Kwa maelezo ya shuhuda,
inasemekana limeanguka saa moja asubuhi ambapo kwa muda huo kulikua na
watoto wa kihindi wanacheza mpira, kulikua na vibarua ambao wanataka
kumwaga zege kuendelea na ujenzi na ndio walikua wanabadilisha nguo
kuanza kazi.
Ni posta mtaa wa Indira Gandhi
pembeni ya msikiti mkubwa wa Itnasheri, lilikua ni gorofa la floor 12
ambapo mpaka sasa hakuna hesabu kamili ya vifo lakini shuhuda anasema
kwa muda mfupi baada ya kuanguka alishuhusia maiti nne.
Sehemu ya chini zinaonekana
bado nzima hazijadondoka ila kifusi cha kutoka juu ndio kimefunika
lakini kuna watu ndani yake wako hai na inaripotiwa wanapata hewa vizuri
na wamekua wakiwapigia ndugu zao na kuwaita waje kwenye eneo la tukio.
Endelea kuwa karibu na millardayo.com taarifa zaidi zinazidi kufatiliwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment