Mahakama
ya juu nchini Marekani imesikiliza hoja dhidi ya sheria inayowanyima
marupurupu ya serikali watu wa jinsia moja waliooana kisheria.
Majaji wanaosikiliza kesi hiyo walifuatilia kwa makini hoja kuhusu sheria ya kulinda ndoa inayojulikana kama DOMA.
Sheria
hiyo inaeleza maana ya ndoa kuwa kati ya mwanamume na mwanamke, kwa
maana kwamba wanandoa wanaume hawawezi kuomba wapewe baadhi ya malipo
kutoka kwa serikali.
Jumanne
wiki hii mahakama hiyo pia ilisikiliza hoja kama sheria inayopiga
marufuku ndoa kati ya wanaume katika jimbo la California, ni kinyume na
katiba.
Majimbo tisa ya Marekani yanatambua ndoa kati ya watu wa jinsia moja, huku 30 yakiwa yameipiga marufuku.
No comments:
Post a Comment