Moshi mweupe ulifuka katika mnarawa paa ya kanisa dogo la Sistina Vatican mjini Rome kuashiria papa mpya ameshapatikana.Hii ilikuwa jana usiku.
Maelfu ya watu walishangilia baada ya
kupata ishara hiyo kuwa papa mpya ameshapatikana.Huku kengele za kanisa
kuu la mtakatifu Petro na makanisa mengine huko Rome zilisikika.
Baada ya saa moja kupita ndio
ikafahamika mrithi wa Papa Benedict wa xvi ni Askofu mkuu wa Buenos
Aires nchini Argentina, Jorge Mario Bergoglio.
Papa huyu mpya amechagua jina la Papa Francis 1
Baadae alijitokeza kibarazani juu kuusalimia umati mkubwa wa watu.Papa mpya aliuomba umati huo kukaa kimyaa kwa muda kumuombea.''Naomba mniombee kwa Mungu ili anibariki''
Papa Francis amekuwa papa wa 266 mwenye miaka 76 papa wa kwanza asiyetoka barani Ulaya na watatu asiye muitaliano.
No comments:
Post a Comment