Mwanamke mmoja huko Oklahoma ameshitakiwa kwa kujaribu kuwauza watoto wake ili apate fedha za kumuwekea thamana mchu wake.
Polisi
katika mji wa Wallisaw wamesema mwanamke huyo Misty VanHorn
aliwasiliana na mnunuzi kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook.
Wamesema
mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 22 alikuwa akitaka dola 1,000 kwa
mtoto wake mwenye miaka miwili au dola 4,000 kwa mtoto wake mdogo mwenye
miezi 10.
Anadaiwa
kuandika katika face book akimuelekeza mnunuzi kuwa afike Sallisaw na
atamkabidhi mtoto pamoja na vitu vyake vyote na kumuachia moja kwa moja.
Mwanamke huyo mnunuzi ambaye hajajulukana anayeishi jimbo la jirani la Arkansas alitoa taari kwa mamlaka za jimbo hilo.
Polisi walifika eneo hilo na kumkamata Misty VanHorn mara moja.
Majirani
zake wamesema VanHom amekuwa akitembea mlango kwa mlango akijaribu
kuchangisha dola 1,000 ili kumtoa mwenzi wake kwa dhamana.
No comments:
Post a Comment