Thursday, March 14, 2013

"NATAMANI KUNYOA KIPARA MAANA SIPENDI KUSHIKWA SHIKWA"...AMANDA



MWIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Tamrina Poshi ‘Amanda’ amefunguka kuwa katika maisha yake hakuna kitu anachokichukia kama kushikwa nywele.
 
Akipiga stori na mwandishi wetu hivi karibuni, Amanda alibainisha kuwa kama ingekuwa ni hiari yake basi angenyoa hata kipara ili asipate usumbufu wa kwenda kushikwa nywele saluni.

“Kwa kweli mwenzenu sijui nipoje, sipendi mtu anishike nywele zangu... yaani sijui najisikiaje,” alisema Amanda ambaye ni mpenzi wa Mbongo Fleva  Joseph Rushahu ‘Bwana Misosi’

MWARICK JAPHET MUJUNGU Web Developer

ASANTE KWA KUTEMBELEA KING SELE BLOG KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI: E-mail.: mwarickit@gmail.com.

No comments:

Post a Comment