JB aliyaongea hayo mwanzoni mwa wiki hii, jijini Dar es Salaam ambapo alisema macho yake yote yapo
Mkoa wa Dar es Salaam ambao una majimbo nane.
JB: Niliposema natangaza kugombea ubunge mwaka 2015 wengi waliamini ni maneno tu, lakini nia yangu ni sahihi. Nitagombea na leo nasema jimbo langu lipo Mkoa wa Dar es Salaam.
Aliongeza kuwa, jimbo atakalogombea litaendelea kubaki kuwa siri ya moyo wake na meneja wake wa kampeni ambaye hakupenda kumtaja jina.
Majimbo yanaounda mkoa wa Dar es Salaam katika uwakilishi bungeni ni Ukonga, Ilala, Kinondoni, Segerea, Kawe, Kigamboni, Ubungo na Temeke.