Wednesday, April 24, 2013

PICHA NA TAARIFA KUTOKA KWA MWANAFUNZI WA ARUSHA, KUHUSU MWANAFUNZI MWENZAKE ALIYE UWAWA KIKATILI.




Huyu Ndio Henry Aliye Uwawa

Mbunge Wa Arusha Mjini Godbless Lema Akiwatuliza Wanafunzi Wa Chuo Hicho


Taarifa Kutoka Kwa Mwanafunzi Mwandishi Kuhusu Taarifa Zinazo Sambaa Kwenye Chuo Cha Uhasibu Arusha Inasema Kuna Kijana Anaitwa Henry Ni Mwanafunzi Wa BEF 2 Kwenye Chuo Cha Uhasibu Arusha Eneo La Njiro, Alikuwa Masomoni Mida Ya Usiku Na Alipomaliza Aliondoka Na Kuelekea Maeneo Ya Esami, Kabla Hajafika Eneo La Malazi Yani Hostel Alipigiwa Simu Na Mwenzake Amsubiri Ili Waende Wote Hostel. Inasemekana Wakati Anamsubiri Rafiki Yake Kwenda Hostel, Kuna Bajaj Ilifika Eneo Hilo Na Watu Hao Wasiojulikana Wakataka Pesa Kutoka Kwa Mwanafunzi Huyo, Majibu Ya Wanafunzi Hao Hayakuwafurahisha Watu Hao Na Ndio Walipochomoa Kisu Na Kumchoma Mmoja Ya Vijana Hao Tumboni Na Shingoni na Kupoteza Maisha Hapo Hapo, Rafiki Aliye Kuwa Nae Inasemekana Alichomwa Kisu Cha Tumboni Na Kuachwa Akishuhudia Mwenzake Akipoteza Maisha.
MWARICK JAPHET TEKELE MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

No comments:

Post a Comment