Korea
Kaskazini hii leo imesema inaingia katika hali ya vita na Korea Kusini,
katika muendelezo wa vita vya maneno dhidi ya utawala mjini Seoul na
Washington, baada ya kuwekewa vikwazo vya kimataifa kufuatia jaribio
lake la silaha za nyuklia.
Shirika
la habari la Korea Kaskazini KCNA, limetoa taarifa inayosema kuwa
kuanzia sasa, uhusiano wa Kaskazini na Kusini utaingia katika hali ya
vita, na kwamba maswala yote yanayojitokeza kati ya Kaskazini na Kusini
yatashughulikiwa ipasavyo.
Tangu
mwanzoni mwa mwezi huu Korea kaskazini imekuwa ikitishia kila siku
kuishambulia Korea kusini pamoja na kambi za kijeshi za Marekani, baada
ya Marekani na Korea Kusini kuanzisha mazoezi ya kawaida ya kijeshi na
imeyaamrisha majeshi yake kukaa kwa tahadhari.
Korea
kaskazini imetoa kitisho kipya kuishambulia Marekani, baada ya ndege
mbili za Marekani chapa B-2 zenye uwezo wa kubeba makombora ya nyuklia
kufanya mazoezi nchini Korea ya Kusini.
No comments:
Post a Comment