Monday, April 22, 2013

ROSE NDAUKA ANASWA KIMAHABA HADHARANIStaa anayefanya poa katika sinema za Kibongo, Rose Donatus Ndauka amenaswa akiwa kimahaba akifanya mambo ya chumbani hadharani na mchumba’ke, Malick Bandawe, Ijumaa Wikienda limewapiga chabo.Tukio hilo lililoshuhudiwa na mwanahabari wetu, lilijiri wikiendi katika Ukumbi wa Hazina Lounge uliopo Coco Beach, Dar ambapo kulikuwa na sherehe ya ‘bethidei’ ya mdogo wake Rose, Recho Ndauka.Baada ya kukolea kwa ‘maji’, Rose na mwandani wake walianza kugandana kama ruba huku wakifanyiana vitendo vya  kimalavidavi.Wakati burudani zikiendelea ukumbini hapo, wawili hao walijitenga pembeni na kuanza kumwagiana mabusu mfululizo huku kila mmoja akijitahidi kuzionesha hisia za upendo alizonazo kwa mwenzake, jambo lililowashangaza baadhi ya wageni waalikwa.


“Makubwa haya! Sijawahi kumuona Rose akiwa kimalovee hivi yaani leo ndiyo mara ya kwanza ila kwa upande mwingine wanaendana na wanapendeza sema tu hawataki kufunga hiyo ndoa jamani tuione,” alisikika dada mmoja akijadili na mwenzake.  Pamoja na hayo, sherehe hiyo ya mdogo wake ilitawaliwa na vituko kibao baada ya wageni waalikwa kukolea ‘maji’ kwani kulikuwa na pombe kali tu huku wasichana wakiwa wamevalia vimini vilivyoacha wazi sehemu kubwa za maungo nyeti hasa wakati wakiserebuka hivyo kuwatoa udenda wanaume wakware.


Kwa hisani ya GLP
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

No comments:

Post a Comment