Monday, April 22, 2013

Mkuu wa wilaya ya Singida adai wanafunzi 118 wameacha shule mwaka jana kutokana na utoro.



Mkuu wa wilaya ya Singida,mwalimu Queen Mlozi, akitoa taarifa yake ya utekelezaji wa ilani cha uchaguzi ya CCM kwa mkuu wa mkoa wa Singida (aliyeketi) Dk.Parseko Kone.Dk.Kone alifanya ziara  ya kiazi katika manispaa ya Singida.(Picha na Nathaniel Limu).

Na  Nathaniel Limu.
Jumla ya wanafunzi 139 wa shule za msingi katika halmashauri ya manispaa ya Singida waliacha shule mwaka jana kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ya utoro.

Akitoa taarifa yake ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM kwa mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone aliyefanya ziara ya kikazi ya siku moja katika manispaa ya Singida, Mkuu  wa wilaya ya Singida Queen Mlozi amesema jumla ya wanafunzi 118 kati yao wavulana 76 na wasichana 42,waliacha shule kutokana na utoro.

Amesema wengine 11 waliacha shule kutokana na kukosa mahitaji muhimu na wawili walifariki dunia katika kipindi hicho cha mwaka jana.

Akifafanua zaidi, amesema kuwa utoro wa wanafunzi katika baadhi ya shule, umeendelea kuwa tatizo kubwa hali inasababishwa na wanafunzi kujihusisha na biashara ndogo ndogo, kuajiriwa na pia wazazi kutowapatia mahitaji muhimu.

Aidha, Mlozi aitaja baadhi ya mikakati ya kudhibiti utoro wa wanafunzi kuwa ni pamoja na kuhamasisha na kuhimiza shule na jamii kuongeza vivutio shuleni ikiwemo kuimarisha bendi za shule, michezo, kwaya na ngoma.

Mkuu huyo wa wilaya, ametaja mikakati mingine kuwa ni kuhamasisha jamii kuwapa watoto chakula cha mchana wawapo shuleni na orodha za watoro kupelekwa kwa maafisa watendaji wa kata ili sheria zichukuliwe.

Wakati huo huo, Mlozi amesema manispaa ya Singida inakabiliwa na upungufu wa vyumba vya madarasa 274, nyumba za walimu 793, matundu ya vyoo 870 na maktaba 43.

MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

No comments:

Post a Comment