Wapiga kura tayari kwa foleni katika mtaa wa Kibera |
Hii leo
wakenya wanapiga kura katika uchaguzi wa kihistoria chini ya katiba
mpya. Foleni tayari zimeanza kushuhudiwa katika vituo.
Kinyang'anyiro ni kikali kati ya Muungano wa Cord na Jubilee wa Raila Odinga na Uhuru Kenyatta.
Kwenye ukurasa huu tutakupasha matukio kila yanapojiri hadi upigaji kura utakapokamilika mwendo wa saa kumi na moja jioni.
10:39 Mwandishi wa BBC aliye
mjiniNyeri anasema kila baada ya nyumba kumi kuna kituo cha kupigia
kura, wapiga kura wamejitokeza kwa wingi, baadhi ya mashine za tume ya
uchaguzi zilifeli lakini baada ya kushughulikiwa mambo yakarejea kuwa
sawa.
i
i
10:31 Mwandishi wa BBC mjini Eldoret Wanyama wa Chebusire
vituo vilifungua mapema mambo, yameenda shwari kwa ujumla wake, lakini
katika baadhi ya vituo, kumekuwa na mushkil , mashine ziligoma katika
kituo cha kupigia kura cha shule ya msingi ya UG, zaidi ya wapiga kura
elfu tatu , hadi sasa ni chini ya watu hamsini wamepiga
10:27 Mkuu wa tume huru ya uchaguzi Isaac Hassan
anahutubia waandishi wa habari kuhusu changamoto inazokabiliwa nazo
tyume hiyo. Isaac anasema vituo vilivyofungua kuchelewa, vitahakikisha
wapiga kura wote wamepiga kura
10:22: Ingawaje tume ya
uchaguzi IEBC inawakubalia watu wawasindikize wazee au wagonjwa kupiga
kura, wapigaji kura wengine wanawakataza kufanya hivyo. Mjini Kisumu
katika kituo cha upigaji kura cha Ukumbi wa Aga Khan, mwandishi wetu Ann Mawathe
dada mmoja alieyejipandikiza blanketi tumboni ili kuwahadaa watu na
akubaliwe kwenda hadi mwanzo wa foleni, alikatazwa kufanya hivyo na
wapiga kura wenzake.
Katika kituo hicho hicho, baba fulani aliyekuwa
amebeba kipochi cha mkewe aliyekuwa na mtoto mgongoni, naye alirudishwa
hadi nyuma kabisa ya foleni hiyo. Pia, mwanamume mwingine aliyejitwika
ufahari fulani kwa vile alikuwa kavalia suti, na kutaka kuruka foleni,
alikatazwa kufanya hivyo.
09:04 Waziri mkuu Raila Odinga
ambaye pia anagombea urais amepiga kura yake katika eneo la Kibera.
Amesema licha ya kupata habari za baadhi ya vituo vya kupigia kura kuwa
na hitilafu kidogo, wapiga kura wasiwe na wasiwasi kwani mambo yatakuwa
shwari
08:43 Mgombea wa urais wa muungano wa CORD, waiziri mkuu Raila Odinga anatarajiwa kupiga kura yake wakati wowote kuanzia sasa
08:30Solomon Mugera anasema kwamba kupiga kura kunachukua takriban dakika 12
08:25 Hassan Majid pia
mwandishi wa BBC anasema kuwa polisi wamepata mwili mmoja wa mtu
aliyeuawa na mwingine kujeruhiwa kwa kukatwa panga katika eneo la
Moshomoroni
08:24 Mwandishi wa BBC mjini Mombasa, Karen Allen
anasema kuwa polisi wamepata maiti za polisi wanne ambao wameuawa
katika eneo la eneo la Changamwe , Kaskazini mwa Mombasa. Hana taarifa
zaidi kwa sasa
yuko katika kituo cha Menengai mjini Nakuru kura
ilianza kupigwa saa moja asubuhi na foleni ni ndefu ingawa inakwenda
polepole mwendo wa kobe
08:15:Fatma Sanbur
yuko mtaani Kibera na anasema watu ni wengi sana lakini hakuna mbinu ya
kupanga foleni. Anasema watu wanapangwa kwa orodha ya majina na hata
baada ya saa moja tangu waanza kupangga foleni saa kumi na moja,
shughuli yab upigaji kura ilikuwa haijaanza
upigaji kura
unaendelea bila wasiwasi na kuwa wanatarajia shughuli itakamilika kwa
muda bila wasiwasi
07:28: Mgombea mwenza wa Uhuru Kenyatta, William Ruro amepiga kura mjini Eldoret
07:32: William Ruto anasema
kuwa anajivunia uchaguzi wa Kenya unafanyika kwa amani licha ya dukuduku
la wengi. Anasema anawataka wapinzani kukubali matokeo ya uchaguzi
vyovyote matokeo hayo yatakavyokuwa.
07:43 Upiga kura bado haujaanza katika baadhi ya
sehemu za Kenya. Wapiga kura wanalalamika kuwa katika vituo kadhaa
tarakilishi zimegoma na kwa hivyo watasubiri muda kabla ya kupiga kura
zao
07:47Eco Seyar
Papa akiwa mjini Nairobi anasema Wakenya wamejitokeza kwawingi jijini
Nairobi katika eneo la Dagoreti. Foleni zilianza kupigwa kuanzia saa
tisa usiku tangu kuanzishwa kwa demokirasia ncini Kenya watu waeneo hili
hawajawai kujitokeza kwa mapenzi kama inavyo onekana.
07:50 Mwandishi wa BBC Ann Mawathe yuko mjini Kisumu na anasema ameona foleni ndefu sana watu wakiwa hamasa kupiga kura. Wamepiga foleni tangu saa nane usiku.
07:52 Mombasa eneo la Kaloleni
mpiga kura mmoja amesema hadi kufikia sasa upigaji kura haujaanza kwani
maafisa wa tume ya uchaguzi bado hawajawasili na vifaa vyao
No comments:
Post a Comment