Rais Jakaya Kikwete
Profesa
Lipumba alisema hiyo inatokana na wasiwasi kuwa mchakato wa Katiba Mpya
hautaweza kukamilika mwaka 2014 hivyo kutokuwa rahisi kwa uchaguzi
kufanyika mwaka 2015.
Akizungumza
Dar es Salaam jana, wakati akifungua kikao cha Baraza Kuu la CUF,
Profesa Lipumba alisema kuwa Serikali inataka kuongezewa muda wa kukaa
madarakani kwa miaka miwili ikimaanisha kuwa Serikali ya Awamu ya Nne
chini ya Rais Jakaya Kikwete itakaa madarakani hadi mwaka 2017.
Hata
hivyo, madai hayo ya Profesa Lipumba yamepingwa vikali na Serikali na
viongozi wake watatu waandamizi ambapo walijibu walipoulizwa kwa
maandishi na mwandishi wetu mjini Dodoma wanakohudhuria kikao cha Bunge.
Waziri
wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe alijibu: “Mchakato wa Katiba upo
‘on track’ (unakwenda vizuri) hatuna sababu ya kufanya hivyo.”
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema alijibu” “Njooni ofisini kwangu nitasema ni kitu gani.”
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi
alijibu kwa utani bila ya kufafanua: “Njooni niwajuze, unajua kamba
haitoki Ukambani kama ilivyo kamba.”
Profesa
Lipumba amemwomba Rais Kikwete asilikubali wazo hilo akisema wananchi
hawatakubali na taifa linaweza kuingia katika mtafaruku.
“Nitapenda
kuona Rais Kikwete akikataa jambo hilo kwani litachafua taswira ya
nchi. Hatua hii ni kinyume cha utawala bora,” alisema Profesa Lipumba.
Alisema
Serikali haipaswi kuhofia uchaguzi kwa sababu ya Katiba kwani bado
uwezekano wa kuandaa uchaguzi wa haki na huru unawezekana kwa utaratibu
mwingine.
“Mchakato
wa Katiba unaendelea, Tume ya Mabadiliko ya Katiba inatuambia kwamba
mwaka 2014 tutakuwa na Katiba Mpya, sasa CUF tunasema kwamba hata kama
Katiba Mpya haitapatikana kwa kipindi hicho kuwe na Tume huru ya
Uchaguzi,” alisema Profesa Lipumba.
Jukwaa la Katiba kutinga mahakamani
Siku
nne baada ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba kutoa rasimu ya mwongozo
kuhusu uundwaji wa Mabaraza ya Katiba, Jukwaa la Katiba Tanzania
(Jukata), limesema litafungua kesi mahakamani kutaka kusitishwa kwa
mchakato mzima wa Katiba Mpya kwa madai kuwa uendeshwaji wake umejaa
mizengwe, itikadi za vyama na rushwa. Limetaja sababu tano ambazo
zimekiukwa.
Limesema
kesi hiyo itasimamiwa na timu ya mawakili 10 watakaoongozwa na
Mwanasheria wa masuala ya Haki za Binadamu, Dk Rugemeleza Nshala na
itawasilishwa mahakamani siku saba zijazo kuanzia jana.
Akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Jukata, Deus
Kibamba alitaja sababu hizo kuwa ni kutokufanyiwa marekebisho katika
sehemu tatu za Sheria ya Mabadiliko ya Katiba kama ilivyoahidiwa na Rais
Kikwete, kuvurugwa kwa Uchaguzi wa Mabaraza ya Katiba, mchakato wa
Katiba kukosa uongozi, kuminywa kwa demokrasia wakati wa mchakato huo
pamoja na Jukwaa hilo kuzuiwa kuonana na Rais ili kueleza upungufu
uliopo.
Chanzo: Gazeti la Mwananchi
No comments:
Post a Comment