Kaimu Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Tatu Burhan
Jumla
ya watu 12, 864, wakiwemo Watanzania na raia wa nje, wamekamatwa na
kufikishwa kwenye vyombo vya dola kwa kosa la kujihusisha na biashara
haramu ya kusafirisha binadamu.
Akizungumza
na NIPASHE jijini Dar es Salaam jana, Kaimu Msemaji Mkuu wa Idara ya
Uhamiaji, Tatu Burhan, alisema kukamatwa kwa watu hao kumetokana na
kuimarishwa kwa mfumo wa usimamizi wa mipaka na udhibiti.
Alisema
raia wa nje wanaofanyabiashara hiyo wanashirikiana na wenyeji, jambo
ambalo ni hatari kwa usalama wa nchi, hivyo ni vyema wakaacha tabia hiyo
kwa kuweka uzalendo mbele.
Aidha,
aliiomba serikali kuongeza vifaa vya kisasa kutokana na kuwepo kwa
mbinu mpya na matumizi ya silaha na kuingizwa kwa silaha za kivita
ambazo hutumika kuleta madhara kwa jamii.
Idara
hiyo nchi nzima ina askari wasiozidi 3,000 huku mahitaji yakiwa ni
8,000, ambapo mpaka wa Tanzania ukiwa mkubwa unaopakana na nchi nyingi
na kutumiwa kama njia ya kwenda nchi nyingine.
Alisema
biashara hiyo imekithiri zaidi katika nchi za Ethiopia, Somalia na
Bagladesh, ambao wengi huingia kwa lengo la kupita njia na wengine
kuweka makazi kwa sababu mbalimbali zinazowasababisha kuzikimbia nchi
zao.
Alisema
nchi nzima kuna vituo 58, huku kukiwa na umbali wa zaidi ya kilomita
200 kutoka kituo kimoja hadi kingine na kutolea mfano kituo cha Tanga
hadi Mtwara kikiwa na umbali wa kilomita 1,200 kwa ukanda wa bahari.
Aidha,
alisema hadi kufikia Desemba 2012, idara imetoa pasipoti 537,426 kati
ya hizo za kawaida ni 518,561, kidiplomasia 4,753, kiutumishi 1,499 na
za Afrika Mashariki 1,2613.
Burhan
alisema kwa mujibu wa takwimu hizo, Watanzania wengi wamewezeshwa
kusafiri nje ya nchi kwa shughuli mbalimbali zikiwemo za biashara,
ajira, masomo, matibabu na nyinginezo.
CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment