Monday, April 22, 2013

WANAWAKE WAUNGANA KUSUSIA BIDHAA NA MAONYESHO YA MWANAMUZIKI DIAMOND



Kwa Kumdhalilisha Bi.Wema Sepetu kwa kumrekodi katika simu na kusambaza mazungumzo nyeti !
Kitendo cha Mwanamuziki wa kizazi kipya Nasibu Abdul Juma maarufu kama Diamond,cha kurekodi mazungumzo yake na star wa Bongo Move Bi.Wema Sepetu,
na kuyatuma mazungumzo yao ya mapenzi katika mitandao ni kitendo cha "Udhalilishaji wa Mwanamke" . kwa kuwa wanamuziki na wasanii wote wanatakiwa wawe ni mfamo na kioo cha jamii katika kuielekeza jamii kuishi 
kwa kufuata na kuheshimu maadili ,lakini mwanamuziki Diamond ameonekana kuwa ni  kiongozi wa "Udhalilishaji wa Mwanamke" kufuatia kitendo chake cha
kurekodi na kusambaza mazungumzo yao ya simu  ya kimapaenzi kati yake na
Bi.Wema Sepetu na mpenzi wake wa sasa Bi.Penny,kitendo hiki ni cha "kuwadhalilisha wanawake wa kitanzania"Tunaowaomba akinamama
na kinadada na wanawake wote kwa ujumla kususia kununua video,vcd,cd
pia kugomea kuhudhuria onyesho lolote lile litakalofanywa na mwamuziki
Nasibu Abdul Juma aka Diamond hadi pale atakapo waomba radhi wanawake wote
wa kitanzania popote pale walipo.
Wanawake wote wanatakiwa kugomea maonyesho ya mwanamuziki huyo na
na kutonunua bidhaa za mwanamuziki huyo Diamond ili kukomesha kabisa tabia hizi chafu za "Udhalilishaji wa Mwanamke" 
Wanawake wote ambao wamempa like au ad katika mitandao kama facebook kujiondoa mara moja na kogemea kununua jarida au gazeti lolote  litakalo mpamba mwanamuziki huyo.
MWARICK JAPHET MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

1 comment:

  1. HUU NDIO MWISHO WAKE SASA ITABIDI DIAMOND ARUDI MBAGARA KUUZA MACHUNGWA

    ReplyDelete