Friday, April 5, 2013

RAY ASALIMU AMRI BAADA YA KUKUBALI KUACHANA NA FILAMU YAKE ILIYODAIWA KUWA INA UDHALILISHAJI MKUBWA



HATIMA ya filamu ya mwigizaji, Vincent Kigosi ‘Ray’, Sister Mary iliyokuwa imezuiwa kwa kudaiwa kudhalilisha ukatoliki, imefahamika kuwa mwigizaji huyo amesalimu amri ya viongozi wa kanisa hilo.


 
Cover la filamu hiyo ya Sister Marry.
Kanisa Katoliki nchini linaloongozwa na Muadhama Polycarp Kadinali Pengo, liliizuia filamu hiyo kwa kile kilichodaiwa kuwa ilikuwa ikionesha udhalilishaji kwa namna ambavyo watawa wamevaa mavazi mafupi.
Baadhi ya vipande vilivyomo katika filamu hiyo.
Akipiga stori na mwandishi wetu, Ray amebainisha kuwa baada ya kuambiwa achomoe vipande vingi kwenye filamu hiyo, ameona ni bora kuachana nayo kwani hata akitoa haitaleta maana hivyo atakujairudia upya wakati mwingine. 

“Asilimia 85 ya filamu niliigizia kanisani na ndivyo walivyosema niviondoe, sina ujanja kwa sasa nimeanza kushuti filamu nyingine kabisa ile labda nije kuirudia upya hapo baadaye,” alisema Ray.



MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

No comments:

Post a Comment