wa Mamlaka ya Bandari Gilbert
Mokiwa; aliyekuwa Meneja wa Bandari ya Bukoba, Alphonce Sambo, na
aliyekuwa Maneja wa Bandari ya Kemondo, Prosper Lugumila.
Kesi hiyo Na. 22 ya mwaka 1998, ilianza kusikilizwa Mei 14 mwaka
2001. Miongoni mwa waendesha mashitaka katika kesi hiyo ni Eliezer
Feleshi.
Hukumu ya kesi ilitolewa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Juxton
Mlay (sasa mstaafu), Ijumaa, 29 Novemba 2002, majira ya saa sita
mchana.
Washitakiwa wote walishinda kesi, kufuatia hukumu ya kurasa 118
iliyosomwa kwa dakika 160 na Jaji Mlay kusema, mv Bukoba ilizama kwa
sababu haikuwa na uwiano wa majini na siyo uzembe wa washitakiwa.
Serikali iliahidi kukata rufaa; lakini hadi leo majaliwa ya rufaa
hiyo hayajulikani; na baadhi ya washitakiwa wamefariki dunia bila kujua
hatma ya kesi hiyo wala stahili zao.
Kwa kipindi kirefu, mv Bukoba ilikuwa ‘kaburi’ lenye kuelea katika
Ziwa Victoria. Ilikwishapigwa marufuku kufanya safari kwa kuwa haikuwa
na viwango vya ubora wa kuwa majini.
Meli hii ilijengwa na kampuni ya Kibelgiji; ikazinduliwa 27 Julai 1979. Siku ya uzinduzi, ilibainika haikuwa thabiti na ilikosa uwiano
No comments:
Post a Comment