Saturday, April 27, 2013

HAYA NDIYO MAKOSA MATATU YALIYOMNYIMA DHAMANA MBUNGE WA ARUSHA MJINI GODBLESS LEMA JANA JIONI NA KUSUBIRI KUFIKISHWA MAHAKAMANI JUMATATU


Mambo yaliyomfanya Mbunge wa arusha Godbless Lema akamatwe na kunyimwa dhamana jana  jioni ni haya yafuatayo baada ya kuongea na Mwanasheria wa Lema wakili Humphrey Mtui
i)Kosa la kwanza ni..
kuwaambia wanafunzi wa chuo cha uhasibu alipoenda kuwatuliza kuwa ‘dhambi kubwa kuliko zote ni woga ‘.Haki hutafutwa na kupiganiwa ikiwa jambo unalipigania ni la msingi na linafaa kupiganiwa(Worth fighting for)

ii)Kosa la pili ni pale alipotamka kuwa ‘’Tumemtafuta mkuu wa mkoa juu ya Matatizo yenu na mlivyoshuhudia hapa amechukua muda mrefu na kuingia kama vile anaingia kwenye send-off.Hawa ndiyo viongozi wetu ambao hawajali matatizo ya wananchi’’Kwa hiyo huo ni uchochezi

iii)Kosa la Tatu ni pale alipotamka kuwaambia wanafunzi kuwa ‘’Mimi Mbunge wenu nipo sambamba nanyi hadi mpate haki yenu na ikiwa mkuu wa mkoa hatakuja hapa kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi wa mkoa nitawaongoza hadi ofisini kwake ili mpate majibu na haki yenu kwani ni haki yenu ya msingi kwa mujibu wa katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ambayo niliapa kuilinda Bungeni na pia inaruhusiwa kwa mujibu wa kikanuni na kifalsafa katika utekelezaji wa utawala bora wa kidemokrasia ambao msingi wake ni kusikilizwa na kulinda haki za binadamu’’Huu nao umeitwa kwamba ni uchochezi.

Maneno ya hapo juu ndiyo yaliyosababisha jeshi la polisi kuvamia nyumbani kwake usiku wa manane ....

Huo umeitwa uchochezi baada ya mkuu wa mkoa kumtumia ujumbe wa mkononi kupitia simu yake kupitia namba 075296027*  aliyotishia kumbambikizia kesi anayoitaka yeye
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

No comments:

Post a Comment